Mbatia: Spika Sitta jiengue CCM, upambane na ufisadi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
%5Cmbatialeo.jpg
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akitoa tamko la chama chake juu ya ufisadi nchini. Ramadhan Semtawa
SPIKA wa Bunge Samuel Sitta ambaye amejijengea umaarufu kutokana na msimamo wake wa kupambana na ufisadi, ametakiwa kujitoa kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuonyesha utashi wake wa dhati katika kupambana na uovu huo.

Kauli ya Mbatia inakuja baada ya Spika Sitta kunukuliwa akisema huenda Mwenyekiti wa TLP Agustine Mrema anapewa fedha kupigia debe CCM ambayo ni chama cha spika huyo.

Akingumzia kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia alisema Spika Sitta ameonyesha dhamira njema kuanika dhambi za CCM za kununua watu ili wakipigie debe chama tawala jambo ambalo, limekuwa likipigiwa kelele siku zote.

Hayo yalisemwa na Spika Sitta wakati akijibu tuhuma za Mrema kwamba spika huyo anakiuka taratibu za uongozi kwa kuzungumzia suala la Richmond nje ya Bunge.


Spika Sitta alisema; “kinachoshangaza yeye ni mwenyekiti wa TLP, lakini ni wa kwanza kuzungumzia matatizo yaliyomo ndani ya CCM, kama ameshindwa huko ni bora arejee CCM ili tupambane huku.

“Kuna uwezekano huyu bwana anapata fedha ili kuipigia debe CCM,” alisema Sitta.

Mbatia kwa upande wake alisema; “namshukuru sana Spika Sitta, amesema ukweli yeye ni mjumbe wa Kamati na Halmashauri kuu ya CCM, alipotoa kauli hii tulistuka sana.

"Lakini tunakwenda upande wa pili, kama Sitta anakiri mfumo huo ni wa kifisadi, CCM ina nunua thamani ya utu kwa fedha kitu ambacho ni dhambi kwanini na yeye asitoke CCM," Mbatia alihoji.

Mbatia alienda mbali na kufafanua kwamba Spika Sitta kama atashindwa kutoka CCM basi na yeye atakuwa ni sehemu ya ufisadi huo ambao umekuwa ukiivuruga nchi.

"Kwa kuwa Spika Sitta amejivika joho la kupambana na ufisadi tunampongeza. Tunampongeza kweli, lakini swali la kushangaza ambalo tunakosa majibu ni kwamba mheshimiwa huyu anafanya nini kwenye chama hicho, ambacho amekiri mwenyewe ni chama cha kifisadi?" alihoji Mbatia.

Mbatia alisema NCCR-Mageuzi kina ushahidi wa kutosha kwamba katiba ya nchi, sheria za nchi na sera mbalimbali za nchi ambazo zimekuwa zikitekelezwa chini ya uongozi wa CCM, ni za kifisadi.

"Hivyo ufisadi umejengeka ndani ya dola na dola yenyewe sasa inatekeleza ufisadi huo," alisema Mbatia.

Alifafanua kwamba, aina hiyo ya ufisadi hauwezi kupigwa vita kwa kutoa matamko tu wala kutunga sheria moja moja na kwamba mfumo kama huo, haurekebishwi kwa kupigwa viraka.

"Mfumo unarekebishwa kwa kuubadili na kuweka mfumo mwingine mahali pake, sasa taifa limefika pabaya sheria zinatungwa kuhalalisha ufisadi kwa njia moja au nyingine.

Katika kuonyesha dhamira ya kufumua mfumo huo, Mbatia alitangaza vigezo saba vya kiongozi bora anayepaswa kuchaguliwa na Watanzania kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Alivitaja vigezo hivyo kwamba ni pamoja na mgombea awe mcha Mungu, mzalendo na mwenye uchungu na nchi yake.

http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18492

Pia awe na ushujaa kutetea maslahi ya taifa, awe mwadilifu awe na moyo na uwezo wa kufanyakazi na aweze kukubali kukosolewa na kuthimini muda.
 
Back
Top Bottom