Mbatia amvua Uongozi wa 'Katibu Wanawake NCCR' Bi Amina!

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,890
382
James Mbatia amemvua uongozi Wa Katibu Wanawake Bi Amina kwa kosa la Kusaini Waraka wa kutaka Mbatia atolewe Uenyekiti Taifa!

Bi Amina tayari amesha kabidhiwa barua hiyo na Kambi Ya Mbatia inaendelea kutengua uteuzi wa wajumbe wote walioteuliwa na Mbatia kama kitisho ili kuepuka kundi la kumtoa.

Leo kuna kikao cha wenyeviti na Makatibu Mikoa kinaendelea ktk Ukumbi wa Katoliki Bunju.

Mbatia anafanya njama za kumuvua uanachama Kafulila.
 
Kiongozi anatakiwa awe na maamuzi sahihi, yanayotakiwa kuchukuliwa kwa wakati.

Big up Mbatia kama hao watu walikuwa na nia ya kuleta makundi ndani ya chama.
 
Kama wanaondolewa kwa kukiuka katiba ya chama ni sawa lakini kama ni kwa hisia ya mwenyekiti itakuwa mbaya. Dr Slaa alisema Kafulila ni sisimizi sasa mmeona yanayompata]
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hivi kama hutakiwi lazima uwepo?

Hivi James Mbatia ANAFANYA KAZI AU BIASHARA GANI?
 
James Mbatia amemvua uongozi Wa Katibu Wanawake Bi Amina kwa kosa la Kusaini Waraka wa kutaka Mbatia atolewe Uenyekiti Taifa!

Bi Amina tayari amesha kabidhiwa barua hiyo na Kambi Ya Mbatia inaendelea kutengua uteuzi wa wajumbe wote walioteuliwa na Mbatia kama kitisho ili kuepuka kundi la kumtoa.

Leo kuna kikao cha wenyeviti na Makatibu Mikoa kinaendelea ktk Ukumbi wa Katoliki Bunju.

Mbatia anafanya njama za kumuvua uanachama Kafulila.

Sijui mambo ya NCCR lakini kwa mwendo huu wa kuvuana kila kukicha naona kama mwisho wa Mbatia uko ukingoni!! Ukiona watu wanakaribia Ikuku utasikia mkuu wa Nchi kamvua huyu madaraka mara yule. Nadhani kwa Kamanda Mbatia maji yako shingoni anataka kuzuia UASI kwa nguvu yoyote ile. Kama hali ni hiyo basi uasi ni mkubwa ndani ya Chama na sijui nini kitamnusuru.
 
Mbatia ni jasiri, jino likipata ugonjwa ni KUNG'OA tu ndiyo dawa muafaka. Twawashangae Mbowe anachukua muda mrefu KUMPIGA chini SHIBUDA
 
Kafulila na Hamad Rashid walikuwa bega kwa bega na wabunge wa ccm kubadilisha tafsiri ya 'kambi rasmi ya upinzania bungeni' kinyume na taratibu za mabunge ya madola. Hatua hii ilichukuliwa kwa makusudi kabisa ili kuzima nguvu ya CHADEMA lakini baada ya hapo akaanza kujiweka karibu na CHADEMA!

Pili, sikuelewa ni vigezo gani alivyotumia kumteua huyu Kafulila kuwa mjumbe wa 'nyongeza' kwenye kamati ya katiba na sheria?

Huyu kijana yuko kwenye hatari ya kuwa Lyatonga Mrema wa kesho! Mrema amekuwa mtalii kwenye vyama vya siasa na kila aingiapo lazima ugomvi uzuke.
 
huyu kaisha sana bora akubali kuachia ngazi asiwe kama Mrema na TLP ambaye hata kama anaongoza vibaya asiambiwe, ukiongea anakufukuza na ngumi juu
 
Kiongozi anatakiwa awe na maamuzi sahihi, yanayotakiwa kuchukuliwa kwa wakati.

Big up Mbatia kama hao watu walikuwa na nia ya kuleta makundi ndani ya chama.
Vipi kesi ya Mhs Halima Mdee mbunge wa Kawe alishaifuta mahakamani???????? Mganga nja tu huyo Bwn Kafulila ukiona unaminywa mbona CDM ni nyumbani????????

Hao mpaka wamalizine na kukaa sawa wenzao watakuwa mbali sana,ndugu zao wa CUF nao mambo si shwari.
mmmmh!kweli magamba noma!
 
Hizo ndio dynamics za ujenzi wa chama chochote na sio jambo la ajabu. Kuenguana na counterkuenguana ni moja ya mikakati ya kujenga au kubomoa chama. NCCR ipo katika critical stage ya either kujifunza kwa haya na kujivua gamba au kupotelea ughaibuni kisitambe tena milele amina. Ni swala la kusuka au kunyoa!
Mungu ibariki Bongo yetu.
 
Jamani achaeni kuwa na migogoro ndani ya chama, Migogoro mara nyingi inadhofisha Chama, leo mkiendelea na huo mgogoro mjue kwamba mwaka 2015, kutakuwa na shida sana hasa kupata nafasi za ubunge katika chama chenu katika mjimbo mbalimbali kaaeni ulizaneni wapi mnatofautiana. Nchi hii tunahitaji vyama vingi ili tuweze kusonga mbele leo ikiachwa ccm peke yake watafuja sana mali asili zetu kwa kisingizio cha wawekezaji.
 
Sijui mambo ya NCCR lakini kwa mwendo huu wa kuvuana kila kukicha naona kama mwisho wa Mbatia uko ukingoni!! Ukiona watu wanakaribia Ikuku utasikia mkuu wa Nchi kamvua huyu madaraka mara yule. Nadhani kwa Kamanda Mbatia maji yako shingoni anataka kuzuia UASI kwa nguvu yoyote ile. Kama hali ni hiyo basi uasi ni mkubwa ndani ya Chama na sijui nini kitamnusuru.

Mbatia ni kamanda? Duh kweli kila mtu na shujaa wake..
 
Mbatia ni jasiri, jino likipata ugonjwa ni KUNG'OA tu ndiyo dawa muafaka. Twawashangae Mbowe anachukua muda mrefu KUMPIGA chini SHIBUDA

Mbowe mjanja ,anamchukulia Shibuda kama kondom, matumizi yake yakiisha unatupa chooni.
 
Back
Top Bottom