Mbinu ya kupunguza uzito kwa haraka

Nina kilo zinaelekea 66, kwa umri wangu nadhani natakiwa niwe na kilo 50 hivi nadhani hiyo ya kuruka kamba itanisaidia kushuka, lakini mtoa mada unaweza ukafafanua kidogo mazoezi ya kupunguza tumbo ni kama yapi maana yako mengi nayo. Wewe unashauri yapi labda?
Natanguliza shukrani.
 
Watu wengi tunataman kupungua ila hiz njia za kutufanya tupungue ndio hatar
 
Nina wasiwasi hapo kwenye kunywa juice ya kabichi mana kuna watu matumbo yetu ni kamavkichekecheo.
Unywe halafu tumbo lijae gesi au livuruge shughuli yake utasimulia mana kama si kuharisha ni mwendo wa kuachia mashuzi tu.
Kabisa na kama una mtungi wa gesi unganisha pipe mpaka asbh utakuwa umeujaza,tayari kwa matumizi ya nyumbani. Kila kitu kinafaida
 
Hapana nilisha jaribu
Hahaha pole ,kama unataka anza tena utatoboa tu
Kupungua unene usitegemee kupungua siku moja au mbil
Unatakiwa uwe mvumilivu matokeo unayaona kuanzia mwez mmona na kuendelea ukiwa very serious
 
Nina kilo zinaelekea 66, kwa umri wangu nadhani natakiwa niwe na kilo 50 hivi nadhani hiyo ya kuruka kamba itanisaidia kushuka, lakini mtoa mada unaweza ukafafanua kidogo mazoezi ya kupunguza tumbo ni kama yapi maana yako mengi nayo. Wewe unashauri yapi labda?
Natanguliza shukrani.
Kinachoangaliwa siyo umri bali Urefu wako....uzito wako no sharti uendane na urefu wako na si umri
 
Jamani mimi si nitakufa kwa njaa, kama huyo samaki labda nimle mzima mpaka nishibe.:p
 
Watu hawajugundua tu, mimi ni shahidi, mmea wa mlonge unasaidia saana, yaan mimi ndani ya mwezi, katambi kimeisha, demu wangu pia, katambi kimeisha,pia tumekuwa na yangi nzuri ya mng'ao mwili mzima. Yaan mtu anae tufahamu lazima atuulize tunatumia nini. Nilichogundua kuhusu mmea huu ukinywa juice yake lazma usikie kiu saana hivo utalazimika kunywa maji kwa wingi,ambapo kutokana na hayo maji ndio matokeo ya ngozi nyororo. UTI utaisikia kwa jirani.
 
Kinachoangaliwa siyo umri bali Urefu wako....uzito wako no sharti uendane na urefu wako na si umri
Body Mass Index(BMI) unachukua weight(kgs) divide by Height Square in Mita times 100 Recommend hapo ni 20-25% ikizid hapo au kupungua ni tatizo unatakiwa uwe katika hiyo range
 
Njia nyingne ya kupunguza uzito ni kunywa maji kabla ya kula hiyo itasaidia kula chakula kidogo kwasabb tumbo limejaa maji
N.B kutokula mlo kamili au kutokula kabisa sio njia nzuri ya kupunguza uzito unaweza pata matatzo kama ulcers au kupunguza kiwango cha sugar in your body
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom