Mbatia akubali yaishe kwa Mdee

Sumasuma

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
342
110
Raymond Kaminyoge
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na NCCR-Mageuzi vimetangaza kurejesha upya ushirikiano wa karibu yanayohusu masuala mbalimbali yenye maslahi kwa wananchi.Katika kuanza utekelezaji wa ushirikiano huo, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amefuta kesi aliyomfungulia mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee akimtuhumu kutumia kampeni chafu wakati wa kampeni ambazo zilimuathiri.

Mbatia alimfungulia Mdee kesi hiyo namba 101, Novemba mwaka 2010, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akitmtuhumu mbunge huyo pia kwamba alitumia lugha ya ubaguzi dhidi yake.Jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza waliwaambia waandishi wa habari kwamba kesi hiyo imefutwa.Katika mkutano huo uliofanyika ofisi za NCCR-Mageuzi Ilala, jijini Dares Salaam, Ruhuza na Dk Slaa waliambatana pamoja.

Makatibu hao walisema hayo mbele ya Wakili Mohamed Tibanyendela aliyekuwa akimwakilisha Mbatia na Wakili Edson Mbogolo anayemtetea Mdee.

Akizungumza kwa niaba ya vyama hivyo, Dk Slaa alisema kesi hiyo imefutwa baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya vyama hivyo viwili.“ Kwa kweli vyama hivi vimefikia muafaka kwamba, kesi hii ifutwe kwa sababu ya maslahi ya wananchi wa Kawe na Watanzania kwa ujumla,”alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema uamuzi huo ulifikiwa baada ya vyama hivyo kubaini kwamba, lengo kuu la chama chochote cha upinzani ni kukiondoa madarakani chama kinachotawala nchi

“ Tumeing’oa CCM katika Jimbo la Kawe wananchi walikuwa wakitaka chama cha upinzani, sasa wapinzani kuendelea kupelekana mahakamani hatutakuwa tunawatendea haki wakazi wa Jimbo la Kawe,”alisema Dk Slaa.
Aliongeza kuwa hata kesi hiyo ikiendelea na Mbatia akashinda, ukiitishwa uchaguzi mdogo ni gharama kubwa ambazo zitabebwa na Watanzania.

“ Ndiyo maana katika uamuzi tuliofikia tumeamua kulenga zaidi maslahi ya wananchi badala ya mtu mmoja mmoja au ya chama,”alisema Dk Mbatia. Alisema mfumo wa kimahakama unatambua usuluhishi wa kesi nje ya mahakama na kwamba, unapunguza gharama za uendeshaji wa kesi ambazo ni mzigo kwa walipakodi.
Hata hivyo, licha ya kukwepa gharama za chaguzi ndogo, Dk Slaa alisema vyama hivyo havitasita kuchukua hatua za kinidhamu ikiwemo kuwafukuza uanachama wanachama watakaokwenda kinyume na maadili ya chama hicho.

“ Hatutaki kufanyika kwa chaguzi ndogo kwa lengo la kukwepa gharama, hii isitumike kwa viongozi kwenda kinyume na maadili, wakikiuka tutawafukuza tu uanachama,”alionya Dk Slaa.Alisema baada ya kufutwa kwa kesi hiyo, vyama hivyo vitaendelea na ushirikiano katika mambo mbalimbali ambayo watadhani yatakuwa na maslahi kwa wananchi ikiwa watashirikiana.

Kauli ya NCCR-Mageuzi
Naye Ruhuza alisema kufutwa kwa kesi hiyo kunaonyesha namna vyama hivyo vilivyo na lengo moja kuu la kuiondoa CCM madarakani.“ Baada ya makovu haya ya uchaguzi kufutwa, tutaendelea kuangalia maeneo mengine ambayo vyama vyetu vinaweza kushirikiana,” alisema Ruhuza.

Ruhuza alisema baada ya kufutwa kwa kesi hiyo, gharama za kesi hiyo zitagharamiwa na chama husika.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Mbatia, Hemed Kanoni na Solomon Lufunda dhidi ya Mdee, Mwanasheria wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kawe.Hati ya kufutwa kwa kesi hiyo ambayo imesainiwa na pande zote iliwasilishwa jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Katika makubaliano ya vyama hivyo viwili, pia imekubalika kwamba visishambuliane wala kuchafuana kwa namna yoyote ile mbele ya umma.

:lol:
 
Pongezi nyingi kwa James Mbatia, Huu ni uamuzi unaokomaza demokrasia.

Together as one!!!!!!
 
Back
Top Bottom