Mbinu chafu za UKAWA kuhujumu wakuu wa wilaya zafichuka

Omary Kipingu

Member
Feb 22, 2016
40
48
MBINU CHAFU ZA UKAWA KUHUJUMU WAKUU WA WILAYA ZAFICHUKA.

Siku chache zilizopita kumetokea tabia ya kushambuliwa kwa maneno kwa baadhi ya wakuu wa wilaya kupitia vyombo vya habari ikiwemo magazeti yakionesha picha mbalimbali za wakuu wa wilaya na kuwakejeli, lakini pia baadhi ya wabunge na mameya na viongozi wengine wamekuwa wakionekana kuwakshfu na kuwadhalilisha wakuu wa wilaya. Hali hii ilishika kasi baada ya Rais kuonesha dalili za kuteuwa wakuu wa wilaya hivi karibuni. Wakuu wa wilaya kikatiba ni wawakilishi wa rais kwa ngazi ya wilaya na ndio wenyeviti wa usalama wa wilaya, kifupi ndio viongozi wakuu ngazi ya wilaya.

Katika uchunguzi uliofanyika wakuu wa wilaya wanaoandamwa sana ni Mh. Paul Makonda (Kinondoni) na Mh. Peter Kasesela (Iringa). Wiki iliyopita mbunge wa iringa Mh. Msigwa (CHADEMA) ameonekana akimkashfu mkuu wa wilaya kwa maelezo kuwa anaingilia kazi zake, lakini pia siku chache baada ya msigwa kumkashfu mkuu wa wilaya, tumemsikia pia meya wa Kinondoni Boniface Jacob (CHADEMA) akimkashfu mkuu wa wilaya kwa maelezo yale yale kwamba anaingilia majukumu yake.

Swali la kujiuliza;

kwanini wanaowakashfu wakuu wa wilaya wawe viongozi wa CHADEMA TU? Na pia kwanini waje na sababu moja tu ya kuingiliwa majukumu yao?? Je hapo mwanzo walikuwa hawaingiliwi majukumu yao?? Pia kwanini wale wakuu wa wilaya wanaoonekana wanawajibika sana na kuendana na kasi ya Rais ndio wanaoandamwa?? Je hakuna agenda ya siri hapa kwa Ukawa juu ya serikari ya awamu ya Tano?? Je, hii sio hasira ya uchaguzi baada ya CCM kushinda na UKAWA kushindwa?? Katika uchunguzi wa kina wa wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kisiasa wameonesha kuwa hali hii inatokana na CHADEMA kukosa mbinu mbadala ya kukubalika tena kisiasa na hii imetokana na Rais Magufuli kukubalika sana kwa jamii kuliko mwanasiasa yeyote katika kipindi hichi, hali inayowatisha UKAWA kuwa wanaweza poteza ushawishi wa kisiasa na kushindwa vibaya uchaguzi ujao 2020. Lakini pia imegundulika kuwa UKAWA wamekutana katika vikao vya siri chini ya Mwenyekiti wao Mh. Freeman Mbowe na kukubalina kutumia mbinu hii ya kuwashughulikia wakuu wa wilaya ili kudhoofisha serikali ya awamu ya tano, hali hii imethibitika pale viongozi wa Ukawa wakianza ziara za kimya kimya mikoani kuanzia wiki iliyopita ili kuwachafua viongozi ngazi za wilaya. Juzi tu Mwenyekiti wa Chadema alienda Bukoba nako alianza kukosoa utendaji wa mkuu wa wilaya na wakurugenzi na kuonesha hawafai akishirikiana na Mbunge wa Bukoba Mh. Rwakatale.Huu ndio mkakati walionao sasa UKAWA juu ya serikali ya awamu ya Tano.

Rai yangu;

Chadema watafute mbinu nyingine kwani mbinu hii imeshajulikana na itawapotezea kabisa nguvu ya kisiasa kwa viongozi wao waliobahatika kupata nafasi mbalimbali ikiwemo ubunge na umeya. Pia Chadema watambue kuwa siasa ya kusubili makosa ya mwingine upate umaarufu imepitwa na wakati, wasipolijua hilo watapotea kabisa kama TLP.

Pia , wakuu wa wilaya wasikatishwe tamaa na maneno ya wakosoaji, kwani ukiona watu wanakusema sana ujue wanatambua mchango wako, kwa hiyo wanachotakiwa kukifanya ni kusimamia ilani waliyopewa ya CCM ambayo ndio anayoisimamia Rais Magufuli na lazima wajue wanatakiwa waendane na kasi ya Rais ili wasije kuwa mizigo kwa serikali hii.

Mwisho;

Siasa sio uadui , tusitumie siasa kubomoa nchi yetu kwani hakuna haja ya kugombania fito wakati tunajenga nyumba moja. Tusitafute sifa nyepesi kwa kutumia kashfa kwa viongozi wengine, zama hizo zishapita, sasa kazi zako na uwezo wako kuwatumikia wananchi ndio utakubeba sio matusi na kejeli.

By Omi K.

Mkulima.
 
Mkuu kwani ww hata nyumbani kwako na mkeo si mna majukumu mmepeana?sasa ikitokea humuendi sawa kwenye hayo majukumu huoni tatizo?ma-DC na viongozi wengine wote ni busara kutambua majukumu yao ili kuepuka huo kuingiliana kwenye utendaji.
 
Wakuu wa wilaya ndiyo wanafanya kampeni chafu dhidi ya wabunge wa ukawa,hilo lipo wazi.Ulichoandika ni pumba tupu.DC wa iringa ni hovyo kabisa ndiyo maana hata ubunge amekosa miaka yote JK akaamua kumhifadhi huko
 
vyama vya upinzania afrika havina mchango wa kuijenga afrika bali ni kudidimiza bara hili na mataifa yake sababu kubwa ni kuwa vyama hivi vinasubiri tatizo litokee ndio navyo vipate gia ya kupandia kwenye umarufu wa siasa, haiwezekani mkuu wa wilaya anajituma ufanya kazi na majukumu ya kuwakomboa watu wa kutoka kwenye wilaya yako halafu unasema unaingiliwa hali ya kuwa tatizo limekuwepo na hata haujataka kutatua na akija mwingine kutatua na unasema unaingiliwa aibu kubwa vyama hivi kwenye utawala magufuli ndo vitayumba sana maana havina hoja ya kusimamia badala ya kuhimiza serikali kuanza kujenga viwanda na kuwaonesha watawala faida ya kuwa na viwanda mnaanza kukimbizana na wateule wa Rais tena huku mkiwatukana matusi kiasi kwamba hawa si watanzania aibu kubwa sana , mie huwa nasema kuwa afrika tunasumbuliwa na UBINFSI NA UJINGA ULIOTOTEA ndo unaotusumbua na kutupeka kwenye umaskini mkubwa
 
Wapin
Wakuu wa wilaya ndiyo wanafanya kampeni chafu dhidi ya wabunge wa ukawa,hilo lipo wazi.Ulichoandika ni pumba tupu.DC wa iringa ni hovyo kabisa ndiyo maana hata ubunge amekosa miaka yote JK akaamua kumhifadhi huko
vyama vya upinzani kwa afrika ni makundi ya wahuni tu wala siyo viongozi wa kutumikia watu hawafai kwa lolote lile.
 
Kwa hiyo wakuu wa wilaya wakikosea wasikosolewe?
Walikosea ini mfano?!?! Kuokoa watu? Kuhakikisha shule zinajengwa ili watoto wasome?!? kwa ufupi hawa wabunge hawajui:
1. Responsibilities zao
2. Roles zao- neno upinzani linaharibu kwao maana yake kuopinga tuuuuu hata kama kitu ni kizuri - so sad!
3. Hawajui mipaka yao.
Kwa kifupi wanaofahamu hutakaa uwasikie wanakwaruzana na Serekali au Viongozi wa serekali. Sasa hivi wanakamsemo.
MIMI nimechaguliwa na wananchi so what?!?!?!? Hao maDC sasa wamechaguliwa na The top ya hao wananchi!! Jaman hebu CHADEMA tumieni ruzuku mnazopewaga kuwapeleka watu wenu SEMINA ELEKEZI!
 
Back
Top Bottom