Mbabazi aahidi kurejesha mwili wa Idi Amin

Primier

Member
Dec 16, 2015
86
14
160210132724_idi_amin_dada_624x351_bbc_nocredit.jpg

Marehemu Idi Amin Dada aliiongoza Uganda kwa miaka minane kati ya mwaka wa 1971 hadi 1979

Mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini Uganda ameahidi kurejesha nyumbani mabaki ya aliyekuwa rais wa nchini hiyo Idi Amin Dada na kuujengea makavazi.

Aliyekuwa waziri mkuu wa Uganda Amama Mbabazi,alisema endapo atachaguliwa kuwa rais azimio lake la kwanza itakuwa kuwapatanisha waganda wa kila tabaka na kabila.

Kwa madhumuni hayo anapanga kuwaleta pamoja watu anaohisi kuwa wanaomuunga mkono Idi Amin wale waliomuunga mkono Milton Obote na wale wanaomuunga mkono rasi wa sasa Yoweri Kaguta Museveni.

Viongozi hao watatu ndio waliochangia kwa njia moja au nyengine mwelekeo wa kisiasa wa Uganda.

Image caption Amama Mbabazi ameahidi kurejesha nyumbani mabaki ya aliyekuwa rais wa nchini hiyo Idi Amin Dada na kuujengea makavazi.
Marehemu Idi Amin Dada aliiongoza Uganda kwa miaka minane kati ya mwaka wa 1971 hadi 1979 utawala ambao ulishuhudia mauaji ya wapinzani wake wengi.

Vilevile anatuhumiwa kwa kuwatimua wahindi wote nchini Uganda kabla ya kupinduliwa na Milton Obote.

Marehemu Idi Amin aliaga dunia akiwa uhamishoni nchini Saudi Arabia.

Rais Yoweri Museveni, anatarajiwa kuchaguliwa tena kuongoza taifa hilo la Afrika Mashariki kwa hatamu ya tano.


Chanzo: BBC
 
Wanafanya uchaguzi kupoteza muda tu kama ilivyo nchi nyingi za Afrika. Hapo Museveni atatawala hadi mauti yatakapomfika
 
Waganda wenyewe watajua wamchague yupi. Huyu anaahidi kuleta masalia ya mwili wa Idi Amin yule anatunga "vesi" kuwavutia wapiga kura. Hii ndiyo raha ya demokrasia. Wapumbavu hupata chaguo wanalostahili.

Vituko na vibweka East Afica.
 
Amama Bwana! kuleta mwili wa marehemu Amini kutasaidia nini sasa wananchi?? ila hata aseme nini kupata urais ni ndoto labda Besgye
 
Ila mbwembwe na ujasiri wa Idd Amin Dadaa.....ni vitu vinavyotakiwa kutu ''inspire'' wa afrika tunaojitambua.
 
Amama Bwana! kuleta mwili wa marehemu Amini kutasaidia nini sasa wananchi?? ila hata aseme nini kupata urais ni ndoto labda Besgye
Mhhh !! LAKINI Mrhm. Iddi Amin alitutia Tanzania ktk madeni hadi leo yanatuandama...!!
nzalendo Bado tunatibu donda ndugu (vita vya kagera kwa kulipa riba la deni ) !!
 
Naaum ... lakini propaganda za mataifa makubwa ndizo zilizo sababisha yale tatokee....Kwa mfano.Leo kikinuka BUja au Congo si wao ni wazungu.....
 
Nyerere alishikwa hasira zaidi Juu ya telegram aliyotumiwa na nduli Iddi Amini

"Ktk barua hiyo dada alimwambia mchonga hivi; Nataka nikuhakikishie kwamba nakupenda sana, na kama ungelikua mwanamke basi ningefikiria jinsi ya kukuoa Japo kichwa chako kimejaa mvi. Lakini kwakuwa ww ni mwanaume basi uwezekano huo haupo"
 
Miafrica bana!!..sasa aurejeshe ili iweje?..kwan tatizo la waganda hasa ni mifupa ya Idd Amini?
 
Back
Top Bottom