Kilimo, soko na faida za Uyoga

Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,503
6,375
Habari wana JF.

Ninajaribu kujifunza kuhusu kilimo cha uyoga na pia ninaperuzi na masoko yake. Nataka kuwa mkulima wa uyoga lakini nataka kwanza nijue namna ya kutoa uyoga bora na kupata masoko ya uhakika.

Nimelima kidogo awamu ya kwanza ya kujifunzia ambao nilifanya wa kula mwenyewe na kugawa mtaani kwangu, sasa ndiyo naingia ulingoni rasmi.

Kama kuna mwenye ushauri na maelekezo zaidi itakuwa bora kwangu!

Wapi masoko ya uhakika ni jambo la msingi kuliko la kuuza mtaani.

=====

Utangulizi
Miaka ya karibuni, utaalamu wa kuotesha uyoga umeanza hapa Tanzania baada ya watu kutilia maanani lishe bora ya protini na manufaa mengine ya zao hilo. Kwa kuwa uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za kuoteshea, urahisi wa teknologia ya kuotesha katika mazingira ya Tanzania na soko lake kwa wananchi na katika hotel. Hata hivyo ni wananchi wachache tu wanaojua kilimo cha uyoga.

Uyoga unaozalishwa unafahamika. Aina zinazofaa kwa Tanzania ni zile ambazo hustawi vizuri, kwenye maeneo ya joto la wastani wa nyuzi joto 20C hadi 33C. Kwa mfano uyoga aina ya mamama n.k. Aina hizi za uyoga pia uhitaji hali ya unyevu hewani (moisture) wa kiasi cha asilimia 75%.

Uoteshaji
Kabla ya kuanza kuzalisha uyoga inabidi kuwa na chumba chenye paa ambalo litazuia jua, mvua, na vumbi. Chumba hiki kinatakiwa kiwe na sakafu inayohifadhi unyevunyevu pamoja na sehemu ya giza ambayo ni muhimu kwa kuotesha utando wa uyoga. Mkulima wa kawaida anaweza kutumia kasha kama sehemu ya giza.

Mbegu
Mbegu za uyoga huzalishwa kwenye maabara zenye vifaa vinavyowezesha kuotesha mbegu hizo bila kuchafuliwa au kuchanganyika na vimelea kama bakteria, ukungu au jamii nyingine za uyoga ambazo haziliwi. Hapa Tanzania hivi sasa maabara hizo zipo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kituo cha utafiti wa kilimo-Uyole, taasisi ya utafiti wa kilimo cha bustani- Tengeru (HORTI –Tengeru, Arusha), na TIRDO

Hatua muhimu za kuotesha uyoga
  1. Kusanya masalia ya mazao kama vile mabua, majani ya mpunga, ngano, pumba za mpunga au mahindi, masalia ya miwa baada ya kukamua nk. Vitu hivi hutumika kama mali ghafi kwa kuoteshea uyoga.
  2. Mabua, majani ya mpunga au migomba yakatwe kwa urefu usiozidi sm 6, au urefu wa vidole kwa kutumia panga au kisu.
  3. Loweka mali ghafi kwenye maji ya kawaida kwa muda wa siku nzima (masaa 24).
  4. Kisha yachemshe kwa muda wa saa mbili ili kuua vijidudu pamoja na vimelea vilivyomo.
  5. Ipua na umwage maji yote halafu tandaza kwenye kichanja kisafi ili yapoe bila kuchafuliwa na vumbi au vijidudu.
  6. Kisha jaza mali ghafi hii katika mifuko ya nailoni tayari kwakupanda mbegu.
Namna ya Kupanda
Kuna aina mbili za upandaji

Aina ya kwanza
Chukua mfuko wa nailoni wenye upana wa cm 40 - 45 na kimo cm 75. Weka tabaka la mali ghafi ya kuoteshea yenye kina cha sm 10 katika mfuko halafu tawanya mbegu ya uyoga juu yake. Baada ya kuweka mbegu, weka tena tabaka nyingine ya vioteshea na kuweka mbegu juu yake. Endelea kuongeza tabaka kwa namna hii mpaka ifike ujazo wa robo tatu ya mfuko.



