Mbeya Golden city hotel - ogopa kabisa hii hoteli

Siku moja nilibanwa kiasi kwamba ilikuwa ni lazima nilale ktk Hotel moja pale Mwanjelwa, nilitonywa na dogo moja wa jikoni kwenye supu kuwa pale kuna mijizi nijihadhari.

Nikatumia mm za jeshini, nguo na mizigo yote nikaingiza uvunguni mwa kitanda na kitanda chenyewe nikabana mlangoni. Kuamka asubuhi, chumba cha pili jamaa ana-rap kilugha,yaani wahuni wameshafanya vitu vyao. Take care.
 
Asante kwa taarifa mkuu.
Hii Hotel iko sehemu gani tuiepuke?
Tena kesho naelekea Mbeya

Ipo maeneo ya sae ktk highway ya mby dar..yaani iogope u never know usije ukaibiwa ndugu yangu..mwizi apande ghorofa ya kwanza its strange sana bila inside job..
 
Siku moja nilibanwa kiasi kwamba ilikuwa ni lazima nilale ktk Hotel moja pale Mwanjelwa, nilitonywa na dogo moja wa jikoni kwenye supu kuwa pale kuna mijizi nijihadhari.

Nikatumia mm za jeshini, nguo na mizigo yote nikaingiza uvunguni mwa kitanda na kitanda chenyewe nikabana mlangoni. Kuamka asubuhi, chumba cha pili jamaa ana-rap kilugha,yaani wahuni wameshafanya vitu vyao. Take care.

Yaani hata mm nadhani wafanyakazi wanahusika kujua wezi ni kina nani maana meneja akawa ananiambia eti kuna kijana maeneo inawezekana ndio ameiba wanafuatilizia..
 
Napafahamu vizuri sana hapo ila nashangaa ni kahoteli kazuri lakini wanashindwa kukaendesha au kwasababu mwenye nayo alishafikisha miaka10 akatangulia mbele za haki??

Nadhani tatizo ni usimamizi au wanaajili bila background check ya hao walinzi au wafanyakazi wengine..ila ni kujihadhari sana na hizi hotel
 
Nenda basi uone hata hiyo nguo ya ndani hutaiona kuhusu soksi labda ziwe zimetoboka ndo itakuwa bahati yako.
Da hivi wana JF mtu huwezi kwenda kulala kituo cha polisi maana hawa ndio walinzi wa raia na mali zao,i believe ukulala hapo utakuwa safe side
 
mi mwenyewe nimeshangaa! Baridi kali vile aafu utake ac? Aafu mwezi wa nne? Huyu ni mpinzani wake tu.

Hehehehe ww unajua mbeya temp now ni kiasi gani?..uzuri wa ac in condition na kusupply air..hata unaweza kuweka joto..lkn ukifunga vioo vyote utapata wapi hewa ndugu yangu..

Halafu sio kila mtu mfanya biashara..nimekaa pale hakuna hata wateja sasa ana biashara gani labda wengine wamejua ndio maana hawakai pale nimeamua kuleta taarifa hata ww ujihadhari..
 
asante kwa taarifa, kwa hali hii kuna umuhimu wa kuficha hela kwenye underwear ulalapp. Pia mkienda mahotelini kama hakuna kabati suruali msitundike, iweke chini ya uvungu......

Heri upate fungus utatibu kuliko kuibiwa ukatudi dar kwa miguu....
 
asante kwa taarifa, kwa hali hii kuna umuhimu wa kuficha hela kwenye underwear ulalapp. Pia mkienda mahotelini kama hakuna kabati suruali msitundike, iweke chini ya uvungu......

Heri upate fungus utatibu kuliko kuibiwa ukatudi dar kwa miguu....

Hata mimi nakubaliana na wewe na ningekua na hii taarifa nadhani hawa wahusikA wa hoteli wasingeniibia. Ila huwezi amini kama hoteli yenyewe wanakwambia eti ungekabidhi vitu reception kabla ya kwenda kulala yaani wanajua humo vyumbani utaibiwa tu..
 
Pole sana. Mimi nilikuwa na kawaida ya kufikia hapo. Kuna siku nikaenda hapo kama saa 12 hivi nikitokea Dar Kwa Sumry nikaambiwa mmiliki wake alipata ajali na kufariki siku hiyo saa 9.00 Mchana. Hivyo nikaenda kukaa ktk hotel inaitwa Paradise bahati mbaya nilikuwa nimepoteza kadi ya Benki hivyo nilikuwa na fedha taslimu kwa ajili ya Semina. Nilikuwa natoka nazo siku zote (mbili)zikiwa kwenye mfuko wa laptop hadi nikalipa na kubakiwa na Tsh 1,500,000/= basi kukawa na onyesho la Makhirikiri karibu na hapo nikaenda na kufanya kosa la kuacha zile fedha kwenye Begi (wanaziita Pilot Bag)

Nilivyorudi kitu cha kwanza nikaangalia nikakuta pesa iko nikalala na hiyo begi haijafunguliwa iko kama nilivyoiacha. Kuamka asubuhi nikalipe nikakuta kila fungu la laki moja inapungua elfu 30,000/=. Nikafanya uhakiki nikakuta kumbe nililizwa pia soksi mpya kama pea mbili, na underwear mpya kama mbili hivi. Hapo ndipo nilipowaaminia.

Nikashuka chini kuripoti nikakutana na bango kuwa vitu vyote vya thamani ikiwa ni pamoja na PESA vikabidhiwe mapokezi!! Upotevu wowote Hoteli haitasikiliza hata kidogo.
Hivyo nikaghairi kuripoti hilo tukio.

Hata hivyo ni hatari sana kukabidhi fedha kiasi kikubwa kwani kuna jamaa yangu alifanya hivyo siku anaondoka akakutana na vijana wenye piki piki pale tu nje ( Siyo Paradise) wakimtaka awakabidhi haraka kiasi hicho bila kuchelewa kwani walikuwa wanawahi kumwua jamaa mwingine hapo mbele

Hivyo wizi upo sehemu nyingi cha kufanya ni kuchukua tahadhari ya hali ya juu, ikiwa ni pamoja na kutokabidhi pesa kaunta.

sasa kama ulikuwa na hela nyingi kwa nini usiweke benki??? mambo mengine mnashawishi wenyewe kuibiwa....hapa ulisababisha mwenyewe......
 
Hiyo ni sawa lkn wangekosa hela hata laptop wangeiba tu..tatizo ni uwizi kufanywa na wahusika wa hotel..huoni hata soksi wamemuibia..

Tupeane taarifa ya hoteli zilizokithiri kwa uwizi ili tuziepuke..
 
Pole na matatizo yaliyokufika! kunasiku nilifikia lunch time hotel iliyo ubungo dar, niliingia chumbani mida ya saa 9 jion kwaajili ya kupumzika huku nikifuatiria jf kwenye laptop yangu. ilipofika saa 4 usiku niliamua kwenda club, niliacha laptop kitandani nikafunga mlango na kukabizi funguo nikaondoka, nilirudi asubuh saa 12 ili nijiandae kuendelea na safari. nilipofungua na kuingia ndani ya chumba nikakuta wajanja wamebeba laptop, nikakuta wamefungua dirisha pia kuna fagio na kisu vimewekwa chini ya dirisha kwandani. niliongea na mtu wa mapokezi lakini hakunipa msaada wowote wa maana zaidi ya kusema ni wezi wameiba, kwavile muda wa safari ulikuwa umewadia sikuwa na njia nyengine zaidi ya kusamehe.
 
Mi baada ya kuibiwa mara moja hela zoote huwa nahifadhi sehemu ambayo Mungu ndiye anayejua na huwa usiku sitoki na kama mtu anataka kuniibia inabidi aniamshe la sivyo hataweza.
 
thanks mkuu, i compliment, itabidi ukilala ufiche kamera somewhere, na surualini uweke mifugo feki!!!
 
Ukiona vipi usiku ufungue mlango uwe wazi kabisa, vuta ka meza wekea mlango ili usijifunge, kama kuna net shusha kama hakuna basi panda kitandani lala. Hakikisha taa inawaka ili wapitao kwenye korido waone kituko ulichofanya cha kuacha mlango wazi.hakika hatoingia mtu kwako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom