Mbeya na mambo yao

Nyie mashemeji acheni kulewa misifa.........angalieni mmeshaambiwa kiwango cha elimu kwenu kimeshuka.........nyie endeleeni na Mwa mwa mwa hapa......
 
mkuu una kumbukumbu safi niliwahi kukaa nzovwe miaka ya 80 hayo uliyoeleza yalikuepo,kuna visa vingi sana niliviona,km mvua ikinyesha tulijipanga barabarani hapo nzovwe ilikua lazima ajali itokee,pia kulikua na kundi la washkaji zake jombi kina kibo nao walikua mtata,wababe huo mkoa usiulize sikumoja mdogo wao kibo alimninginiza mwanae nzovwe sokoni kataka kumchinja live mbele ya umati wa watu,fununu zikaja kwamba ndio alikua mkuu wa wachinjaji na wachunaji forest,mara ya mwisho nasikia kibo mwingine alitaka kulipua hicho kitongoji nzovwe kwa bomu akaghairi akajiua mwenyewe,na jombi alikuja kamatwa itigi huko kwa oda ya rais baada ya kupora mbeya,huko kote umetaja umesahau nzovwe mkuu pale ndo ilikua kitongoji cha uharamia,ukikusanya watoto wa sokolo,mbembela,kalongoti*hatari zaidi*,kibo,mwamwaja,tunyande,kina chande na jairo,yani ilikua baraa,jombi wafuasi wake wote alitoa nzovwe na walikua watu wa kazi kweli,lakini sidhani kama kuna mmojawapo aliishia pazuri


da...
mkuu asante sana kwa kunikumbusha kina Tunyande na basi lake injini nyuma
 
round.gif
 
Mwe umwe, mungumbwisye kutali!

Vijana maarufu kwa vurugu kule Isanga mbeya
Mwasimba wa Nonde alikuwa ni noma,alipandisha bendera yake nonde kule.
 
Nakumbuka vita kati ya watoto wa Isanga na Nonde pale uwanja wa sokoine, kijana wa nonde alipigiliwa msumari wa inch sita kiunoni
 
Kuwafananisha Nsekela na Mwaikambo na hawa wa leo akina Mwandosya na Mwakyusa ni sawa na kufananisha mlima Kilimanjaro na kichuguu!!! Hawa wa leo wamejaa ubinafsi tu!!
Kama unataka kujua Mwandosya amefanya nini kwao uliza wanaotoka huko
 
Ninachowapendea ni watu ambao wanamsimamo thabiti na hivyo wanaweza kusimama na kuanzisha kitu kikawa kweli kitu hata kama mazingira ni magumu kiasi gani, kwa hiyo NGO nyingi unakuta kiongozi mnyakyusa KIWOHEDE, SERO, kuna ile ya mama Siwale etc, pia kupeleka Injili Mwakasege, Bukuku, Mwaitege, A Mwasongwe, Christan Mwasongwe etc Bravo wanyakyusa!
 
ni Mbeya pekee kwenye ugonjwa wa zinaa unaitwa Mandeletele, usiombe ukupate huo gono na kaswende ni cha mtoto.
 
Jombi alikuwa ni jambazi maarufu zambia na tanzania akiteka magari, kupora magari na mali za watu.Alikuwa akitoa taarifa kabla hajafanya uhalifu wake. Wazungu wa Denmark waliokuwa wakifadhili mradi wa maji danida walikatisha msaada wao baada ya Jombi kuua na kubaka mke wa mkurugenzi wa mradi huo. Mkapa akatoa amri kuwa jombi akamatwe. Vikosi maalum ndio vilivyoenda kumkamata jombi
sasa JOMBI ALIFUNGWA , YUko hai ama ? hii stori ya Jombi imeniacha kinywa wazi
 
Chungu na Daraja la Mungu vipo Mbeya maeneo ya Kiwila chuo cha magereza
Bwawa la ajabu liko Masoko Mbeya
Rungwe Volcanic mt uko Mbeya
Matema beach iko Mbeya the only beautiful beach in the southern highlands
 
Kweli aisee........maana....wee acha tu nidhamu hii sijapata ona.......

Kinachonishinda kuelewa.....pamoja na Mkoa ule kujaaliwa na wasomi weengi sana......wengi sana wako nje ya nchi.......na wanafahamu sana kwao kulivyo na kila kitu i.e. potentials za kiuchumi......lakini.....lakini.....hawana hata WEBSITE.......

Mijitu kama akina Mwandosya, Mwakalinga, Mwakyusa, Lole ipo ipo tu (joke)........ubinafsi umewazidi na mawivu yasiyokuwa na maendeleo yamewajaa....mke wangu ananisimulia kuwa akina Marehemu Nsekela na Mwaikambo walifanya mengi....sasa sijui hii mijitu mingine inafanya nini

Ha ha ha haaaa!!
Mkuu umeniweza, lakini ukifika karibu na mkoa wa Mbeya sikiliza Mbeya Highlands FM 92.7Mhz. Inasikika mkoa mzima.
Siku hizi mambo kimya kimya.
 
Mbeya nilifika mwaka 79 na sijakanyaga tena.
naogopa kwenda kama kweli hayo masuala ya kutisha yapo na yanatendeka sasa
 
Ha ha ha haaaa!!
Mkuu umeniweza, lakini ukifika karibu na mkoa wa Mbeya sikiliza Mbeya Highlands FM 92.7Mhz. Inasikika mkoa mzima.
Siku hizi mambo kimya kimya.

Hongera sana shemeji.......kumbe ule mradi ulishaanza!!.......dada yako hapa anaomba uiweke mtandaoni pia........nafikiri ndio itakuwa radio ya pili kusikika mtandaoni........
 
-beach nzuri mbeya matema beach...
-wasanii wengi ukiacha waimbaji wa nyimbo za injili wanatoka mbeya au walikulia mbeya
-wachezaji wengi wmaarufu wa mpira wapo mbeya
-makaa ya mawe mbeya
-daraja la mungu la ajabu mbeya kiwira
-ziwa la ajabu la mviringo lipo mlimani mbeya
-kahawa mbeya
-watu wenye nguvu
 
sasa JOMBI ALIFUNGWA , YUko hai ama ? hii stori ya Jombi imeniacha kinywa wazi


Jombi ni mzima kabisa na yuko pale Soweto (Mbeya). Ana gereji yake pale, ina jina la VETA, nadhani wanafunzi wa VETA wa auto mechanics wanajifunzia pale. Nilimkuta tarehe 26/12/2009 nilipokwenda kukarabati gari langu pale, yuko fiti kinoma.
Hata mie nilikuwa simfahamu hadi nilipooneshwa na watu kwamba ndio yeye, na wala sikujua kwamba ile gereji ni ya kwake.
 
-beach nzuri mbeya matema beach...
-wasanii wengi ukiacha waimbaji wa nyimbo za injili wanatoka mbeya au walikulia mbeya
-wachezaji wengi wmaarufu wa mpira wapo mbeya
-makaa ya mawe mbeya
-daraja la mungu la ajabu mbeya kiwira
-ziwa la ajabu la mviringo lipo mlimani mbeya
-kahawa mbeya
-watu wenye nguvu

Hapo sasa, Yule mchezaji wa Simba S.C. Emmanuel Gabriel Mwakyusa anatoka Mbeya maeneo haya haya ya Iyunga
 
Back
Top Bottom