Mbarali Kwafukuta

leta uzibitisho sio ushabiki na udaku

mimi niko huku hakuna kitu cha namna hiyo

Uzuri wako ni kwamba matukio mengi yanayotokea na kuripotiwa hapa, wewe unapinga na kudai uko sehemu hiyo!!!! Hii inakuwaje wewe upo kila mahali?

Very interesting!!!!

Tiba
 
Nimepokea taarifa nyingine kuwa FFU wamechemka kuwatawanya wananchi ambao wamefunga barabara kuu inayounganisha makao makuu ya wilaya (Rujewa) na Mbarali rice farms katika mji mdogo maarufu uitwao Ubaruku. Polisi wamerudi kituo kikubwa cha wilaya cha polisi mjini Rujewa, sijui wanakusanya nguvu au vipi. Mtoa taarifa anasema watu wamekusudia kuyarejesha mashamba mikononi mwa wananchi kwa nguvu kwani wansemezana "kama misri na Libya".
Source: eye witness
 
Uzuri wako ni kwamba matukio mengi yanayotokea na kuripotiwa hapa, wewe unapinga na kudai uko sehemu hiyo!!!! Hii inakuwaje wewe upo kila mahali?

Very interesting!!!!

Tiba

Achana naye unaweza ukajikuta unajibizana na mr. Ibilisi ndio maana mi nimempotezea
 
Mbarali ni nyumbani kwetu,hivyo tunasikia mambo hayaendi sawa,ni lazima tuhoji na kudadisi ili tujue ukweli wa mambo.na kama ni kweli kwamba kuna hali tete inayohusisha suala la shamba lililokodishwa kwa mwekezaji,basi hapo kuna tatizo tena tatizo kubwa.na kama serikali yetu ni sikivu,basi tunatarajia itaheshimu matakwa na wananchi.
 
Nimepigiwa simu na rafiki yangu ambaye yupo Mbeya Wilaya ya Mbarali kuwa vikosi vya FFU vimepiga kambi kule baada ya wananchi kuzuia mwekezaji wa mashamba ya mpunga (NAFCO) kuondoa machine ya kukoboa mpunga iliyokuwepo pale shirikani muda mrefu. Wananchi wanadai ni mwekezaji ni wa muda tu na kila kitu amekikuta na hakuna kuondoka na kitu na wamefunga barabara toka jana hali iliyofanya polisi wa wilayani hapo kuomba msaada wa polisi zaidi kutoka makao makuu ya mkoa ambao wamemwagwa leo pale wakiwa full na bendera nyekungu mikononi.

Inasemekana yamepigwa baadhi ya mabomu ya machozi na kuwakamata baadhi ya viongozi wa wananchi jambo ambalo limeamsha hasira za wananchi hao na sasa wanasema wanalitaka shamba lote lililochukuliwa na mwekezaji huyo. wanadai hakuna kulala hadi hadi haki itendeke.

Mwenye habari zaidi tafadhari tumwagie.

Source: Eye witness

Ndiyo ni haki yenu hakikshen wanachukua ilo shamba. Haya na hapo vp CDM wamechochea mana cxx ndo zao kutulalamikia. Iyo ndo kaz ya pipoz power!
 
Tokea achukue hilo shamba amewekeza kiasi gani? Kwa nini anawakodishia wananchi shamba wakati amepewa ili alilime kibiashara?

Wananchi wa Mbarali wana kila sababu ya kumfanya huyo muwekezaji alikimbie hilo shamba kwani ardhi hiyo ilikuwa yao kabla ya kuipa serikali enzi za Nyerere kufungua mashamba ya serikali chini ya NAFCO; ilikuwa busara baada ya sera za nchi kubadilika serikali ilitakiwa kuwarudushia wananchi ardhi yao ili waendelee kulima mpunga badala ya kumuuzia huyo muhindi kwa bei ya kutupa!! Nawaunga mkono wananchi wa Mbarali kwa kudai kile lilicho chao!! ALUTA CONTINUA!!
 
Back
Top Bottom