Mbinu mpya wa wezi

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,524
863
Sent: Friday, 20 January 2012, 8:02
Subject: UHALIFU MPYA - KAA CHONJO


Wandugu,

Nimepata pepe hii toka kwa rafiki mmoja. Sina sababu ya kutoamini au kutilia shaka tarifa hii kuh "ubunifu" huu wa vibaka. Jihadhari.

KUMEZUKA WIMBI JIPYA LA UHALIFU, HII IKO NAMNA HII:-

UNAKUTA MFUKO WA NYLON( MAARUFU KAMA MIFUKO YA CONDOM,RAMBO,PLASTIC) BARABARANI . UKIUKANYAGA TU LAZIMA UTAPATA PUNCHER MAANA NDANI YAKE KUNA KIBAO KILICHOPIGILIWA MISUMARI ZAIDI YA UNAVYOFIKIRIA WEWE. UKISHUKA GARINI KUANGALIA KULIKONI WIMBI LA VIBAKA LINAKUVAMIA NA HAKUNA UTAKACHOBAKIA NACHO ZAIDI YA GARI MAANA LITAKUWA HALINA UPEPO BAADHI YA MAGURUDUMU.VIBAO NI VINGI KWA UMBALI MFUPI MFUPI.

HII IMETOKEA JANA TABATA KISUKURU MAENEO YA MAKOKA MIDA YA SAA TATU USIKU. WALIOPATA PUNCHER NI PAMOJA NA MKE WANGU NA MAGARI MENGINE KIBAO, WALIOLIFANIKIWA KUIBIWA SIJAPATA TAARIFA BADO ILA TULIJI-ORGANISE NA KUPITA NJIA ZOTE NA KUVUKUSANYA.


WATAKUPIGA KIASI GANI HIYO INATEGEMEA KIWANGO CHA BANGI WALICHOVUTA NA UNAJEURI KIASI GANI.

TAHADHARI.

USIKANYAGE MFUKO WA NYLON ( KWEPA).

UKIKANYAGA BAHATI MBAYA JIANDAE VYEMA KABLA YA KUSHUKA GARINI AU TEMBEA NA PUNCHER UMBALI KIDOGO.

MTAARIFU NA MWENZAKO.
 
sasa ulivyosema "ukikanyaga"nkadhani hadi si watembea kwa mguu inatuhusu kumbe wenye mandinga tu poleni
 
Asante kwa taarifa Mkuu, nitapitia Ubungo kununua yale mapanga ya kukatia kucha, nikipata hiyo dharura nashuka nalo, atakayenifuata nguvu zangu zitaishia kwenye kucha zake.
 
haya majamaa yana mbinu nyingi sana arroo!!!borra tumejua na hii lakini najua zipo nyigi tu mkuu,hivyo kuibiwa kupo pale x2
 
sasa ulivyosema "ukikanyaga"nkadhani hadi si watembea kwa mguu inatuhusu kumbe wenye mandinga tu poleni

duhu, huyu jamaa kanishitua. kumbe inawahusu famila bora, wacha mgawane kipato japo mara moja kwa mwezi sio mbaya sana
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom