Elections 2010 Mbinu za kudhibiti Mawakala wa CHADEMA

Ngisibara

JF-Expert Member
Jan 2, 2009
3,301
2,076
Kutokana na uzoefu tulioona katika uchaguzi wa 2005 na chaguzi ndogo zilizopita ni wazi kuwa CCM hushinda kwa uwizi, ujanjajanja wa mabox ya kura au kula njama na mawakala uchwala wenye njaa kali ambao hujifanya ni wakereketwa wa Chadema kumbe wao huomba uwakala ili tu wapate mshiko kutoka Chadema, hebu angalia kule Busanda mawakala walivyouza chama kwa kusaini ripoti mbili na kuishia porini, Hivyo wakereketwa wa Chadema mliopata bahati ya kuwa mawakala au kuwa na rafiki zenu wanaojua mbinu hizo hebu tujadili ni zipi? na ni jinsi gani tufanye kudhibiti upuuzi huu wa CCM, Mwaka huu kuna dalili nzuri kabisa kuwa majimbo mengi yataenda Chadema lakini mafisi haya yalivyo na njaa kali safari hii siamini kabisa kama tutapona na tayari tumejionea jinsi walivyokulana wao kwa wao kwenye kura za maoni bila chembe ya aibu, labda mie nianze kwa kusema kuwa kuanzia wakati huu Mawakala wawe screened uaminifu wao kwa chama halafu itakapofika wakati tusiokoteze okoteze mitaani kama dharula, tuwe nao tayari na tuwawezeshe katika kipindi chote cha kupiga kura na kuhesabu, na pia wawe wanacommunicate na viongozi mara kwa mara kujulisha nini kinaendelea na kama kuna tatizo basi wasaidiwe haraka kwani hili linawezekana kwa kutumia simu za kiganjani zipo nyingi siku hizi......nawasilisha tuchangie ndugu zangu wa Chadema tu na si vinginevyo
 
Point noted, lakini pia nawasiwasi simu siku hiyo zikawa busy kila wakati yaani mawasiliano yakawa hakuna kabisa! hivyo basi ni bora tukajua plan B hata plan C kama kuna hilo likitokea.
 
mimi nadhani kwa vile wanafunzi wengi wa vyuo vya elimu ya juu wapo rikizo na ndo mtaji mkuu wa chadema watafutwe au makada wa CHADEMA walio rikizo watumike ipasavyo kulinda kura zetu
 
Ni nani anachagua mawakala ni chama au mgombea? Kama ni mgombea ni utaratibu mzuri anaweza kuchagua watu anao waamini.
 
Kwanza ni kwa watu wenye uchungu na nchi kujitolea kuwa mawakala kwa gharama zao wenyewe. Kwa wale wenye kazi zao na hawategemei uwakala kwa kipato ni rahisi kusimamia ukweli kwani ni zoezi la siku moja tu. Mimi ntawasiliana na viongozi wa Chadema waniweke kusimamia Kura mana sina shida na 10,000 za CCM.
Wengine tufuate nyayo, na tuwaombe rafiki zetu tunaowajua nao wajitolee ili Chama kitumie Hela itakazokusanya sehemu nyingine kwa kulipa vizuri mawakala huko vijijini!
 
Hutakuwa peke yako mkuu Mozze.
Binafsi nitajitolea tena bure, thamani ya ukombozi unaohitajika ni kubwa sana kuliko hako kaposho ka elfu kumi
 
CHADEMA ikifikia ukomavu wa kuwa ni chama cha siasa na si vuguvugu la wananchi hapo hawatahofu juu ya mawakala kwani hawa watakuwa ni watu waliolelewa katika maadili ya chama hivyo hakuta kuwa wasiwasi kama watawasaliti.
 
mimi nadhani kwa vile wanafunzi wengi wa vyuo vya elimu ya juu wapo rikizo na ndo mtaji mkuu wa chadema watafutwe au makada wa CHADEMA walio rikizo watumike ipasavyo kulinda kura zetu

good Point with Minor corrections!. Likizo
 
Mimi niko tayari pia kusimamia. Sihitaji kulipwa Chochote. Kwa upande wa Rais ni vigumu sana kuweza kuchagua wasimamizi mwenyewe sababu ya ukubwa wa nchi na vituo vingi. nakubali kuwa zoezi hili linatakiwa kufanywa mapema. Mnyika anapaswa kulichukua hili na kulifanyia kazi haraka na kutupatia majibu ili tujue namna ya kujipanga. Ngisibara, ahsante kwa mawazo mazuri.
 
Hutakuwa peke yako mkuu Mozze.
Binafsi nitajitolea tena bure, thamani ya ukombozi unaohitajika ni kubwa sana kuliko hako kaposho ka elfu kumi

Je, taa zikizima? Je, wakienda kunywa chai? Je, wakipata njaa? Je, wakipewa dau kubwa? Mbona wabunge na madiwani kadhaa wamesaliti?
 
Kuna watu wengi wazalendo na wana mioyo ya kujitolea, kwa gharama zao... Je, Mawasiliano yatakuwaje kupanga mikakati?
 
Mnaosema mnajitolea kuwa mawakala je mlihudhuria mkutano wa FOS juzi j'mosi pale Hoteli ya Land Mark au almradi mtu kasema anajitolea hata kama yuko Denmark, kwa taarifa yenu mipango ya mikakati inaendelea.
 
Back
Top Bottom