Mazungumzo kati ya serikali na madaktari yavunjika, tarehe 3 march hiyooooo...

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
Niliwahi kuanzisha mada humu ndani ikisema kwamba mambo si shwari kati ya ma DR na Kamati ya Bwana Pinda! Hii imejidhihirisha leo ambapo kamati hiyo imeshakabidhi mapendekezo yake kwa mh. Pinda lakini:hatari: kwa juhudi kubwa wawakilishi wa ma Dr. wameomba mazungumzo na PM kabla hajatangaza maamuzi yake ili pande mbili zifikie negotiation, cha ajabu kwenye kikao hicho wanaalikwa watu LUKUKI-manesi, wafamasia,watu wa mionzi na watu wote wa kada za afya. Madaktari wamegoma kufanya kikao kikijumuisha hao watu wote kwa sababu zifuatazo;
-Issue ya mgomo ilikuwa ni ya madaktari TU, wafanyakazi wengine hawakugoma, kwa hiyo wanataka kudandia walichoanzisha wenzao
- Kinachojadiliwa ni madai 8 TU waliyopendekeza maDR kwa waziri mkuu, je hao wengine madai yao ni yapi?
-Kada zote zikiingia humo,issue nzima itakuwa neutralized!

Zimebaki siku 2 kufika mwisho wa tarehe aliyoahidi PM kumaliza hili tatizo, kikao kimevunjika, je ni nini kitatokea?

MY TAKE;
-Serikali bado inacheza politics kwenye hii game
-Madaktari watakutana 3/3/2012 kwa maamuzi mazito zaidi ya yale ya mwanzo
-Je sisi wananchi tunasemaje??

MUNGU TUNUSURU!!
 
siasa siasa siasa! Kwenye mambo ya msingi.tusubiri tarehe tatu tujue maazimio ya madaktari.by the way nadhani wamesikia yanayotokea kenya!
 
Kikatiba powers nyingi ziko kwa Raisi, haya yote yatakwisha tukiwa na katiba mpya itakayokidhi Watz wote. Pinda anasubiri boss amwelekeze la kufanya.Kwa mtazamo wangu lakini....
 
Pinda bado hajajifunza! Anadhani madaktari ni kama walimu wanapotishiwa nyau na sura mbaya wanaamini kweli ni nyau! Wao wako makini... Kama anataka mambo yamharibikie tena aendekeze mambo ya taarifa za ki intellejisia wanayyomdanganya nayo TISS. Pinda Pinda! Shauri yako!
 
Wala sio siasa serikali inachofanya bali ni kuanika level ya ujinga na upeo mdogo wa kufikiri wa wahusika,ingekuwa siasa wangelishughulikia vzuri kujipatia sifa na trust ya wananchi,hv kweli unacheza na dokta ni akili kweli?maisha ya wananchi wanachezea danadana halafu 2015 mtadhubutu kuomba kura?
 
Asubuhi ya leo nitakuwa Muhimbili nitayafuatilia haya mambo in details, siwezi kukaa tena kwenye keyboard halafu ndugu zetu wanakufa.
Nadhani sasa JK anataka kuondoka madarakani for good, no excuse this time.
 
Basi madaktari wakikinukisha hiyo tar 3......
Vichwa panzi waongo utawasikia "Rais si aliahidi kulishughulikia suala lao kwenye hotuba ya juzi"...
Utafikiri bado tupo kwenye zama za ahadi.

muda wa kushughulikia umeshapita,kinachohitajika tarehe tatu ni jinsi serikali ilivyotekeleza mahitaji ya madaktari.sidhani kama ahadi ya ''maisha bora kwa kila daktari itakubaliwa''
 
Tusibiri tarehe 3, lakini madaktari wasiyumbishe msimamo wao. Ndugu zetu watakufa, lakini haki yao ikipatikana itawaponya wengi zaidi kuliko kuendelea kufanya kazi katika mazingira nyanyasi. Ikiwa serikali itakengeuka, mgomo uwe kwa kwenda mbele hata kama watafukuzwa kazi. Taaluma yao haipokonywi na mtu yeyote.
Kwa upande wa pili, serikali itumie busara katika suala hili. Isifanye mchezo kama ilivyozoea kufanya na walimu, na wafanyakazi wa idara zingine, ambao serikali ikishapiga chafya tu wanafyata mkia.
Madaktari mmeanza vizuri ingawa ndugu zetu walikufa, lakini msiyumbishwe hadi haki yenu ipatikane. Ili mtuhudumie kwa moyo mkuu. Mungu awabariki na kuwaongoza katika yote.
 
Waheshimiwa Madakatari,
Nawaomba msiyumbe hata kidogo katika msimamo wenu.
Hapomnaposhikilia ni pazuri sana ongezeni pressure minya zaidi.

Serikali yetu inaongozwa na Watanzania Mahabithi, watu katika umbo lwenye Roho na utashi washetani.

Viongozi wa serikali ya CCM, Hasa Bosi wao Jakaya Mrisho Kikwete,niwatu hatari sana na wasiothamini ustawi wa Mtanzania yeyote.
Jakaya Mrisho Kikwete ni mtu anayejari famiia yake na familia za Mfisadi wenzake.

Jakya Mrisho Kikwete amekosa uzalendo kabisa.
Kakosa uzalendo kwa kitendo chake cha kushindwa kuingilia kati na kutatua jambo muhimu linalohusu Tiba jambo ambalo ni Kifo au Uhai / kufa na Kupona kwa Mtanzania yeyote bila kujali Tabaka lake.
Madaktari wakigoma kwa madai ya msingi maana yake Mtanzania yeyote ambaye ana hitilafu katika mfumo wa kuendeleza uhai mwilini mwak, He or she is on his own.
Nijuavyo mimi yeye Kikwete na Elites wenzake hata wakichomwa na mbigili kwenye nyayo, haooooo! Appolo India au St Anne UK Ulaya kutibiwa kwa gharama ya kodi ya walalahoi wote.
Mgomo wa Madakari kwao ni kama kelele za wapiga Madogori ili kupunga pepo.

Jakaya Mrisho Kikwete yuko disconnected na Watanzania na kaficha kichwa mchangani kaa Mbuni not in touch with reality.

Jakaya Mrisho Kikwete ana ulemavu katika mfumo wake wa mishipa ya Fahamu na Ubongo,sehemu inayoshughulikia Aibu imecorrupt kabisa aidha ipo lakini social na inheritance problems zinaizuia kufanya kazi iliyokusudiwa. Na ndiyo mana mara kwa kwa mara Bosi huyu huanguka majukwaani kutokana na mfumo wa fahamu kukosa ushirikano. Yeye hana ushirikiano na watanzania pia mwii wake hauna ushirikiano.

Jakaya Mrisho Kikwete kama Rais wa nchi ameonyesha wazi kwamba uwezo wake, nia yake na mwelekeo wake katika utendaji wa shughuli za kawaida za kila siku za serikali ya CCM na zile zinazohusu ustawi wa raia wake, umefikia kikomo au Tamati. Ni mtu anayesubiri astaafu na kuongeza idadi ya marais wastaafu.

Wakati Madaktari wanagoma nchini Tanzania yeye aliamua kwenda nje ya nchi katika Mkutano wa Forum ya Uchumi ambako kwa udhaifu mkubwa alishindwa kueleza mikakati ya serikali yake kuhusu Elimu na miundo mbinu ya elimu katika kipindi hiki cha utawala wake na miaka ijayopale alipoulizwa swali na Brown waziri mkuu wa zamani wa UK. Badala yake alijibu swali hilo kwa kurefer situation yetu ilivyo kuwa baada ya uhuru 1961 ya barabara 3 za lami,.
Cammon Mr Prez?? Hivi mkikaa kujadili Masuala ya Taaluma ya Elimu na ustawi wake mnaongelea mapaja,viuno vya mademu tuuu na kupiga Katerero tu??