MFUKO+WA+UYOGA.bmp

Aina ya Pili
Changanya malighafi ya kuoteshea (baada ya kuchemshwa na kupoa) na mbegu ya uyoga katika uwiano wa 1: 25 (mbegu : malighafi ya kuoteshea) kwa uyoga aina ya mamama (Pleurotus spp.). Kisha mchanganyiko huo ujazwe katika mifuko ya nailoni mifuko hii iwe na ukubwa wa cm 20 kwa cm 40 ambamo unaweza kujaza kilo 1 – 1.5 ya mali ghafi ya kuoteshea.



MFUKO.bmp
Funga mifuko na toboa matundu kwenye mifuko yenye kipenyo cha cm 1 kwa kila umbali wa cm 6 hadi 10 kwa kila mfuko.Matundu yawe mengi ili kuingiza hewa ya kutosha ndani ya mifuko. Kumbuka uyoga ni kiumbe hai hivyo unahitaji kupumua.

UYOGA+MATUNDU.bmp

Matunzo
Weka mifuko kwenye chumba cha giza. Kwa mkulima wa kawaida waweza kutumia kasha lisilopitisha mwanga kama chumba cha giza. Acha mifuko humo kwa muda wa siku 14 - 21 bila kufunua ili ukungu mweupe uweze kutanda vizuri.

Utando wa uyoga ukishatanda vizuri kwenye mali ghafi ya kuoteshea, hamishia kwenye chumba chenye mwanga na hewa ya kutosha kisicho pigwa na jua. Katika chumba chenye mwanga, mifuko inaweza kuwekwa kwenye, meza, chanja la waya au miti.

Mifuko inaweza pia kuning'inizwa kwenye kamba toka kwenye boriti za paa la chumba hicho. Unatakiwa kudumisha hali ya unyevu kwenye chumba hicho cha mwanga kwa kumwaga maji sakafuni. Ukiona vipando vinakauka unaweza kunyunyizia maji yaliyochemshwa na kupoa juu ya mifuko mara tatu au zaidi kwa siku. Tumia bomba la mkononi lenye ukubwa wa lita moja kunyunyizia maji. Tafadhali: usizidishe maji kwani maji yakiwa mengi sana yaweza kuozesha uyoga uliyoanza kuota. Aina nyingi za uyoga huanza kutoa vichwa (pini) siku 2 - 3 baada ya kuwekwa kwenye mwanga.

Uvunaji
Uyoga huwa tayari kuchumwa siku tatu baada ya vichwa /pini kuonekana. Uyoga uvunwe kwa mkono kwa kushika katikati ya shina la uyoga kisha zungusha hadi uyoga ung'oke. Usiondoe kichwa peke yake katika kuvuna uyoga kwani kubakiza shina huzuia uyoga mwingine kutokea. Mkulima anatakiwa ajue soko la uyoga kabla ya kuvuna ili kuepuka gharama za kuhifadhi. Kwani uyoga ukishavunwa unatakiwa uliwe kabla haujaharibika.

Jinsi ya kuhifadhi
i) Unaweza ukauweka uyoga kwenye mifuko ya karatasi na kuhifadhi kwenye jokofu.
ii) Unaweza ukauanika juani hadi ukauke na kuweka kwenye mifuko ya nailoni liyofungwa vizuri ili isipitishe hewa na unyevu.

Soko la Uyoga
i) Watu wengi hupenda uyoga mbichi uliotoka shambani wakati huo huo kama kitoweo, kwa kutumia kama nyama, samaki, au kama kiungo.
ii) Unaweza kuuza uyoga mbichi kwa bei ya shilingi 6000/= hadi 10000/= kwa kilo kwa uyoga.
Pia unaweza kuuza nje ya nchi ikiwa uyoga wako ni kiasi kikubwa na uko katika viwango vinavyo kubalika kimataifa.

Mambo ya Kuzingatia
Uzalishaji wa uyoga huzingatia sana hali ya hewa na vifaa ulivyonavyo, hivyo basi, kabla hujachagua aina ya uyoga unaotaka kupanda pata ushauri kwa wataalamu walio karibu nawe.

Ukishanunua mbegu, kama hupandikwa muda huo, hakikisha umehifadhi mbegu hiyo kwenye jokofu. Kama huna jokofu la kuhifadhia, nunua mbegu baada ya kuandaa kila kitu. Hata hivyo, uotaji wa mbegu huwa mzuri kama zitakaa nje ya jokofu kwa siku mbili.

Mbegu za uyoga huwekwa ndani ya chupa yenye ujazo wamililita 300, waweza kutumia chupa moja katika kupanda kwenye kilo 15 ya mali ghafi ya kuoteshea. Hakikisha
unamaliza mbegu yote iliyo ndani ya chupa kwani ikibaki itapata maambukizo ya vimelea.
Hakikishaunaponunua mbegu iwe ni nyeupe. Mbegu ambayo siyo nyeupe ni dalili za maambukizo ya vimelea vingine na hivyo haifai kwa kupanda.

Hakikisha chumba cha kupandia ni kisafi na hakipati vumbi toka nje ili kuzuia maambukizo ya magonjwa ya uyoga.

Usimwagilie uyoga maji yasiyochemshwa kwani maji hayo mara nyingi si salama. Yaweza kusababisha vimelea vingine kuota, kwani uyoga ni dhaifu kuhimili ushindani wa vimelea.

Pia waweza kusababisha magonjwa ya uyoga ambayo kutibu kwake kunahitaji kutumia dawa za viwandani ambazo ni sumu na hivyo kusababisha madhara kwa mlaji. Unaweza kupata faida nyingi kutokana na uzalishaji wa uyoga.


Faida za Uyoga
Lishe kama protini inayolingana na ile ipatikanayo kwenye maziwa, samaki na kunde. Pia utapata vitamini B, C, na D, na madini ya joto, phosphoras, chuma na potashi.

Uyoga husadikika kutibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, moyo, shinikizo la damu na figo.

Masalia ya mazao hutumika katika kuzalishia uyoga, na baada ya kilimo cha uyoga yanaweza kutumika kama mbolea asili kwa kilimo cha bustani. Masalia ya kilimo cha uyoga pia hutumika kama chakula cha mifugo kama ng'ombe.

Kilimo hiki huhitaji eneo dogo sana la ardhi na kiasi kidogo cha maji, hivyo hupunguza tatizo la ukosefu wa ardhi na ugomvi katika jamii ambao unatokana na tatizo hilo.

Kilimo hiki ni ch mwaka mzima, na mzunguko wa kwanza ni kati ya wiki 6 mpaka 12

Kilimo hiki ni njia nyepesi ya kutoaajira kwa familia kutokana na gharama ndogo, teknolojia rahisi inayotumika na pato lake kubwa.

Karibuni

 
Mimi nimewahi kutembelea shamba moja la uyoga katika mkoa wa Dodoma. Kwa kuwa napenda sana uyoga, nilifurahi sana kuona unavyoshughulikiwa. Mhusika alikuwa na mabanda kadhaa makubwa ambayo yameezekwa kwa nyasi.

Inasemekana mabanda ya aina hiyo yanafaa zaidi kwa kuwa hayaruhusu joto jingi hasa maeneo yenye jua kali kama maeneo ya katikati ya Tanganyika (nina maana Tanzania Bara). Kwa sababu hizo ndugu yangu inategemea uko maeneo gani ya nchi yetu. Banda halihitaji kuwa na mwanga sana ili upate matunda mazuri zaidi.

Kwa maelezo niliyoyapata pale shambani, usafi katika banda unahitajika sana na uangalizi wa karibu. Bila kusahau uwepo wa maji ya kutosha kwa ajili ya kunyunyizia uyoga kila inapohitajika.

============

uyoga pix 9.jpg
Mkulima akionesha uyoga uliioteshwa kwenye mifuko ya plastiki

Wakulima wakionyesha jinsi uyoga unavyooteshwa.JPG

KWA mujibu wa tafiti mbalimbali kuna aina nyingi za uyoga duniani ambazo zina matumizi tofauti yakiwemo ya chakula na dawa.

Chama cha Wazalishaji Uyoga cha Dar es Salaam, (DMGA) kinasema kwamba uyoga umegawanyika katika makundi makuu matatu; kundi la kwanza likiwa la uyoga-taka (saprophyetes). Kinafafanua kwamba uyoga huu hupata virutubisho vyake kutoka kwenye miti mikavu na masalia ya mazao ya kilimo.

Aina nyingine kwa mujibu wa DMGA ni uyoga tegemezi (parasites) ambao hupata virutubisho vyake kutokana na mimea na wanyama hai na huweza kusababisha uharibifu mkubwa wa mimea na wanyama hao. Uyoga ufaano (symbionts) ni aina nyingine ambayo DMGA wanasema hupata virutubisho vyake kutokana na mimea na wanyama wanaoishi karibu nao bila kuleta madhara.

Huu pia ni uyoga unaoishi kwa kutegemeana. DMGA wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Judith Muro wanasema uyoga ni mmea mkavu ambao hauwezi kujitengenezea chakula, lakini hutoa vimeng'enyo vinavyosaidia kuyeyusha mabaki ya mimea au wanyama ili kujipatia chakula.

Uyoga huweza kuota wenyewe porini au kuoteshwa kitaalamu na matumizi ya uyoga kwa binadamu ni pamoja na lishe na tiba. Uyoga una vitamini lishe B, C na D, madini ya fosfarasi, chumvi, potasiam na chokaa na pia una protini kwa wingi kiasi cha wastani wa asilimia 10 hadi 49.

Mbali na wingi wa vitamini lishe, pia uyoga ni tiba inayosaidia kuimarika kwa kinga za mwili na kudhibiti magonjwa kutokana na kuwa na viinilishe vingi.

"Zipo aina mbalimbali za dawa kwa mtindo wa vidoge, maji na sindano zinazotengenezwa kutokana na uyoga," anasema Muro. "Dawa hizo zinaweza kutibu au kuzuia magonjwa ya kifua kikuu, kusukari, moyo, shinikizo la damu, figo, saratani mbalimbali, vidonda vya tumbo na lehemu," anasema.

Kutokana na umuhimu wa uyoga kuwa lishe na tiba kwa binadamu Juni 28, mwaka huu Chama cha Wazalishaji Uyoga cha Dar es Salaam kilifanya maonesho ya uyoga kwa vikundi vya wakulima wa zao hilo katika Shule ya Sekondari Mongola, iliyopo Kata ya Mzumbe, wilayani Mvomero, Morogoro.

Vikundi vya wakulima wa uyoga kutoka Kata ya Mikese, Wilaya ya Morogoro na Kijiji cha Vigenge, Kata ya Mzumbe, vilishiriki kwa kuonesha bidhaa zitokanazo na uyoga na mapishi. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa DMGA, Judith Muro, vikundi vya akinamama vimekuwa na hamasa kubwa zaidi hasa baada ya kutambua kuwa uyoga unaweza kuwa chanzo cha mapato kwa familia na hivyo kuwa njia mojawapo ya kupunguza umasikini.

"Uyoga ni rafiki wa mazingira kwa kuwa unatumia makapi ya viwandani na mashambani ambayo yangeweza kuwa kero kwa jamii. "Baada ya kuvuna uyoga mabaki yake hutumika kurutubisha ardhi na kuua minyoo ya ardhini inayoshambulia mazao kama nyanya na migomba," anaelezea Muro.

Anasema uyoga unaweza kuwa ajira kwa vijana pia wazee na unafaa pia kuwa kilimo cha wenye kipato kidogo mijini kwa kuwa hauhitaji eneo kubwa la kuzalishia. Anasema kwa kutambua umuhimu wa uyoga, Mwenyekiti huyo anaiomba Serikali hasa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika iliingize zao la uyoga kwenye mfumo wa kuendeleza mazao muhimu na lipatiwe rasilimali watu na fedha katika kuliendeleza.

"Bado uzalishaji wa mbegu bora za uyoga nchini hautoshelezi na uzalishaji wake haujaingizwa kwenye mfumo wa kudhibiti mbegu ili wakulima wapate mbegu bora. Ombi letu kwa serikali ni zao hili kuingizwa kwenye mfumo wa kuendeleza mazao nchini," anabainisha. Kwa upande wake, mkulima wa uyoga wa Kijiji cha Vigenge, Kata ya Mzumbe, Janeth Mbwambo, anasema tangu ameanza kushiriki kilimo cha uyoga, kimempatia mafanikio makubwa ya kiuchumi.

Mbwambo ambaye ni Ofisa Ugani katika Kijiji hicho anasema ameotesha uyoga katika banda lenye urefu wa mita nne kwa mita tano. "Uyoga unaniingizia fedha kuanzia Sh milioni nne hadi nane kwa kipindi cha miezi mitatu ya uzalishaji. Fedha hizi zinanisaidia kuboresha maisha na familia yangu," anasema Ofisa Ugani huyo.

Naye mkulima mwingine wa uyoga, Maria Shindika, anasema licha ya kuwepo kwa soko la zao hilo, bado wakulima wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa mbegu, hali inayowafanya waoteshe kwenye maeneo madogo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Anthony Mtaka, ambaye alikuwa mgeni rasmi siku ya maonesho ya uyoga, anakitaka chama hicho kuweka mfumo utakaowaunganisha wakulima wa zao hilo wa mikoa yote nchini ili kuongeza uzalishaji utakaotosheleza soko la ndani na nje.

Mkuu wa Wilaya anasema, hatua hiyo itakuwa ni kuendeleza juhudi zilizokuwa zimeanzishwa na Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa. Anasema Mzee Kawawa, baada ya kustaafu alikijita katika kilimo cha uyoga hapa nchini na kuwa mhamasishaji mkuu wa zao hilo.

Hata hivyo anasema huko nyuma uyoga ulikuwa unaliwa na wale waliokuwa na utamaduni wa kuufahamu hususan ule wa msituni na wale waliokuwa wakitembelea hoteli kubwa hususan wapenzi wa supu ya uyoga.

"Kupitia siku hii ya maonesho ya uyoga, jamii inaweza kupata fursa ya kujifunza na kufahamu faida na matumizi ya uyoga katika mwili wa binadamu," anasema Mkuu huyo wa Wilaya ya Mvomero. Anaongeza: "Historia ya kilimo cha uyoga inaonesha kuwa ina zaidi kidogo ya miaka 10 hivyo hapa ninaona kuna baadhi yetu tunahitaji kuweka nguvu zaidi katika kuendeleza zao hili.

Anasema kwamba tangu Mzee Kawawa afariki dunia kasi ya kuhamasisha kilimo cha uyoga nchini imeshuka na kwamba kutokana na umuhimu wake jamii inapaswa kufufua juhudi zilizoanzishwa na Mzee Kawawa. "Mzee Kawawa alikuwa ni kiungo muhimu katika uendelezaji wa zao la uyoga. Chama hiki kwa sasa kifanye kazi aliyoanzisha huyu mzee wetu kabla ya kifo chake kama njia ya kumuenzi pia," anasisitiza Mtaka.

Mtaka pia anakishauri chama hicho kuelekeza nguvu zake katika kufundisha zaidi juu ya ujasiriamali wakulima wote na si wa uyoga pekee pamoja na kusimamia uzalishaji bora wa zao hilo. Anasema chama hicho kinapaswa kuwa na mtandao ikiwa ni pamoja na kuchukua jukumu la kuwatafutia wakulima masoko ya uhakika, hususan katika hoteli kubwa na maduka makubwa maarufu kama supermarkets.


Chanzo: Habari Leo

 
Ndugu yangu kuhusu soko inategemea uko wapi. Kama ni maeneo ya miji mikubwa uyoga unahitajika kwa wingi sana katika hoteli kubwa kubwa. Katika hoteli hizo kuna kitu kinaitwa supu ya uyoga ambayo hutayarishwa kabla mteja hajaanza kupata chakula katika hoteli kwa mlo wa kihoteli.
 
Ukiweza kupata uyoga wa hali ya juu unaokubalika, hapa Nairobi soko ni la uhakika kwenye mahoteli makubwa makubwa. Kunao wakulima wakubwa huku wa uyoga but for export purposes only, kwa hivyo local market haijatoshelezwa.

Ni kilimo kizuri sana lakini ni lazima uwe muangalifu sana kwenye masuala ya usafi na kadhalika kama vile mchangiaji mmoja hapo juu ameshauri. Unaweza uka google "how to grow mushrooms" na utapata sites nyingi zitakazo kupa mafunzo. All the best.
 
Najipanga kwa kuanza kujishughulisha na kilimo, biashara ya uyoga ila bado sijajua masoko ya bidhaa hiyo yako vipi. Mwenyeufahamu wa biashara hii naomba anijuze
 
Kwahiyo tujadili nini sasa?!Kama uyoga sio mboga/dawa?!

Nwy mi nasema tu kwamba uyoga ni mtamu ukiandaliwa vizuri kwenye mboga.Nakumbuka niliwahi kusema siwezi kula hata siku moja ila siku nilipoonja nikadata nao.
 
Uyoga ni sehemu ya kuvu inayotokea juu ya ardhi na kukuza vibufu vinavyofanana na mbegu ya mimea. Uyoga mara nyingi huitwa mimea lakini si mimea ni sehemu ndogo ya kuvu au fungi.

Kazi ya uyoga kwa fungi yake ni kama matunda kwa mmea yaani ni kusaidia kuzaa na kusambaza. Uyoga ni tu sehemu ndogo ya fungi yote inayoendelea kama miseli ndani ya ardhi kwa mita nyingi. Uyoga si fungi mwenyewe bali kitu kama tunda lake. Unajengwa na nyuzi nyingi za kungunyanzi na kuwa mahali pa kukuza vibufu ambavyo ni kama mbegu wa fungi.

Uyoga kama chakula Uyoga ni maarufu kama chakula lakini ni chakula kinachohitaji uangalifu na utaalamu. Zinapikwa, kukaangwa na aina kadhaa pia huunganishwa bichi katika saladi.Uyoga huwa na protini nyingi pamoja na madini na vitamini ndani yake. Kwa hiyo ni chakula bora. Kwa upande mwingine kuna uyoga za sumu zinazofanana na uyoga za kuliwa na sumu ni kali inaweza kuua.


Uyoga
 
KUNA AINA 14,000 ZA UYOGA.KATI HIZO ZINZOLIKA NI 3000 NA AMBAZO NI AMHUSUSI KWA DAWA NI AINA 700.HIVYO KWA FAIDA UYOGA HUTUMIKA KAMA CHAKULA NA DAWA.KUUTAMBUA INABIDI KUANGALIA RANGI,UMBO,SAIZI YAKE ILI KUTOFAUTISHA WA KULIWA NA AMBAO NI SUMU.FAIDA ZA UYOGA NI NYINGI MNO. 1=HULETA NGUVU NA AFYA MWILINI, 2=INA MADINI MUHIMU KAMA PATASHIUM,SHABA,SELENIAMU NA 3= VITAMINI KAMA VITAMINI E,VITAMIN B,VITAMIN NIACIN, 4=HUSAIDIA WATU WENYE SHINIKIZO LA DAMU KUPUNGIZA UZITO, 5=ASILIMIA 80 HUWA NA MAJI,SODIAMU,MAFUTA,ASILIMIA10 FIBRE.

MADINI YA SHABA HUSAIDIA KUPUNGUZA VIJIENEZI VINAVYOSABABISHA UGONJWA WA MOYO.MADINI KAMA SELENIAMU HUSAIDA KUSAFISHA DAMU.UYOGA UKILIWA MARA MBILIZAIDI YA KILA SIKU KWA WANAUME WANAOFANYA KAZI ZANGUVU MFANO VIWANDANI UNAPUNGUZA MATATIZO YA CANCER. YA PROSTATE:NIZUNGUMZIA AINA 4 ZA UYOGA 1=AGARIUCUS BISPORUS ,HUU UNAPUNGUZA KANSA YA MATITI NA YA PROSTATE KWA WANAUME, 2=SHIITAKE -HUU UNAPUNGUZA MAFUA NA BARIDI, 3=CRIMIN HUU UNA POTASIAMU KWA WING NA UNASAIDA KUPUNGUZA MATATIZO YA MOYO, 4=LENTINAN HUU UNA UMUHIMU MKUBWA HASA UNASAIDIA KUONGEZA KINGA ZA MWILI,KUPAMBANA NA MAGONJWA NA KUPAMBANA NA VIMELEA SABABISHI VYA KANSA:Mushrooms have been used for thousands of years both as food and for medicinal purposes. They are often classified as a vegetable or a herb, but they are actually fungi. While there are over 14,000 mushrooms, only about 3,000 are edible, about 700 have known medicinal properties, and fewer than one percent are recognized as poisonous.

