Mazungumzo ya kamati ya CHADEMA na Jakaya kwa ufupi

Inaonekana hutuba za huyu Dr mh JK, ww ndo huwa unamuandaliaga maana... tehe tehe tehe
 
Mkuu wewe ni mbunifu lakini umeyakatisha hayo mazungumzo.
Hiyo imekamilika mkuu. subiri uone Chadema watakavyotoka uko wako disappointed. Never will he adress serious
issues seriously.
 
Nahisi hawezi kuwa peke yake
atakuwa na
-wasira aka tyson
-kingunge aka tps
-celina aka kombania
-....................
...................
....................
 
Hii ni ya hapa hapa. Agenda Yangu ni kudadavua kama Mkutano huu utawezesha Mswada kurudishwa kwa
wananchi on the way back to Bungeni au ni porojo tuu
Nimeipenda lakini mbona kikao mwanzo hadi mwisho ni maneno machache hivyo?

Unawajuwa wote waliohudhuria kikao?

Naona pia kama wamezungumzia zaidi kuhusiana na Arusha na Lema kuliko katiba ambapo nilidhani ndo the main agenda?
 
Kikwete: Kwanza napenda kuwashukuru kwa kuonesha njia njema kabisa ya Kuzungumzia Mustakabali wa
Katiba ya nchi yetu. Kwa kweli nimefarijika sana na ninawapongeza sana kwa moyo wa kizarendo
Mliouonyesha.

Kikwete: Pili naomba tusahau yote yaliyopita hasa ukizingatia ukweli kwamba hata Glass Kabatini ugongana
Sembuse sisi binaadamu bwana, au siyo Bwana Mbowe.

Mbowe: Ni Kweli Muheshimiwa, lakini kwa Maslahi ya Taifa Letu, Kuna mambo ya Msingi ambayo si busara
Kuyasahu badala yake ni nyema kuendelea kuyakumbuka na kuyakumbusha mpaka pale yatakapopatiwa
Majibu ya uhakika.

Kikwete: Ni kweli, lakini ninachomaanisha ni kwamba kwa sababu tuko hapa kujadili mchakato wa kuandaa katiba
Mpya ni vyema tukasahau yote yaliyotokea apo nyuma kama Maswala ya CHADEMA kutoka nje ya Bunge,
Maswala ya Muswada ama kusomwa mara ya Kwanza ama Mara ya Pili Bungeni na hata Upitishwaji wake Bungeni
Ukizingatia kwamba Bado sijausign kuwa sheria nikitambua kwamba Mazungumzo yetu leo yanaweza kuboresha
zaidi mchakato huu kwa Maslahi ya Taifa.

LISSU: Samahani Mheshimiwa Rais, Kwani wewe binafsi umeuonaje mchakato mzima ulivyokwenda mpaka kufikia
Mswada huo kufikishwa kwako ili usainiwe kuwa sheria.

Kikwete: Tehe tehe tehe, LISSU bwana, tehe tehe tehe, aaaahaaaa. Unajua, haya mambo bwana, ndio maana
mimi nimesema hapa kwamba ni vyema tukasahau yaliyopita ama sivyo mazungumzo yetu yatakuwa mareefu
sana na mwisho wa siku watanzania watatushangaa wote.
Mimi, mimi, mimi dhamira yangu ni kuhakikisha kwamba, Katika mchakato wetu huu, hatufikii kwenye hatua
mbaya kama majirani zetu, sababu haya mambo ukianza kuyawekea maandamano na mihadhara mwisho wake
kwa kweli kabisa hauwezi kuwa mzuri.

Anakunywa Maji kidogo, kisha anaendelea
Pale Kenya pale, wakati wa mchakato wao damu imemwagika pale, sasa mimi siko tayari kuona hili linatokea hapa,
na ndio maana hata kwenye swala la madiwani wa arusha, mimi niliwaelekeza Waziri Mkuu na Katibu wangu Mkama
kuhakikisha Mnakaa, mnazungumza na kulimaliza hili, lakini kinachoendelea pale mi hata sikielewi nikiuliza naambiwa
tatizo ni Lema, vyombo vya habari kwanza vilikuwa vinasema tatizo ni Chitanda, sasa Chitanda simsikii tena
naambiwa tatizo ni Kamanda wa Polisi Zuberi na Mkuu wa Mkoa, mimi sielewi kabisa nini kinaendelea Pale, na hali
hii inachafua kabisa picha ya nchi yetu uko nje.

Anakunywa Maji tena.alafu
Pale Arusha Pale, kile ni kitovu cha Utalii nchini Mwetu, sasa Arusha tukiichezea itatualibia kabisa kabisa, ndio maana
mi nasema swala la Arusha tunatakiwa tukae kama hapa tuzungumze na kulipatia Muafaka. Hii nyumba tunajenga
wote kwa nini tugombee fito Jamani.

Mimi, mimi nasema, wakati tuko Kwenye kikao cha Kamati kuu Dodoma Pale, kuna watu walitaka kukataa nisionane
na CHADEMA, mi nikasema hapana, Lazima nionane nao hawa, kwa sababu hata mimi hili swala la Katiba mpya bado sijalielewa
vizuri.

Kwa hiyo mi nawashukuru sana kwa Moyo wa Uzalendo mliouonyesha, na niko tayari kuonana na nyie na kuzungumza
hata kwenye mambo mengine, sina tatizo hata kidogo na nyie, si unaona bwana, tumezungumza na hakuna mtu
ametoka damu, hii ndio watanzania wanataka kuona.

Mimi kwa kweli niwashukuru sana, na hizi ndio siasa za kizalendo kwelikweli, asanteni sana na karibu tena.

Nice gesture lakini ime-base kwa mbowe na Lissu tu, vipi kuhusu Lema na wengineo? They should have something to present also!
 
Ukiacha utani lakini Jambo la kukutana ni jambo la afya ya siasa zetu. Ikumbukwe kuwa katiba mpya si ilani ya CCM, hivyo wasitudanganye wabunge wa CCM ( akina makinda, Wasira n.k)

Kwamba tusiruhusu mawazo ya watu wachache kuliburuza Bunge, kwani lini wabunge wa CCM walifanya vikao na wapiga kura wao na kukusanya maoni juu ya mswada wa kutunga katiba mpya?

Wenye ilani yao ni muhimu wasikiizwe ili kuona appoach yao ilikuwa ni ipi. Ndio maana sipendi utaratibu wa kuongea mambo ya MSINGI uani kwenye kichaka cha " wazee" wa DSM ambao hata hakuna wa kuuliza swali zaidi ya kusubiri seating allowance.
 
Nimeipenda lakini mbona kikao mwanzo hadi mwisho ni maneno machache hivyo?

Unawajuwa wote waliohudhuria kikao?

Naona pia kama wamezungumzia zaidi kuhusiana na Arusha na Lema kuliko katiba ambapo nilidhani ndo the main agenda?
Jakaya never drive the tabled Agendas, especially when they involve head scratching and making decisions.
He will always find way to talk an issue out and leave everyone stranded.
 
Nice gesture lakini ime-base kwa mbowe na Lissu tu, vipi kuhusu Lema na wengineo? They should have something to present also!
The point is, Jakaya likes to speak, talk, explain, elaborate, analyse, talk talk talk all alone.
ndo maana hata mawaziri huwa wanalala kwenye vikao vyao.

Any way, Moja ya Members ni Profesa Baregu, so, do you guys seat there and wait Jakaya
or any of his kitchen Cabinet member to adress the issues this Professa bring up, objectively?
 
Back
Top Bottom