Mbinu za kukuza mahusiano baina ya watu

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,453
3,203
Chanzo: www.wilguy-jibebe.blogspot.com.

Mahusiano baina ya mtu na jamii yake ndiyo yanayomfanya mtu au afanikiwe au asifanikiwe. Mahusiano baina ya mtu na mtu hutegemea uwezo wa mtu husika kushirikiana na jamii yake, kushirikiana kunakojengwa na kutegemeana na si kutegemea.

Ili kuboresha mahusiano, yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:


a) Upendo.
Ili mtu apendwe anapaswa kujipenda kwanza; kujipenda huanza kwa muonekeno wa ndani na kisha wa nje. kujipenda na kuwapenda watu wengine huonekana machoni mwa watu kupitia mienendo. Mtu anayewapenda wenzake hujitahidi kutoa msaada wa hali au mali ili wenzake watimize malengo yao.

b) Kukumbuka majina.
Mtu anapowataja watu anaowasilina nao kwa majina, au kueleza jinsi anajua kule watokako huwatia watu faraja; kuwafanya wote wajione ni jamii moja, pia kuwafanya watu husika kujiona ni muhimu (wanathaminiwa) miongoni mwa jamii.

c) Kukubali juhudi za watu.
Kukubali matunda (matokeo) ya jitihada za watu wengine; kwa kuzipa thamani au ubora unaotakiwa hudhihirisha harakati za watu na kuwafanya waongeze matumaini na juhudi.

d) Kusikiliza kwa makini.
Kusikiliza ni bora zaidi ya kuongea katika nyakati nyingi. Mtu hudhihirisha kwa kiasi gani habari yake ianavyoungwa mkono kwa kadiri anavyosikilizwa. Hivyo kukuza hekima na uelewa wa msikilizaji. Baada ya kusikiliza/ kusoma mtu anapaswa kujibu kwa kadiri ya hekima na dhamira yake.

e) Kuruhusu hisia za watu.
Kuruhusu hisia, mtizamo au mada kutoka kwa mtu/watu zijadiliwe humfanya mtu/ watu kuzungumza kwa uhuru juu ya kufanikiwa na chanagamoto zake. Hivyo kumfanya mtu/ watu kuifurahia uhusiano wake na jamii yake.

f) Kutia moyo.
Kuwatia moyo watu ambao hawajafanikiwa kiasi cha kuridhisha hutoa ahueni kwa mtu husika. Yafaa kuwatendea watu kadiri ya mtu anavyotaka atendewe. Kuwatakia watu heri husaidia kupunguza mawazo na kauli za kurudisha nyuma.

Kwa makala kama hizi na nyinginezo, tembelea www.wilguy-jibebe.blogspot.com kila mara, soma na toa maoni yako ili kujenga MUSTAKABALI WETU.
 
Back
Top Bottom