Many people enjoy going to the woods to pick their own mushrooms. However, identifying mushrooms can be a real challenge. The color, shape and size of the fruiting body can vary tremendously. It is important to properly identify the mushroom that is collected, so as to avoid a poisonous species.

Today, mushrooms are enjoyed for their flavor and texture. They can impart their own flavor to food or take on the flavor of other ingredients. Their flavor normally intensifies during cooking, and their texture holds up well to usual cooking methods, including stir-frying and sauteing.

It is popular to add mushrooms to soups, salads, and sandwiches, or to use them as an appetizer. They also add an appealing touch to vegetable-based casseroles and stews. In the US, mushroom extracts are increasingly being used in nutraceutical products and sports drinks.

Mushrooms contain about 80 to 90 percent water, and are very low in calories (only 100 cal/oz). They have very little sodium and fat, and 8 to 10 percent of the dry weight is fiber. Hence, they are an ideal food for persons following a weight management program or a diet for hypertensives.

Mushrooms are an excellent source of potassium, a mineral that helps lower elevated blood pressure and reduces the risk of stroke. One medium portabella mushroom has even more potassium than a banana or a glass of orange juice. One serving of mushrooms also provides about 20 to 40 percent of the daily value of copper, a mineral that has cardioprotective properties.

Mushrooms are a rich source of riboflavin, niacin, and selenium. Selenium is an antioxidant that works with vitamin E to protect cells from the damaging effects of free radicals. Male health professionals who consumed twice the recommended daily intake of selenium cut their risk of prostate cancer by 65 percent. In the Baltimore study on Aging, men with the lowest blood selenium levels were 4 to 5 times more likely to have prostate cancer compared to those with the highest selenium levels.

The most commonly consumed mushroom in the United States is Agaricus bisporus or the white button mushroom. A. bisporus has two other forms - Crimini or brown mushrooms with a more earthy flavor and firmer texture, and Portabella mushrooms with a large umbrella-shaped cap and meaty flavor.

All three mushrooms, but especially the fresh button mushrooms, possess substances that inhibit the activity of aromatase (an enzyme involved in estrogen production), and 5-alpha-reductase (an enzyme that converts testosterone to DHT). The latest findings show that white button mushrooms can reduce the risk of breast cancer and prostate cancer. An extract of white button mushrooms decreased cell proliferation and decreased tumor size in a dose-dependent manner. The chemoprotective effect can be seen with an intake of about 100 grams (3.5 ozs) of mushrooms per day.

Shiitake mushrooms have been used for centuries by the Chinese and Japanese to treat colds and flu. Lentinan, a beta-glucan isolated from the fruiting body of shiitake mushrooms, appears to stimulate the immune system, help fight infection, and demonstrates anti-tumor activity
 
UYOGA (MUSHROOM)• Hufanya damu kuwa nyepesi• Huzuia saratani• Hushusha kiwango cha kolestro• Huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili• Hudhoofisha virusi.
 
Nilikuwa nasumbuliwa na aleji kwa miaka mingi,sili nyama,sili mayai,.yani ilikuwa tabu tupu,mshikaji alikuwa ananishawishi kumsindikiza kunywa juisi ya uyoga(infact kulingana na maelezo ya daktari inachanganywa na kiasi kidogo cha alcohol kuextract dawa yenyewe kutoka kwenye huo uyoga),aliniambia inatibu hata na aleji,kisukari na magonjwa mengi,..siku moja niliijaribu,asubuhi nilipata relief ya ajabu..nikawa member kila siku,ila nilinotice kitu flani siku ya kwanza..

UWEZO WA KUFANYA MAPENZI unakuwa maradufu...nikagundua kwanini nilikuta watu(wanaume)kibao,wazee kwa vijana...UYOGA NI NOMA...aleji nimepona,.umaarufu wangu kitandani umeongezeka mara kumi ya ule wa awali ambao nao ulikuwa juu kama m-ashoki(make no mistake)..
 
Back
Top Bottom