Mbatia alinganisha kuteuliwa kwake kuwa Mbunge na CHADEMA-Mtwara

ubwabwa asili yake ni kuliwa na watu wa mwambao yani hadi huko mtwara,wale wa pembezoni mwa bahari wanapenda sana ubwabwa..tena wa nazi
 
kesi yake na kafulila imeishia wapi? au baada ya kupewa ubunge imeisha??2015 atagombea jimbo gani au ataubiri tena kiti cha huruma kama cha sasa??

Kuhusu Kafulila alisema hakumuomba samahani angemsamehe ,mbona Halima Mdee aliomba samahani mbele ya Waandishi wa habari nikamsamehe nikafuta kesi.
 
Kweli huyu jamaa kachoka. Tatizo lake ni mastres yaliyotokana na azma ya moyo na nafsi yake ya kutaka kuwa kiongozi badala ya uongozi. Kwisha kazi....juzi alipigwa chini na Mdee sasa 2015 sijui atagomea wapi. Je, ni Mtwara ama Vunjo? Kwa uzembe huu wa kujenga hoja huyu braza kaka wa Iwa Kirua Vunjo almaarufu kama KV London aende zake kwao akalime kahawa na mdizi za kuuza KNCU au Rindima kama alisili.

Kwakweli stress ni hatari.
 
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia aliwacharukia wasomi wa vyuo vikuu kwa kuwaambia kuwa wanapaswa kuonyesha katika jamii kuwa ni watu wameelimika na siyo waliyokariri vitabu tu katika usomi wao

Kejeli hiyo nzito kwa wasomi hao aliitoa Jumanne jioni wiki hii kwa jazba katika mkutano wake wa hadhara uliyofanyika soko kuu mjini Mtwara wakati akijibu maswali yaliyoulizwa na wanachuo wa chuo kikuu kishiriki cha SAUT cha Stella Maris Mtwara ya kukubali uteuzi wa Rais kuwa mbunge.

“Achana na siasa chafu majitaka nyepesi nyepesi zilizopitwa na wakati, mbona Prof. Baregu Chadema ameteuliwa na Rais Tume ya Katiba hamhoji na zito kabwe tume ya madini je ni CCM” Mbatia Aliuwauliza kwa kufoka.

Maswali hayo yaliyoonyesha kumchefua Mbatia kutokana na umati mkubwa waliyokuwepo kuripuka kwa shangwe kubwa kuwashangilia vijana hao waliyokuwa wanamtwanga maswali hayo ya kutaka kujua ajenda aliyonayo ya ndoa yake ya kisiasa na serikali ya CCM.


Vijana hao waliuliza maswali hayo baada ya hutoba yake iliyoonekana kuwakera wengi kutokana na madai ya kuwa serikali ya CCM haijafanya kitu cha maendeleo katika mikoa hii na ya Bandari Mtwara kuuza kwa wawekezaji.

Mwanachuo Yusufu Nanyambo na Peter Justine wa Chuo kikuu hicho katika maswali yao walimtaka Mbatia kuwafafanulia wanainchi kukubali kwake kuteuliwa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama kilichopo madarakani bungeni atakuwa upande gani.
Walimtaka kuwaeleza atakuwa mtetezi wa serikali aliyofunga nayo ndoa ya kisiasa au upinzani unaoikosoa serikali ambayo yeye imwona anafaa kuitetea ukilinganisha na maelefu ya wanachama CCM walionao.

Vijana hao huku wakishangiliwa na umati huo wa watu walionekana kumchefua zaidi Mbatia walipokumbusha tuhuma za Halima Mdee na Kafulila za kuwa anatumika CCM ndani ya Upinzai na kuwataka wananchi wasimwamini.


“Hii sasa inathibitisha bila kuacha shaka yo yote tuhuma zile za Mdee na Kafulila je kwa nini tusiamini kuwa umeteuliwa kwenda kudhoofisha upinzaini bungeni kama wanavyoonekana wengine?” Alimhoji Jastine huku akishangiliwa.

Mbatia aliwataka wasomi hao kutumia uhuru wao wa kutakari mambo ya kitaifa na kutoa maoni yao vizuri kwa kuzingatia taaluma na kuonyesha kuwa wao wameelimika na siyo watu waliyokariri vitabu tu.

Alisema katika katiba ya Jmahuri ya Tanzania ibara 16 kifungu 66 kifungu kidogo cha 1.A kinampa mamlaka ya Rais kuteuwa wabunge 10 kuingia katika bunge la Jamhuri ya Tanzania kifungu hicho hakisemi kuwa ni wa Chama tawala pekee.

Mbatia aliendelea kutoa mifano mbali mbali ikiwemo ya Prof. Baregu kuteuliwa katika tume ya Katiba na Zito Kabwe katika tume ya madini na kuhoji wakiwa katika kamati hizo wanamwakilisha nani Chadema au Rais wa Serikali aliyewateuwa.

Hata hivyo pamoja na Mbatia kutumia muda mwingi kulelezea jamabo hilo na kuwataka watu wasimhukumu au kumpima kwa nadharia bali vitendo bado wengi wakiwemo wasomi hao hawakuridhika.

Walidai kuwa mifano aliyoitoa haiendani na hicho alichonacho yeye kwa sababu hiyo nafasi ni ya kisiasa na siyo ya kiutendaji kama tume.

Aitha wengi walimkosoa kwa kudai kuwa serikali ya CCM hakufanya cho chote cha maendeleo mikoa ya kusini kwa kusema amewaona watu wa mikoa ya Mtwara na Lindi hawaoni na hawaelewi.

“Hivi huyu haoni umeme wa gesi huu barabara daraja la Mtambaswaala na uwekekazaji wa viwanda na gesi asilia?” Alisema Ahmedi Juma wa Soko kuu mjini Mtwara

Mkasa wa Mbatia katika mkutano huo ambao ni wapili katika eneo hili hili la soko kuu katika kipindi cha miezi miwili iliyopita ulianzia pale alipokosa watu waliyodaiwa kujiunga na chama hicho na kuwa tayari kukabidhiwa kadi juzi katika mkutano huo.

Ukimwacha mwanachama mmoja kutoka CUF alijitokeza na kupokea kadi yake wengine waliitwa kwa muda mrefu bila kutokea na hivyo kuwaambia waende wakachukuwe kadi zao ofisini hali ambayo ilidaiwa walidanywa tu


Taarifa hii imeandikwa na mimi mwenyewe Chitembedya nilikuwa katika mkutano tangu mwanzo hadi mwisho.
 
Haya kaka kwanza hongera kwa taarifa. Pia natoa wito kwa mbatia asikose kuhuthuria m4c, jangwani, kwani atapitwa na mengi
 
Mbatia sasa majukwaa yatakuwa moto kwako. it is a total confusion kuwa mbunge wa kuteuliwa na sisiem. unasimamia wapi?
 
basi mie nikajua analumbana kuhusu suala la ushoga.... maana wanamzushia ati yeye ni mdau muhimu sana kwenye suala la ushoga
 
Back
Top Bottom