Mbio za Lowassa kuelekea 2010

lowassa is far much better than muungwana na ndio ambayo kidogo alifanya serikali ya JK ....mwaka wa kwanza wafikie mafanikio ambayo yamesimama ghafla especially mafanikio ya shule za kata kila kijiji ...ambayo hadi leo jk anayaimba ..its was lowassa"s baby...hilo halina ubishi...,na ukiondoa kasoro za lowassa ..basi lowassa is better kuliko jk hivi alivyo ....kwani kama utasema labda jk sio fisadi sana ..lakini lazima tujuwe sluggishness yake inaligharimu taifa kiasi gani....

Kuhusu kugombea kwa lowassa sioni kama ni issue kubwa kwani chama kitaamua ..yeye hajatamka tofauti na mtu kama JOHN MAGALE SHIBUDA ambaye yeye kashatamka rasmi interest yake.....

Wakuu zangu jamani mweee!.
Lowassa analindwa na JK kama anavyolindwa Mkapa, Rostam, Karamagi, Meghji, Kingunge na wengineo woote mafisadi wa CCM. Hii ni ilani kuu ya chama pamoja na kwamba haipo ktk maandishi..

Sioni kitu kikubwa kabisa ambacho anatendewa Lowassa ndani ya chama tofauti na wengine hadi hivi sasa kiasi kwamba tufikirie Lowassa anaweza kugombea urais kwa sababu tu anasafishwa ni kutoona mbali zaidi marefu ya mkono..

Hivi kweli watu mnaamini shule za kata ni kazi ya Lowassa toka anaingia Uwaziri mkuu hadi anaondoka kila siku ukifungua gazeti kuna cotoon za Lowassa mara atatuletea mvua za kisayansi, scandal za ndege kupaa, kufukuza kazi waajiriwa,majibu ya kihuni kwa ndugu yetu Mwanakijiji bado tu mnafikira huyu mtu ana nafuu zake kuliko JK ati kwa sababu JK analigharimu Taifa..Sasa ni lipi linatugharimu ambalo halikuwepo wakati Lowassa akiwa PM!

Ama kweli sisi - Miafrika Ndivyo Tulivyo!
 
Wakuu zangu jamani mweee!.
Lowassa analindwa na JK kama anavyolindwa Mkapa, Rostam, Karamagi, Meghji, Kingunge na wengineo woote mafisadi wa CCM. Hii ni ilani kuu ya chama pamoja na kwamba haipo ktk maandishi..

Sioni kitu kikubwa kabisa ambacho anatendewa Lowassa ndani ya chama tofauti na wengine hadi hivi sasa kiasi kwamba tufikirie Lowassa anaweza kugombea urais kwa sababu tu anasafishwa ni kutoona mbali zaidi marefu ya mkono..

Hivi kweli watu mnaamini shule za kata ni kazi ya Lowassa toka anaingia Uwaziri mkuu hadi anaondoka kila siku ukifungua gazeti kuna cotoon za Lowassa mara atatuletea mvua za kisayansi, scandal za ndege kupaa, kufukuza kazi waajiriwa,majibu ya kihuni kwa ndugu yetu Mwanakijiji bado tu mnafikira huyu mtu ana nafuu zake kuliko JK ati kwa sababu JK analigharimu Taifa..Sasa ni lipi linatugharimu ambalo halikuwepo wakati Lowassa akiwa PM!

Ama kweli sisi - Miafrika Ndivyo Tulivyo!

MKUU kama kweli Lowassa akirudi ubunge na serikalini, inabidi tumnunulie Nyani Ngabu zawadi kubwa. Kwani tutathibitisha ile kauli yake ya "Miafrika ndivyo tulivyo". Eddo ameprove kabisa kuwa hawezi kuwa kiongozi mkuu, uwaziri mkuu ulimshinda kabisa. Siwezi kukubali kuwa shule za kata aliweza kuziendeleza in two years, yote ambayo JK anajisifu nayo sasa hivi ni kazi ya Mkapa, Mkapa alikuja na mpaka uliokamili kuhusu elimu ambao una lengo la kufikisha elimu kwa kila mtanzania, kwanini kazi ya Mkapa na Sumaye credit apewe Lowassa.
Alipokuwa PM Lowassa alikuwa anafikiri hela na urais hakuna lolote alilofanya.
Kulikuwa na ujinga mwingi tu, kama ulivyosema kutukana watumishi wa serikali na kujaribu hata kuwakejeli wasomi wakati kwa taaluma zao, and now we are talking of his come back? Kwli ndivyo tulivyo.
 
Nauliza swali tu. Ni kwanini story yoyote mpya ya Lowassa inaunganishwa kwenye hii thread ya 'Lowassa anasafishwa'?? Nadhani hatuzitendei haki hizo stroy mpya. Nawasilisha.
 
Sidhani kama kuna ubaya mada zinazofanana kuunganishwa na hata mmi nashauri ile iliyowekwa kuhusu "Huyu Lowassa" ikawekwa humu baada ya kuchangamkiwa
 
Halisi,

Nilisema awali kabisa kuwa kosa pekee tunaloweza kumkamata nalo Lowassa ni Uzembe kutokana na hii Richmond, na zaidi tukitaka sana ni kutumia madaraka na kukiuka kanuni za kazi, jinsi Yona, Mramba na Mgonja walivyofanyiwa.

Lakini tofauti ni kuwa Lowassa, hawawajibishwa kwa uzembe wake wala kulitia Taifa hasara. Alichokifanya kwa kujiuzulu, kimechukuliwa kama adhabu tosha.

Sasa kwa sisi wengine ambao hupima mambo kwa undani, je haya yote ni changa la macho na tangu awali ilikuwa ni makubaliano yao hawa wawili kuwa Kikwete atawale kwa kipindi kimoja kisha amwachie Lowassa au imelazimika kukatisha safari ya Kikwete kwenda kipindi cha pili kutokana na kinachotokea sasa hivi nchini?

Kwenye thread yangu ya mgongano wa Katiba https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kumu-katiba-ya-tanzania-na-katiba-ya-ccm.html nimeuliza ikiwa CCM leo wataridhia kuwa Kikwete hawafai, wanaweza kumvua Uanachama na Uongozi kiurahisi na kuondokana na mfumo wa kiserikali ambao ungeshurtisha Bunge na Mahakama kuu zihusike.

Ni kutokana na udhaifu huu wa kuhakikisha kuna uwajibikaji na Kikwete kukosa Sauti na Mamlaka ndani ya chama, leo hii kina Sitta na Mwakyembe wanatapatapa na kupiga kelele za kuhujumiwa kutokana na haya ya kuonyesha kuwa Lowassa kajipanga vyema na yuko tayari kukichukua Chama mikononi mwake.

Mimi sisikitiki kwa linalotokea CCM, wacha litokee ili tuone sura za kweli za wale wanaodai wao ni Wanamapinduzi na wale wanaotuhumiwa kuwa ni Mafisadi.

CCM kumekuwa na upuuzi na ujinga tangu mchakato wa urais 1995. Na mbaya zaidi ni alichokifanya Mkapa 2005 kwa kufunika Demokrasia kwa ajili ya kutoa upendeleo na kulindana.

Kama Lowassa ataendelea na moto wake wa kutaka Urais ndani ya CCM, sitarajii kusikia Kikwete akisema ataendelea na kipindi cha pili.

Tetesi za kusema kuwa yeye ataondoka baada ya kipindi kimoja zitatimia hata kama sababu nyingine zinavumishwa ni kuhusu hali yake kiafya.

Swali ni jee, Wapiganaji wanajiandaa vipi kujibu hili? na nani kati yao yupo tayari kugombea kumpinga Kikwete hata kama Lowassa hatachukua fomu?

kwani mkulu anasumbuliwa na nini jamani? mpaka hata waje wavumishe kwamba afya yake siyo nzuri.
 
Lowasa alishakataliwa na Mwalimu tangu zamani kama si JK mbona kuna wana CCM wengi tu na wenye uchungu na TZ....Please for goodness sake tunataka Rais ambaye anaweka maslahi ya Taifa mbele siyo yake
 
Sidhani kama kuna ubaya mada zinazofanana kuunganishwa na hata mmi nashauri ile iliyowekwa kuhusu "Huyu Lowassa" ikawekwa humu baada ya kuchangamkiwa
 
EL anaumiza vichwa vya waTZ balaa yeye yupo kimyaaaaaaa anawaangalia tu mnavyo kuja mara hili mara lile yeye anakula maisha tu.
 
Lowassa wenyewe amaekanusha kwenye moja la magazeti mama kuwa hajasema nia yake ya kugombea uarais na wala hata gombea .

suala si kupitishwa na Chama chako ndio uwe rais,suala unauzika kwa wananchi?na sisi wananchi ndio tuna maamuzi ya mwisho wa kuamaua nani awe rais wetu. na si chama!!!!!!!!!!!!!
 
Hakuna kanusha wala kukataa, bali alisema kuwa hajasema kuwa hatagombea au atagombea, soma mwananchi ya leo

walafi wa madaraka huto kauli kama hizi
 
kwani mkulu anasumbuliwa na nini jamani? mpaka hata waje wavumishe kwamba afya yake siyo nzuri.

Kikwete anaumwa, hapa kuna mambo ya privacy za ugonjwa, wanasema si ngoma lakini somewhat equally serious.
 
Kikwete anaumwa, hapa kuna mambo ya privacy za ugonjwa, wanasema si ngoma lakini somewhat equally serious.

asante kwa info mkuu.
ugonjwa wa mkulu ukemewe kwa nguvu zote za bwana, ni bora apate hata yule shibuda,huyu lowassa amekaa kihasira hasira tu.
 
Lowassa awaonya wanaomgombanisha na Kikwete



WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amesema, hana mpango wa kuwania urais wa Tanzania mwakani.

Mbunge huyo wa Monduli amewaonya wanaotaka kumkosanisha na Rais Jakaya Kikwete na kusema ataendelea kumuunga mkono kiongozi huyo.

Lowassa amesema leo kuwa,zipo dalili kuwa kuna watu wanaotaka kuvuruga uhusiano wao wa kirafiki na Rais, kwa kuzusha mambo ambayo hata yeye hayafikirii.

Amekanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti la Jumapili iliyopita (si HabariLEO)kwamba vikao vya juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) vinaweza kumsimamisha kama mgombea pekee wa chama hicho kwa madai kuwa nafasi ya Kikwete kusimamishwa haitabiriki.

Lowassa amesema,yamesemwa mengi ameyavumilia,lakini hili la kutaka kumkosanisha na rafiki yake limemuuma.

Kwa mujibu wa Lowassa, urafiki wake na Kikwete ni wa muda mrefu hivyo hana sababu ya kutaka kuuvuruga kwa sababu ya madaraka.

"Urafiki wetu ni wa tangu chuo kikuu (cha Dar es Salaam)... katika siasa pia, kwani mwaka 1995 tulikubaliana tukaenda Dodoma kuchukua fomu za urais tukiwa pamoja, kwamba akipata mmoja ni sawa tu na amepata mwingine.

"Hatukuishia hapo, ilipokuja mwaka 2005 nikaamua kumpisha mwenzangu kwani namwamini ana uwezo, nami nikamuunga mkono na kuendesha hata vikao vyake vya kampeni... nitaendelea kumuunga mkono huyu," amesema.

Amesisitiza kwamba,yeye na Kikwete hawakukutana barabarani na hivyo hatakubali wavurugwe barabarani kama baadhi ya watu wanavyotaka iwe.

Mwanasiasa huyo amebainishwa kwamba,amekuwa akiwasiliana na Rais Kikwete mara kwa mara, ana kwa ana na hata kwa simu.

"Tunakutana na Rais kama marafiki mara nyingi tu, mara zingine tunatumiana text (ujumbe wa simu) sasa leo kitoke wapi cha kunifanya mimi niamue kupambana naye katika urais mwakani?," amehoji Lowassa.

Amewatahadharisha wana CCM wenzake kuepuka watu wanaotaka kupotosha kwa kutumia ajenda zao za kisiasa, kwa sababu wanafahamu kwamba wasema uongo lakini wanaendelea kuukumbatia.

Amempongeza Rais Kikwete kwa kutekeleza Ilani ya CCM kama inavyotakiwa, na akasema anafahamu kwamba kwa utaratibu wa CCM kupata viongozi wake wa juu ni kumwachia mtu amalize vipindi vyake viwili vya miaka mitano mitano.

Amesema, amekuwa kimya kwa muda mrefu kwa sababu hakuona sababu ya kujibu kila linalosemwa, lakini yeye ni binadamu hivyo ana hisia za maumivu hasa anapoona watu wanazidi kuupotosha umma.

"Mimi kwa kipindi chote hicho tangu nijiuzulu, Februari 2007, nimekuwa jimboni mwangu Monduli nikishughulikia matatizo ya wapiga kura wangu na hivyo sikuona sababu ya kuanza kujibizana... lakini waelewe nina imani na Kikwete," amesema Lowassa.

"Watu wanadhani mimi kukutana na Watanzania wenzangu hawa basi nawania urais, huku ni kupotosha watu nanawaomba wenye fikra hizo waachane nazo kabisa... wajue tu kuwa mwakani nitaendelea kuwa na Kikwete, tuache majungu tuhudumie wananchi wetu inavyopasa," amesema.

Lowassa alijiuzulu kwa kuwajibika katika mkutano wa Bunge Februari mwaka juzi kutokana na kashfa ya mitambo ya kufua umeme wa dharura maarufu kama Richmond, na muda wote huo amekaa kimya huku wapinzani wake wakitumia magazeti kuandika kuwa anawania urais mwakani badala ya Kikwete.
 
Halisi,

Naona Lowassa kakanusha hizo habari; mimi ningemwona ni mjinga kweli kweli kama angekuwa anafikiria kugombea 2010. Kwa siasa za TZ ninavyoziona mimi Lowassa anamhitaji sana JK kuliko JK anavyomhitaji Lowassa. Naamini Lowassa angependa kurudi serikalini baada ya uchaguzi wa 2010, hivyo hawezi kumuudhi mtu ambaye anaweza kumsaidia kufanikisha hilo.

Pia hii habari ilivyoandikwa unaona tu kama imeandaliwa na wabaya wa Lowassa. Sio mjuzi wa mambo ya habari lakini kwa jinsi siasa za TZ zinavyoenda sasa unaweza kuanza kupata idea jinsi waandishi wetu wanavyotumika kuchonganisha/kupamba baadhi ya wanasiasa.

Kinachotokea sasa wanasiasa wote wanataka kujikomba kwa JK. Ndio maana kila mmoja wao anafuatilia kila neno dogo analolisema JK.

Binadamu kama unatetea haki au unapinga maovu huhitaji kufuata upepo. Mapambano ya CCM dhidi ya uhalifu ni ya kufuata upepo na ndio maana wengine tunayaita mapambano ya usanii.

Mtu anayefikiri kuna mtu wa maana atajitokeza mwaka 2010 kumpinga JK mimi nitamwita ni mtabiri au hajui siasa za CCM zinavyoendeshwa. Hakuna waziri hata mmoja ambaye atampinga JK 2010.


Kwamba naiamini ama siiamini hii habari, ni mjadala mrefu na mpana maana sijui chanzo chake halisi cha aliyeiandika. Jambo la msingi ambalo ninaweza kuwa nakubaliana nalo ni kwamba EL anautaka URAIS, ni lini na kwa njia gani hilo nalo sijui.

Kwamba Lowassa hawezi kuwa Rais wa Tanzania, nalo siwezi kupingana na wewe ama kukubaliana nawe moja kwa moja maana nao ni mjadala mrefu sana kwa mazingira yetu ya sasa. Kuna vigezo vingi vya kuangaliwa na vyote vinaweza kuwa vya kufikirika maana lolote linaweza kutokea.

Kuhusu habari hii kuandaliwa na wanaompinga Lowassa, hilo naweza kupinga japo si kwa asilimia 100. Nina sababu nzito ambazo baadhi ya wahusika watakubaliana na mimi, na zaidi waandishi wa habari wenye kujua vyumba vya habari vya Tanzania vinavyoendeshwa ikiwamo Tanzania Daima Jumapili. Ni mjadala mrefu na mpana tupeane nafasi tusiubane.
 
Kigogo, naungana mkono na wewe kwa jambo moja kuwa hakuna tatizo mtu yeyote kugombea urais wa nchi hii. Jambo la msingi hapa ni je Mh. Lowasa anawafaa watanzania kwa kipindi hiki ambacho wamegubikwa na wimbi la umasikini kwa sababu ya watu wachache wanaopola mali za nchi? Tunapojadili maada hii tuache ushwaiba au ushabiki wa chama, tuangalie kama huyo mtu ana mwelekeo wa kuwakomboa watanzania kama rais wa nchi. Lowasa alikuwa msaidizi wa karibu wa Kikwete, je katika uongozi wake watanzania wamenufaika vipi? What if tukimpa nchi, nini hatima ya nchi yetu? Lowasa ni mchapa kazi sana lakini....Nikiri pia kuwa Mh. Lowasa anautaka urais kwa nguvu zote. Kazi kwake ni pale Mh. Kikwete atakaposema anaitaka awamu ya pili. Pamoja na nguvu aliyonayo Lowasa bado Kikwete ana nafasi kubwa ya kuteuliwa hasa ukizingatia kuwa yeye ndiye mwenyeketi wa chama.
 
Lowasa hafai hata kuwa katibu kata wanao mtaja eti anataka kugombea urais ni wanahabari wakurupukaji.kashfa zote bado kuna watu wanafikiri Lowasa ni mjinga kugombana na muungwana.

Muungwana anamlinda sana Lowasa asipelekwe Kisutu na Lowasa anajua hilo.katika mazingira ya kawaida si rahisi mtu anayekulinda ukorofishana naye.

Lowasa ameshapotea katika ramani ya siasa za Tanzania hana wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu yeye mwenyewe kwa kukataa kujibu hoja za tume ya mheshimiwa Mwakyembe pale mjengoni.Anapoteza muda na fedha nyingi alizotuibia kujisafisha na kujijenga upya kisiasa wote wanaowekeza kwa Ngoyai wataishia kuaibika na kuangamia kisiasa muungwana ni mjanja tayari keshagundua hilo hataki kabisa kujinasibu na wanamtandao mafisadi.
 
Back
Top Bottom