Mbatia aonya kuhusu mauaji ya raia

DOOKY

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
370
50
WAKATI bado kuna sintofahamu ya mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia, amewaonya Wanasiasa na Viongozi wa dini kutotoa kauli nzito ambazo zinaweza kuhatarisha amani.
Pia, Mbatia pamoja na Viongozi wengine wa vyama vya siasa nchini vimemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kukaa kikao cha dharula ili kujadili suala hilo kwa undani. Source http://dewjiblog.com/2012/09/06/mba...usu-mauaji-amepanga-kukutana-na-waziri-pinda/
 
mbatia hana jipya,anashindwa kusema ukweli kuwa serikali na ccm waache kuwaua raia.sasa dini na wanasiasa wamefanya nini???shida watu wenye ugamba ndani yao hawapendi kusema ukweli.kama wameua makusudi alitaka wasemeje.ndiyo jeshila polisi na serikali wanatufundisha ukororfi kwa kuua wananchi.
 
Mkuu Mamajack,
Pengine mleta mada hakuandika kila kitu kilichosemwa na Mbatia katika mkutano wake na waandishi wa habari. Kama anaweza kufanya hivyo, itakuwa vyema zaidi. Mbatia amezungumza kwa niaba ya TCD, chombo ambacho kinaviweka pamoja vyama vyote vya siasa vilivyo na uwakilishi bungeni (labda, hayo ndiyo makubaliano ya vyama hivyo). Katika mazungumzo yake ameeleza kusudio la vyama hivyo kwa pamoja kukutana na Waziri Mkuu kama jitihada mojawapo ya kuhakikisha Taifa letu linarejea katika amani (mauaji ya raia wasio na hatia yanakomeshwa).
Labda ni vizuri kilichoko kwenye source kikasoma (kama kuna ufafanuzi zaidi).
 
mbatia is too soft on this government...huwezi kuisema serikali iliyokupa ubunge
 
Mkuu Mamajack,
Pengine mleta mada hakuandika kila kitu kilichosemwa na Mbatia katika mkutano wake na waandishi wa habari. Kama anaweza kufanya hivyo, itakuwa vyema zaidi. Mbatia amezungumza kwa niaba ya TCD, chombo ambacho kinaviweka pamoja vyama vyote vya siasa vilivyo na uwakilishi bungeni (labda, hayo ndiyo makubaliano ya vyama hivyo). Katika mazungumzo yake ameeleza kusudio la vyama hivyo kwa pamoja kukutana na Waziri Mkuu kama jitihada mojawapo ya kuhakikisha Taifa letu linarejea katika amani (mauaji ya raia wasio na hatia yanakomeshwa).
Labda ni vizuri kilichoko kwenye source kikasoma (kama kuna ufafanuzi zaidi).
Kwani Mbatia ni Mbunge wa chama gani? anawakilisha chama gani Bungeni? Kauli yake haitofautiani na ya Nape Nnauye.
 
wakati bado kuna sintofahamu ya mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha channel ten, daudi mwangosi, mwenyekiti wa kituo cha demokrasia tanzania (tcd), james mbatia, amewaonya wanasiasa na viongozi wa dini kutotoa kauli nzito ambazo zinaweza kuhatarisha amani.
pia, mbatia pamoja na viongozi wengine wa vyama vya siasa nchini vimemtaka waziri mkuu, mizengo pinda kukaa kikao cha dharula ili kujadili suala hilo kwa undani.
mi nashangaa sana, hiyo sintofahamu iko wapi? Mbona humu jf watu tunamjua muuaji na ushahidi wa picha umeishawekwa. Hata kama bomu lilitoka kwingine lakini kafia mikononi mwao, cha kushangaza walikuwa wamemzunguka na cha ajabu bomu likapenya na likamfikia mwangosi.
 
Back
Top Bottom