Mbio za uongozi CCM: Sumaye amuengua Nagu, Mama Salma Hana mpinzani Lindi, UWT Dar moto......

Hivi Mama Maria alikuwa naye M NEC ? Na Mama Mkapa je alikuwa nani ? Ama kweli CCM ina mambo mengi baada ya hapo watasema Chadema ya ukoo ?

swali zuri. hii ni ajabu, subiri kidogo utasikia Ridhiwani anagombea na miraji pia. ni vituko mno
 
Jana nimesoma kwenye gazeti kwamba Ridhiwani Kikwete ni mgombea pekee wa NEC huko wilayani kwao kwa maana ya kwamba anapita bila kupingwa. Leo Gazeti la mwananchi (kwenye habari inayomhusu Nagu)limeandika kwamba mke wa Rais Salma Kikwete ni mgombea pekee wa nafasi hiyo huko Lindi mjini! Sasa hii inamaanisha nini? iko wapi demokrasia ya kweli?? Nitahama chama wakati wowote kuanzia sasa
 
hahahaha mkuu umenichekesha sana wenyewe mnawaogopa mnategemea nini!
waambie wagombee ubunge waone cdm watakavyoingia huko!
 
haaaaaaaa, bado ulikua huko tu, una nasaba yoyote mbele ya jina lako ambayo inalandana na kiongozi yyeyote aliyepita?
Jana nimesoma kwenye gazeti kwamba Ridhiwani Kikwete ni mgombea pekee wa NEC huko wilayani kwao kwa maana ya kwamba anapita bila kupingwa. Leo Gazeti la mwananchi (kwenye habari inayomhusu Nagu)limeandika kwamba mke wa Rais Salma Kikwete ni mgombea pekee wa nafasi hiyo huko Lindi mjini! Sasa hii inamaanisha nini? iko wapi demokrasia ya kweli?? Nitahama chama wakati wowote kuanzia sasa
 
kwa mtu anayeijua vizuri tanzania, hashangai kwanini tuna umasikini wakutupwa wakati tuna rasilimali zote muhimu.Haya ndo majibu.... Salma kikwete awe kiongozi ili iweje? ana uwezo gani katika kuiletea nchi maendeleo? Lakini yote haya amesababisha JK. Kitendo cha mtu dhaifu vile kua rais wa nchi kume-encourage kila mtu kujiona anauwezo wa kua kiongozi.
Salma Kikwete hajakosa mpinzani sema watu ima wamehongwa au wameogopa ikulu. Salma ana nini cha mno zaidi ya kuwa mke wa rais kuweza kuwazidi wenzake? Ana elimu gani au usafi upi vya kupigiwa mfano kuwashinda wengine? Kwa vile CCM ni chama cha kifalme ambapo ufalme wa sasa ni wa Kikwete, Salma lazima apite. Hata kama Salma angempendekeza mbwa wake angeshinda kutokana na tabia ya woga na kujipendekeza vya wana CCM. Mara hii mmesahau zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM ambazo Nyerere alizikosoa?Huu ni ushahidi kuwa CCM haiko kwa ajili ya wananchi bali kikundi kidogo cha walaji wenye madaraka na tamaa ya madaraka. Ningekuwa Jakaya nisingemruhusu first lady kujiingiza kwenye siasa zisizo saizi yake. Ila tamaa haina macho wala hisia zaidi ya majuto.
 
Si kwamba Salma amekosa mpinzani-wanaopaswa kumpinga wameogopa ikulu. Zaidi ya kuwa mke wa rais Salma ana sifa gani ya kukosa mpinzani? Ana elimu au ujuzi gani? Kwa vile CCM ni chama cha kifalme lazima mke au mwana wa mfalme apite. Hii inachangiwa na tabia ya woga na kujipendekeza vya CCM. Ningekuwa Jakaya nisingemruhusu first lady kujiingiza kwenye siasa za aibu ambazo hazilingani na hadhi yake. Kwa vile tamaa haina macho wala mawazo zaidi ya majuto hili limewekekana hata kama ni aibu tupu. Lini atafanya kazi za umma na za chama? Anyway, kwa vile siku za CCM zimekwisha, acha watuonyesha ubovu na uovu wao zaidi.

riz1.mama riz1 na baba riz1 duu si nec ya familia hiyo?
 
Mama clinton vp! George bush Jr Vp! Katiba ya ccm haimzuii mke wa rais au mtoto wa rais kujihusisha na siasa. Ya dr. Slaa na kugawa ubunge wa viti maalum kwa mademu wake vp! Cdm mnaongozwa na chuki zilizopita kiasi
 
....Wakibadilishe jina tu na kukiita chama cha vikwete. Ana wadhifa mkubwa kama first lady lakini haukumtosha mpaka naye ajiingize kwenye siasa!!! Tamaa hizi mbaya sana!!!

CCM ni chama cha kifalme hasa katika muhula wa huu wa kikwete. Jana nilisoma gazeti moja kama sim tanzaniadaima ni mwananchi kuwa ridhiwani huko pwani kapita bila kupingwa hana mpinzani haya leo teno nasoma hapa salma kikwete lindi kapita bila kupingwa.

Jamani hata ukitumia akili fupi tu hivi kweli ujumbe wa nec unavyowapasua watu vichwa huko mawilayani watu waliokuwa wanasaidiana katika harakati za kisiasa leo ndo wapinzani katika kinyang'anyiro hiki eti wengine wamepita bila kupingwa na wote wana mahusiano na rais ambae ni mwenyekiti.

Washabiki wa Chadema wakati mwingine mnacoment mambo ya ajabu sana. Wengi wenu hamtaki Democrasia kwenye Chama chenu wakitokea watu ndani ya Chama wanaompinga Slaa huyo mtu ataitwa majina yote mabaya. Lakini ikitokea CCM mnalalamika kama siyo unafiki kama wa Sita.
 
....Wakibadilishe jina tu na kukiita chama cha vikwete. Ana wadhifa mkubwa kama first lady lakini haukumtosha mpaka naye ajiingize kwenye siasa!!! Tamaa hizi mbaya sana!!!

What a double standard?
Msipende kukariri mambo jamani
 
....Wakibadilishe jina tu na kukiita chama cha vikwete. Ana wadhifa mkubwa kama first lady lakini haukumtosha mpaka naye ajiingize kwenye siasa!!! Tamaa hizi mbaya sana!!!

Nakuunga mkono Mkuu. Nadhani hii ni taswira halisi ya Uswahili, Ulimbukeni na Inferiolity Complex. Huyu Bi mkubwa tayari ni Mama wa Taifa kutokana na cheo alicho nacho Mbaba. Haingii akilini tena akagombee nafasi za 'Ukarani' na 'Ukatibu kata' na kwa maana hiyo kuwazibia Nafasi wanawake wenzake ambao wangeweza kuishika!
Kaaz Kweli kweli.

  • Thanks
Reactions: BAK
Salma Kikwete hajakosa mpinzani sema watu ima wamehongwa au wameogopa ikulu. Salma ana nini cha mno zaidi ya kuwa mke wa rais kuweza kuwazidi wenzake? Ana elimu gani au usafi upi vya kupigiwa mfano kuwashinda wengine? Kwa vile CCM ni chama cha kifalme ambapo ufalme wa sasa ni wa Kikwete, Salma lazima apite. Hata kama Salma angempendekeza mbwa wake angeshinda kutokana na tabia ya woga na kujipendekeza vya wana CCM. Mara hii mmesahau zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM ambazo Nyerere alizikosoa?Huu ni ushahidi kuwa CCM haiko kwa ajili ya wananchi bali kikundi kidogo cha walaji wenye madaraka na tamaa ya madaraka. Ningekuwa Jakaya nisingemruhusu first lady kujiingiza kwenye siasa zisizo saizi yake. Ila tamaa haina macho wala hisia zaidi ya majuto.

Salma ana madudu kibao na WAMA yake. Si msafi hata.
 
du watu wanataaa sana mama salma wapi na wapi kwenye siasa au ndio membe anajipanga hivyo ila kwenye siasa watu wanamegana baba mkubwa angalie akitoka ikulu yasije yakatokea haya........ me yangu macho mwanae nae naona kapitwa bila kupingwa bagamoyo....haya bana me nalaumu kwa nini baba yangu akugombea urais
 
Jamani du bora nagu katoka nakingine nikatembeza rushwa zamatrekta za jeshi eti zake na kazuia wengine wasipate
 
Sidhani kama kunakiongozi yeyote wa CDM anaweza kusimama hadharani akalipinga hili kwa moyo wa dhati kama wafanyanyavyo wanazi wa CDM humu ndani

Lakini kwakuwa humu ndani uataonekana GREAT THINKER wa ukweli tu kama UTAPINGA CHOCHOTE kinachofanywa na CCM hata kama hakina mantiki kiasi gani, basi watu wataropoka watakavyo na kupeana like na sapoti za kumwaga utadhani hivi ndio vita vya ukombozi wa fikra vya mama salma kutumia haki yake kikatiba kugombea nafasi hiyo
 
wabunge wengine wasipoenguliwa pia kuwania ujumbe NEC mawilayani na uenyekiti wa mikoa kwa walioomba, nitaamini Sumaye kaanza rafu za urais 2015

Hakuna cha Sumaye kuanza rafu wala nini,ni kanuni walizojiwekea hawa magamba; kwavile huwa hawasomi na kuelewa pale wanapozipitisha ndio maana huwa wanakuja kushtuka wakati wa utekelezaji!! Unaona hata sheria bungeni huwa wanazipisha hovyo hovyo; zinapokuja kuanza kutekelezwa zinaonekana kuwa na mapungufu halafu wanazirudisha bungeni tena kuzibadilisha!! Hao ndio magamba halisi!!!!
 
ZeMarcopolo , nini kauli yako kuhusu hiyo kanuni iliyotumika kumuengua Dr Nagu? Imetafsiriwa inavyopaswa? kwa kuwa idadi ya wanaCCM wanaogombea nafasi hizo bila kujali uwepo wa kanuni hiyo, je unadhani kanuni hiyo imeelewa vyema miongoni mwa wanaCCM? Mhe Nnauye Jr najua huwa unapita humu unaweza kufafanua vizuri mambo haya hasa kanuni hiyo ilivyotumika kumuengua Dr Nagu.

Mkuu sana SMU tatizo ni mwandishi wa hii habari. Hiyo siyo kanuni ila ni mizani ya vigezo. Kinachofanyika ni kwamba chama kinajitahidi kurudi zaidi kwa wananchi kwa kuwa na wajumbe wa NEC toka ngazi ya Wilaya wakati hapo awali walikuwa wanaanzia ngazi ya mkoa. Sasa katika kufanya hivyo ukiacha nafasi hizo kuchukuliwa na mawaziri lengo kuu la kurekebisha katiba linakuwa halijafikiwa. Kanuni inatoa kipaumbele kwa wagombea ambao ni wakazi wa kila siku wa Wilaya husika. Its obvious kuwa Waziri atahitajika kuishi Dar es Salaam au Dodoma, hivyo basi akatazwi kugombea ila iwapo kutakuwa na wagombea waliokidhi vigezo zaidi yake basi anawekwa pembeni.
Ndio maana unaona mama Salma kaclose deal na wagombea "nje ya mahakama" kwa sababu na yeye kungekuwa na wagombea wakazi wa eneo husika wa kila siku ingebidi awekwe pembeni kwa mizani ya vigezo.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: SMU
....Ndio maana unaona mama Salma kaclose deal na wagombea "nje ya mahakama" kwa sababu na yeye kungekuwa na wagombea wakazi wa eneo husika wa kila siku ingebidi awekwe pembeni kwa mizani ya vigezo.
Dah siasa zina rafu sana....ha ha ha!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom