Mbele giza ajira za ualimu

Tt4tat boy

Member
Nov 26, 2015
45
10
Heshima kwenu wakuu, nina wasiwasi mkubwa sana hapo baadae katika hizi ajira za ualimu maana nikichunguza kuna shule kwa sasa walimu wanagawana maada za kufundisha hali hii inanipa shaka kidogo na kuniaminisha kuwa huenda walimu wametosha, nasema haya kwa sababu kuna mdogo wangu yupo chuo na aliniomba ushauri kuhusu kozi ipi asome mimi nikakurupuka kwa mbwembwe na mkwara mzito kuwa akasomee UALIMU sasa nikijaribu kuchunguza wadau wanavyo sema duu nakata tamaa kabisa maana nilikuwa sitaki dogo ahangaike kusaka ajira na ndo kwanza tupo first yea mwaka huu all in all Mungu yupo , kazi ni kazi, mnasemaje wadau kuhusu hili swala
 
Ndo hivyo tumejaa hadi tunagawana topic. Mi nafikiria kushauri maafisa elimu kutugawia maeneo ya kufanya usafi shuleni kuliko kuchukua mishaara ya bure.
 
Kwa upande wa walimu wa arts ni KWELI tumejaa, lkn kwa upande wa walimu wa science bado wanahitajika sana tu
 
Heshima kwenu wakuu, nina wasiwasi mkubwa sana hapo baadae katika hizi ajira za ualimu maana nikichunguza kuna shule kwa sasa walimu wanagawana maada za kufundisha hali hii inanipa shaka kidogo na kuniaminisha kuwa huenda walimu wametosha, nasema haya kwa sababu kuna mdogo wangu yupo chuo na aliniomba ushauri kuhusu kozi ipi asome mimi nikakurupuka kwa mbwembwe na mkwara mzito kuwa akasomee UALIMU sasa nikijaribu kuchunguza wadau wanavyo sema duu nakata tamaa kabisa maana nilikuwa sitaki dogo ahangaike kusaka ajira na ndo kwanza tupo first yea mwaka huu all in all Mungu yupo , kazi ni kazi, mnasemaje wadau kuhusu hili swala

We jamaa umefika chuo, still bado unategemea spoonfeed tu?
Ulipoamua kusoma education doesnt mean kwamba serekali isipokukumbuka basi huna altenative.

Kuna watu wengi wamesomea huo ualim but hawafanyi ualimu, wanaishi

Kuna wengi pia wamejiajiri, na pia wameajiliwa private school.

Anza sasa kuwa na mentality ya kutoitegemea serekali ikuajili mwalimu, ajira hizo zitegemee kama dharura tuu
 
Kama ni mwalimu wa kiswahili na history hesabu maumivu aisee shule yetu kuna walimu wapya wa history 12 kiswahili 20 bora English na Geography kidogo si wengi sana. Mwalimu wa biology na physics yupo mmoja tu shule nzima mpaka wanaajili wale walomaliza form 6 ya science kama temporary
 
Watu wengine banaa yaani unawaza ajiraa na kati Uko fest year, na nyie mnaosema ajira hamn wala myie siyo serikaliii , arts wamejaa mjin na cyo vijijini achen kuongea vtu ambavyo ...
 
Alafu mi watu nawashangaa sana eti eeenhee c wa Arts tumejaaa, so lengo lenu walimu wa arts wasiajiliwe au? Shule zenyew tumesom kayumb ambazo haizielewkii unaanzaj kusom chemia somo ambaloo haujawahi muona hata mwalimu wakee, watu wanaosema ajira hamn wao cyo serikalii , na walimu tutaajiriwaa kama kakawaida kama MTU alisomea kozi zingne acje kuwa discourage watu hapaaa
 
Mimi naomba nishauri kitu kimoja.
Haya ni masuala ya maisha ya watu.
Si vizur kutoa maneno ambayo unajua fika kwamba yanalenga kukatisha watu tamaa ( hata kama ni ya kweli).
Ingefaa kusema kwamba waalim wa masomo ya arts wapo wengi ila uhakika Wa ajira upo mikononi mwa serikali yenyewe.

Unaweza Leo usipate ajira ya ualim but miaka michache ijayo ukaja hapa kushukuru kwa kukosa ajira ya ualim. Trust me.

Maana mwenyezi Mungu ana njia nyingi zakutufikishia rizk.

Unaweza pata plan nzur ya mchongo wowote ambao utakutoa sana hapo baadae na pengine ungekuwa kwenye ajira ya ualim usingeweza kuwaza mchongo huo.

Naomba waalim tarajali Wa masomo ya arts tusikatishwe tamaa na maneno ya watu ambao pengine hawaelew madhara ya kujifanya wasemaji Wa wizara zinazohusika na ajira za ualim.
 
Heshima kwenu wakuu, nina wasiwasi mkubwa sana hapo baadae katika hizi ajira za ualimu maana nikichunguza kuna shule kwa sasa walimu wanagawana maada za kufundisha hali hii inanipa shaka kidogo na kuniaminisha kuwa huenda walimu wametosha, nasema haya kwa sababu kuna mdogo wangu yupo chuo na aliniomba ushauri kuhusu kozi ipi asome mimi nikakurupuka kwa mbwembwe na mkwara mzito kuwa akasomee UALIMU sasa nikijaribu kuchunguza wadau wanavyo sema duu nakata tamaa kabisa maana nilikuwa sitaki dogo ahangaike kusaka ajira na ndo kwanza tupo first yea mwaka huu all in all Mungu yupo , kazi ni kazi, mnasemaje wadau kuhusu hili swala

Pole tatizo lako liko kwenye uelewa!Tunaposema ajira hatumaanishi kwa Magufuli tu!Hata kwa Rwakatale au kwa Rugemalira mdogo wako anaweza kuajiriwa.
 
Watu wengine banaa yaani unawaza ajiraa na kati Uko fest year, na nyie mnaosema ajira hamn wala myie siyo serikaliii , arts wamejaa mjin na cyo vijijini achen kuongea vtu ambavyo ...

Acha kujiliwaza dogo, mwaka huu walimu wote elfu 36 wameletwa kwenye halmashauri za wilaya ambapo hakuna shule iliyopokea walimu chini ya 20 na hapo unakuta sayansi ni ni mmoja au wawili au hakuna kabisa.
 
walimu bado wanaitajika sana kwani bado tatizo lipo ukienda vijijini unakuta walimu wawil wanasimamia shule moja na bado ukiangalia sio wote wanaosomea ualimu watakuja taka ajiliwa hapana wengne ni njia tu wanapita pia ukumbuke idadi ya wastafu kwenye secta ya elimu bado ipo aijasimama na bado utambue walimu wengi upoteza maisha sana na kwa idadi kubwa bado hitaji la walimu lipo na aliishi kesho
 
Heshima kwenu wakuu, nina wasiwasi mkubwa sana hapo baadae katika hizi ajira za ualimu maana nikichunguza kuna shule kwa sasa walimu wanagawana maada za kufundisha hali hii inanipa shaka kidogo na kuniaminisha kuwa huenda walimu wametosha, nasema haya kwa sababu kuna mdogo wangu yupo chuo na aliniomba ushauri kuhusu kozi ipi asome mimi nikakurupuka kwa mbwembwe na mkwara mzito kuwa akasomee UALIMU sasa nikijaribu kuchunguza wadau wanavyo sema duu nakata tamaa kabisa maana nilikuwa sitaki dogo ahangaike kusaka ajira na ndo kwanza tupo first yea mwaka huu all in all Mungu yupo , kazi ni kazi, mnasemaje wadau kuhusu hili swala

Watu wengine mnaboa bwana wewe mwenyewe ndio upo first year, unazingizia kuwa mdogo ako ndio anayehitaji ushauri, we si upo UDOM wewe, tena upo block Q room no 45 we soma tu kwa bidii sasa ukianza kufikiria kuwa utaajiriwa au hautaajiriwa ivi utasoma kweli wewe..naona kama utadisco tu, maana utakuwa huna moyo wa kusoma.
 
Back
Top Bottom