Mbeya: Barabara yapigwa sementi badala ya lami

huyu bwana anazungumzia ulaya gani wanaziba viraka vya lami kwa kuweka cement? sijaona hicho kitu,uakarabati wao lazima waweke lami hasa baada ya winter na mara nyingi hutanguliza cement kwanza na kuziba kwa lami juu kama walivofanya wachina kuanzia ubungo hadi eneo la mliman city.labd utuambie wanatumia zege kwenye vilima korofi kuanzia mwanzo na sio kuchanganya
mbeya wameibiwa hakuna lolote ujinga mtupu.
 
Kwa waliosoma Arts kuanzia Form I ni ngumu kuelewa "elasticity"!

Cement haiwezi kuziba "kiraka" cha barabara ambayo imetengenezwa awali kwa kiwango cha lami - Ni uendawazimu and mostl likely UJINGA!

Nitaelewa kama ni hatua ya dharura.....kwamba hawana lami na barabara imeharibika kupitiliza (na labda kuna mkubwa atapita mitaa hiyo siku za karibuni)....
Kwa kulinganisha flexibility, Lami ni flexible, wakati zege ni almost rigid.....sasa kuchanganya hivi sio sahihi...
Bottom line, zege waliloweka litazidi kuharibu hiyo lami ya zamani.....
 
Mkuu hakuna cha dharura wala nini, bei ya pipa la lami ambayo kwa viraka hivyo hayafiki hata matano ni kama milioni mbili hivi tena huwa wanaichemsha na kuni na unachanganya na kokoto (Hamjawahi kuwaona wakandarasi wa kuunga unga wa Tanroads??). Sasa hiyo halmashauri ya jiji la Mbeya haina m2 na hizo nyenzo?
 
Kwanza huyu Idd kakaaa sana mkoa wa Mbeya alianzia wilaya ya Kyela enzi hizo akiwa ndyumyana(kijana)hadi sasa anazeka yupo hapo hapo mkoani Mbeya anazunguka kutoka A to B,B to A ni kama vile ana MoU na mkoa wa Mbeya , ana kahimaya kake hapo mkoani.
 
Simenti (SARUJI) kama ndo lilikuwa lengo, haiwezi kutengeneza barabara, achilia mbali kuziba viraka barabarani!

Types of pavements:-
  • Flexible pavement ( Hapa zipo kibao tu:- Single surface dressing, double surface dressing, asphalt concrete...)

  • Rigid pavement.( Tembelea mlima kitonga mkoa wa iringa). Hapo pichani nnachokiona ni uzibaji wa viraka kwa kutumia zege. Sasa tufanye wastani wa kiraka kimoja kina ujazo wa 0.214 = (0.75 x 0.75 x 0.38)m[SUP]3[/SUP] , na bei kwa ujazo wa 1m[SUP]3 [/SUP]iwe ni 250,000.00 kwa mfano. Hii ndo kusema kiraka kimoja kinagharimu Ths.53,500.00. Tufanye mobilization cost kuwa ni Tshs. 40ml, bakaa hapo ni 360ml. Ok, chukua 360ml/53,500.00 kwa kiraka. Hapo ni viraka 6,729 hivi. Ni vingi sana na kwa ufupi hiyo si barabara ya kuziba viraka. Mleta mada ananichanganya maana nashindwa kuelewa lengo ni nini hasa?
 
huyu bwana anazungumzia ulaya gani wanaziba viraka vya lami kwa kuweka cement? sijaona hicho kitu,uakarabati wao lazima waweke lami hasa baada ya winter na mara nyingi hutanguliza cement kwanza na kuziba kwa lami juu kama walivofanya wachina kuanzia ubungo hadi eneo la mliman city.labd utuambie wanatumia zege kwenye vilima korofi kuanzia mwanzo na sio kuchanganya
mbeya wameibiwa hakuna lolote ujinga mtupu.

Unazungumzia tabaka gani katika haya ( Subgrade, Sub base and Base course)? Twende pamoja mkuu.
 
jamani angalieni bara bara ya lami hiyo ....itawekwaje viraka vya sementi? eti hadi ulata wanafanya...ulaya gani? kuweka viraka ka cement kwenye bara bara ya lami? sijaona

"Taa eee taa, taa mpya kwa taa kuukuu"
Mi si mtaalam wa ujenzi, ila kama cement ni bora zaidi ya lami, kwanini basi wasitumie lami ktk kujenga barabara zetu ukizingatia tuna viwanda vya cement nchini itasaidia pia kuongeza pato la nchi na ajira kwa vijana endapo usimamizi au uwajibikaji wa kila mmoja wetu utazingatiwa.
 
Hii hata kabla ya kuangalia hizo picha nilianza kucheka kwa kukumbuka "Visa vya Pwagu na Pwaguzi" pale walipotengeneza barabara kwa kuweka mkaa badala ya lami.
waMbeya, "manyoya hayo, kuku kaliwa zamani".

Mbeya kwa miujiza haijambo! si Magufuli wala Kandoro ataona hilo, Unazungumzia 400 million na viraka vya cement ya Pozorana na bado bado tatizo halionekani hata kwa wachangiaji wengi wa J/F, any way tumezoea tutafika.
 
Kumbukeni,hicho kipande cha barabara hapo Meta kila mwaka kinakarabatiwa kwa kufukia hayo mashimo,mara waweke udongo sasa sementi,sijui mwakani wataweka nini.
Hayati Mwalimu Nyerere alisema "Ulaya wanakula 10 percent na barabara inajengwa,Afrika wanakula 10 percent na barabara haijengwi" Ni kweli hayo ni manyoya ndege alishaliwa siku nyingi.

Mgagakikikoko.
 
Lami na cement zina elasticity tofauti hasa hali ya hewa inapobadilika. Nina wasiwasi na huyo mkandarasi, nijuavyo mimi kama ulijebga kwa lami, tia viraka vya lami ili ku maintain the same elasticity kwa nyakati tofauti za mwaka. Kama ni barabara ya cement mwanzo mwisho, au kuna layer ya cement na lami then naweza kukubali. Huo ni usanii
 
Hii hata kabla ya kuangalia hizo picha nilianza kucheka kwa kukumbuka "Visa vya Pwagu na Pwaguzi" pale walipotengeneza barabara kwa kuweka mkaa badala ya lami.
waMbeya, "manyoya hayo, kuku kaliwa zamani".

Dah, ila pwagu na pwaguzi , licha ya kuchekesha, lilikuwa darasa tosha.
 
Hii barabara ni juzi tu imefumuliwa yote na kutengenezwa upya, leo hii inasakafiwa na saruji!
Hivi mhandisi wa jiji anajielewa kweli? Anashindwa nini kufanya solution ya kudumu kwa kuweka grade ya lami itayokidhi misukosuko ya hapo!?
 
Hii habari ya mwaka 2012,wakazi wa huko watupe status yake kwa sasa.....
 
Nafikiri hii post iliwekwa kabla barabara haijafumuliwa yote na kujengwa upya. Japo mpya iliyojengwa na wachina nayo ilifumuliwa baada ya kutoboka toboka kabla ya makabidhiano, wakatakiwa kujenga upya mwishoni mwa mwaka jana ambayo inatumika hadi sasa.
 
Back
Top Bottom