Mbege nzuri inatengenezwa vipi

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,889
32,289
Wanabodi,
Naitaji msaada wenu jinsi ya kutengeneza Mbege nzuri..

Yoyote mwenye kujua naomba anielekeze jinsi maandalizi yake na vifaa gani vinavyotakiwa.

Nipeni maujanja ya kutengeneza Mbege wana JF.
 
wanabodi,
naitaji msaada wenu jinsi ya kutengeneza mbege nzuri..

yoyote mwenye kujua naomba anielekeze jinsi maandalizi yake na vifaa gani vinavyotakiwa.

Nipeni maujanja ya kutengeneza mbege wana jf.

wazo zuri,.......
 
1. uwe na ulezi (maandalizi yake nitakupa ukitaka)
2. uwe na ndizi mbivu (maandalizi yake nitakupa ukitaka)
3. pipa (mongutonyi), kata (kipata)
4. kuni
5. msesewe
6. maji (haijalishi ni safi au ni salama)

ukitaka maandalizi nitakupa kesho mida hii nawahi daladala.
 
Ntakupeleka kwa mama Judy ukajifunze from the best. Vipi unataka kuanzisha biashara?
 
1. uwe na ulezi (maandalizi yake nitakupa ukitaka)
2. uwe na ndizi mbivu (maandalizi yake nitakupa ukitaka)
3. pipa (mongutonyi), kata (kipata)
4. kuni
5. msesewe
6. maji (haijalishi ni safi au ni salama)

ukitaka maandalizi nitakupa kesho mida hii nawahi daladala.

Nashukuru sana ndugu yangu kwa maelezekezo yako mazuri.
 
MBEGE.jpg Umenikumbusha hii kitu ritz! Nimeimiss sana!!
 
Na inakuaje muda wa ku-expire ukishaitengeneza?
 
Unanunua makunduu, unaroweka kwa siku kadhaa kwenye kihondi (3 days), kisha unayapika mpaka yaive kabisa!
na kubadilika rangi kuwa dark brown! Unaacha Makundu yapoe kisha nayo unayaweka kwenye kihondi chake mpaka kesho yake
(1 DAY),
Baada ya hapo unachukua mfuko wa mahindi maarufu kama SAFLET, Unauosha vizuri uhakikishe ni msafi kabisa na haujatoboka mahali, Kifuatacho unajaza yale makunduu kidogo kidogo kwenye ule mfuko wa saflet kisha unaanza kukamua! ili kutenganisha majimaji yanayotoka kwenye makunduu na ile hard material yaani makundu yenyewe(at this stage hatuhitaji ile hard material ila yale maji maji yake tu..yanayoitwa "olea") kwahiyo unaikamua kistadi mpaka iishe na unakuta tayari yameshakaa mkao wa kumixiwa na bidhaa ingine ili upate mbege!
Bidhaa hiyo ni zao la mbege liitwalo unga wa ulezi. Huu unaupika kama uji wa ulezi hivyo hivyo halafu ukishapoa unaenda kuumix kwenye ile "OLEA"..kumbuka ili mbege iwe kali na yenye ladha nzuri mixture yote ifanyike kwenye Kihondi! , ukishamix unaiache ilale usiku kucha kabla ya kuanza kutumiwa, ..Ile waste products inayopatikana baada ya kukamua makunduu usiitupe ni chakula nzuri sana ya Nguruwe.

NB:
1)Makunduu - ni ndizi aina mbalimbali zilizowiva amabazo hutumika kupikia pombe.
zinapatikana sana masoko ya moshi sijui huko dar!
2)Kihondi - Ni chombo maalum cha kuwekea pombe kimetengenezwa na gogo kubwa la mti na kinaweza kuweka litre 80 na kuendelea za pombe.
3)Olea - Ni Juice inayotoka kwenye makunduu kwenye mchakato wa kutengeneza pombe..hii haileweshi!
Utaalamu huu niliuona kwa bibi yangu(R.i.p) kule old Moshi sango karibu na mjororoni!
 
Rej hii sio fresh kabisa. Ndio nini kunifanya nitamani kulamba screen ya hiki kitochi changu?
hahahah...inahusika sana!! mi napenda ile tamu ambayo ni fresh iliyotengenezwa siku hiyo hiyo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom