Mbaguzi Ismail Jussa Anapozidi kufunguka..

Msajili

Senior Member
Apr 1, 2012
116
38
Hii nimeipata kwenye wall yake ya Facebook.

Uchaguzi mdogo wa Bububu: Mengi yamesemwa toka jana. Naziona hamaki na hasira, nazihisi hisia za kukata tamaa na kutafishika. Uchaguzi wa Bububu ulikuwa ni zaidi ya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Mwakilishi. Haukuwa uchaguzi kati ya CUF na CCM kama wengi walivyodhania au walivyoutazama. Ulikuwa ni mfano wa kura ya maoni ndogo kuhusu mwelekeo wa nchi yetu. Ulikuwa ni uchaguzi kati ya wapenda maridhiano na wayachukiao. Ulikuwa ni uchaguzi kati ya wapenda maendeleo na wahafidhina. Lakini kubwa zaidi ulikuwa ni uchaguzi kati ya wanaotaka Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na wale vibaraka wanaotaka Zanzibar iendelee kuwa koloni la Tanganyika. Umma ulipoonekana kuwa upande wa wanaopenda maridhiano, wanaotaka maendeleo na wanaoitaka Zanzibar yenye mamlaka kamili, watawala wakijumuika kati ya vibaraka waliopo Zanzibar na wakoloni wanaowatumikia wakaamua kutumia nguvu kubwa ili kujaribu sauti ya nguvu hiyo isitoke. Wasichokijua ni sauti imetoka na imesikika, tena bila ya kisisi.

Balozi Seif Ali Iddi (katika comment moja jamaa alimwita Balozi wa Tanganyika nchini Zanzibar) na wenziwe wanaotumikia agenda ya Tanganyika hapa Zanzibar walidhani kwa kutumia nguvu ile kubwa watatuyumbisha na kutuhamakisha tuivunje Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo yeye na wenzake hawakuahi kuiamini wala kuiunga mkono na kwa kufanya hivyo wakadhani watafanikiwa kuyavunja maridhiano na umoja wa Wazanzibari.

Wakadhani wakifanikiwa katika hilo watakuwa wamevunja umoja na ari ya Wazanzibari kudai nchi yao. Wamepwerewa wao na mabwana wanaowatumikia. Akili zetu razina. Haondoki mtu kwenye mstari. Tutayalinda maridhiano na umoja wa Wazanzibari. Na tutalilinda na kulipeleka mbele vuguvugu la Wazanzibari linalojumuisha makundi na taasisi tofauti kuirudisha Zanzibar yetu.
 
Hii nimeipata kwenye wall yake ya Facebook .

Uchaguzi mdogo wa Bububu: Mengi yamesemwa toka jana. Naziona hamaki na hasira, nazihisi hisia za kukata tamaa na kutafishika. Uchaguzi wa Bububu ulikuwa ni zaidi ya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Mwakilishi. Haukuwa uchaguzi kati ya CUF na CCM kama wengi walivyodhania au walivyoutazama. Ulikuwa ni mfano wa kura ya maoni ndogo kuhusu mwelekeo wa nchi yetu. Ulikuwa ni uchaguzi kati ya wapenda maridhiano na wayachukiao. Ulikuwa ni uchaguzi kati ya wapenda maendeleo na wahafidhina. Lakini kubwa zaidi ulikuwa ni uchaguzi kati ya wanaotaka Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na wale vibaraka wanaotaka Zanzibar iendelee kuwa koloni la Tanganyika. Umma ulipoonekana kuwa upande wa wanaopenda maridhiano, wanaotaka maendeleo na wanaoitaka Zanzibar yenye mamlaka kamili, watawala wakijumuika kati ya vibaraka waliopo Zanzibar na wakoloni wanaowatumikia wakaamua kutumia nguvu kubwa ili kujaribu sauti ya nguvu hiyo isitoke. Wasichokijua ni sauti imetoka na imesikika, tena bila ya kisisi. Balozi Seif Ali Iddi (katika comment moja jamaa alimwita Balozi wa Tanganyika nchini Zanzibar) na wenziwe wanaotumikia agenda ya Tanganyika hapa Zanzibar walidhani kwa kutumia nguvu ile kubwa watatuyumbisha na kutuhamakisha tuivunje Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo yeye na wenzake hawakuahi kuiamini wala kuiunga mkono na kwa kufanya hivyo wakadhani watafanikiwa kuyavunja maridhiano na umoja wa Wazanzibari. Wakadhani wakifanikiwa katika hilo watakuwa wamevunja umoja na ari ya Wazanzibari kudai nchi yao. Wamepwerewa wao na mabwana wanaowatumikia. Akili zetu razina. Haondoki mtu kwenye mstari. Tutayalinda maridhiano na umoja wa Wazanzibari. Na tutalilinda na kulipeleka mbele vuguvugu la Wazanzibari linalojumuisha makundi na taasisi tofauti kuirudisha Zanzibar yetu.

Maneno ya Jussa yako juu ya mstari wala hajakosea.Kama mtu kutetea utu wake na nchi yake ni ubaguzi basi wabaguzi tupo wengi. Tunajua fika Seif Ali Iddi ni Balozi wa Tanganyika nchini Zanzibar na Sheni na wenzake ni Vibaraka. Wazanzibar hatutoki kwenye mstari, tutasimama pale pale ''Jamuhuri Ya Watu Wa Zanzibar Kwanza''
 
Bora al shaababu kuliko anaeuwa vikongwe na albino, uko wapi ustaarabu na ubinaadamu Danganyika!
 
Jusa anawanyima usingizi eeh!!!
Hiyo post si ya Jussa ni ya Salma Said wa Mwananchi msikurupuke!!!!
 
Jusa anawanyima usingizi eeh!!!
Hiyo post si ya Jussa ni ya Salma Said wa Mwananchi msikurupuke!!!!
Mkuu asante kwa rekebisho hilo, ila hawezi tunyima usingizi labda pale tutakapoanza kudai Pemba yetu maana hakuana andiko lolote linaloonyesha ni lini tuliungana na Unguja.
 
Jusa mbona ni mwehu tu! nani bado anamsikiliza. kama mmeungana kisha mnapingana namna hiyo kwa nini kung'ang'ania muungano huo (namaanisha muunganiko wa CCMCUF). Njaa na uendawazimu......ukichanganya na yale mambo mengine = Jusa
 
Tulishamzoea huyu al shabaab,Sijuikwenye bunge la jamhuri anatafuta nini?

Jussa alikua mbunge wa kuteuliwa na Rais nadhani kwa mwaka mmoja ktk bunge la 2005 - 2010! Siku hizi yupo BLW Zanzibar akiwakilisha jimbo la Mji Mkongwe! Sioni makosa ya mwandishi pengine kama wewe unafaidika na huu muungano wa kinyonyaji! Akina Shein na balozi Seif Iddi ni vibaraka wa CCM wanaotawala Zanzibar!
 
Jusa anafany kinachotushinda wengi..... yeye sio mnafiki, ana uwezo na uthubutu

mimi sipendi zanzibar iwe kwenye muungano, napenda zainzibar kama leisure destination tu

mfumo uliopo unawafanya wawe wavivu, wanatucost tu na hawana chochote cha ziada ambacho ni lazima tuwe nao kwenye muungano. wakiwa huru wataenda mbaili zaidi, watatuheshimu zaidi, watatupenda zaidi na mimi ntapenda zaidi kwenda zanzibar kutembea

SIUPENDI MUUNGANO KWA MOYO WANGU WOTE, LAKINI NAWAPENDA WAZANZIBARI NA UTU WAO.... MUUNGANO UNAWAMALIZA, UNAWANYIMA NAFASI, NA PIA UNATUNYAMAZISHA NA KUTUNYIMA MAFASI KAMA TANZANIA BARA KUFANYA MAMBO YETU..... MUUNGANO UMEKUA NDOA YA MITALA

WAUVUNJE TU, TUENDE ZANZIBAR KWA PASSPORT, LABA HESHIMA ITARUDI
 
Nimesoma bandiko la Ismail Jussa sijaona ubaguzi wowote zaidi ya kutetea Zanzibar yao kama sisi tunavyotetea Tanganyika yetu, mleta huu uzi naomba kukuuliza Tundu Lissu naye ni mbaguzi. Alichokisema Jussa ndio alichokisema Lissu.
 
Nimesoma bandiko la Ismail
Jussa sijaona ubaguzi wowote zaidi ya kutetea Zanzibar yao kama sisi
tunavyotetea Tanganyika yetu, mleta huu uzi naomba kukuuliza Tundu Lissu
naye ni mbaguzi. Alichokisema Jussa ndio alichokisema Lissu.

kama ni hivyo kwanini wazanzibari wanamchukia sana Tundu Lissu kuanzia bungeni hadi mitaani?
 
Hakuna ubaguzi katika hilo ni ukweli mtupu, kwani hiyo ni haki yake ya kuongea lile ambalo analiona ndani ya moyo wake lipo right....hata mm namuunga mkono Mheshimiwa Jusa....Kwanza Zanzibar muungano baadae.........
 
Najifunza kuwa great thinker. Kwa kuzungumzia itikadi tu wakati anasema uchaguzi huu ulikuwa zaidi ya kuchagua mwakilishi huku akiacha kuzungumzia ushindi wa hao anaowalaumu una maana gani, inaonesha upungufu wa kiufahamu. Kama angekuwa mkweli angekubali kuwa kwa ushindi wa hao akina Balozi Idd, maana yake ni kuwa wengi wao bado wanataka muungano (kutawaliwa na wakoloni, kama Jussa anavoiweka).

Kama anadhani kulikuwa na hila katika ushindi wa CCM, ni vema akazungumzia hilo. Kwenye ballot box, mawazo yake yameshindwa!!

Sipendi Muungano lakini ninaungana na utaratibu uliopo wa kutumia kura. Ninakubali kuwa wanaotaka Muungano kwa kupitia CCM wameshinda!!
 
kwa sababu alijaribu kuifuta nchi yao kwenye ramani ya dunia kwa kusema Zanzibar sio nchi,lilikua kosa kubwa sana kwa wazanzibar na wakiipta nchi yao hataruhusiwa kukanyaga huko wameapa.
 
Back
Top Bottom