Jakaya Mrisho Kikwete kama Rais wa Tanzania ni Gharasha,mindless,hopeless,zero value na empty heart. ingekuwa supu angekuwa ni supu ya Bamia isiyo tiwa chumvi.

Amekaa kimya muda wotehuu juzi anazuka kutoka ndani ya Comfort Cave lake huku akijipangusa matongo tongo,kikoi kiunoni na kitovu nje na kuongelea suala la Madaktari as if limetokea jana na ndo kwanza kaambiwa.

Wagonjwa kibao walisha kufa, maafa mengi yalisha tokea yeye anakuja kutoa pole baada ya kulipwa Perdiem za siku 40 na ushee.
Hatuna one silver Bullet ya kuondoa mtatizo yote tuliyo nayo. Lakini wakati huo huo ni ujuha kuendelea kufikiri tuna Rais Waziri mkuu na baraza la mwaziri wenye uwezo,dira na nia ya kutatua japo sehemu ndogo ya matatizo yetu.

Kama kazi ya kuwa Rais, Waziri mkuu, waziri,mbunge Inspector wa Polisi na hata balozi wa nchi ni ku Ignore kila Tatizo tulilonalo, kutetea uzembe na ubadhirifu,kuiba ,kusema uongo katika vyombo vya habari na zaidi kutumi jeshi a polisi kulinda waovu wote na maovu yote?????
Viongozi wetu wote ni genge la Mafia katika vyeo mbalimbali.
Viongozi wetu ni maajenti wa Ibilisi wa kuzimu.
Viongozi wetu wapo kuhakikisha hali za watanzania zinazidi kuwa duni kila siku
Viongozi wetu,hasa Jakaya Mrisho Kikwete, ni Mumiani watu wanaoishi kwa kunyonya damu.

Madaktari mmeshika mpini,mgomo wenu ni muhimu sana katika kuleta mabadiriko ya maana katika kitengo cha Tiba pia katika uimarishaji mapambano haya muhimu ya kuondoa utawala mzima wa serikali ya CCM na vibaraka wao ambao ni Makampuni ya vilembwe wa Carl Peters.

Muwe imara na jasiri katika m
 
Pinda asidhani maDr ni UDOMASA ya UDOM aliyoiahidi mambo mengi bila ya kuyatekeleza, kama vile kumwondoa Mllacha
 
Ndugu wana jamii!
Sitaki kuamini kuwa serikali imefanya kosa katika kuwaita kada nyingine, tatizo ni tafsiri ya neno daktari. Kiserikali, kutokana na matatizo ya huko nyuma, neno daktari linamaana ya kada zote za afya kutokana na mfumo udaktari uliopo wizara ya afya, ambapo hata kada zingine kama za nurse, famasia ati kurugenzi zinaongozwa na daktari. Sasa, serikali inalitambua hilo ndio maana, haiwezi kuboresha maslahi ya madaktari bila ya kuziboresha kada zingine.HAIWEZEKANI. Nao pia wana madai yao, ndio maana hata wauguzi wanadai kurugenzi yao, famasi kadhalika, sasa mnataka madaktari ndio wawasemee???? huko nyuma wakati wa Raisi mwinyi, mgomo ulitokea, na baada ya serkali kukubali matakwa ya madaktari, maslahi yaliboreshwa kwa madaktari tuu, hii ilileta shida sana pae manesi walipogoma. Na kiukweli, kada zote za afya zinafanya kazi kama timu ya pamoja na hakuna aliye juu ya mwingine, tatizo ni saikolojia ya madaktari wa tanzania kujiona wako juu kuliko taaluma zingine, nenda ulaya, mgonjwa hawezi kupatiwa dawa kama haijapitiwa na mfamasia, n.k , hivyo wasijione ni special sana, kada zote zinaumuhimu, leo manesi wakisema hatufanyi kazi, madaktari mnaweza kufanya kazi peke yenu???? mlipogoma, vifo si vingi sana kama manesi wakigoma.
Acheni ubinafsi, ndio sababu hata manesi wataka idara yao, na si kila kitu paka mganga mkuu hata kama kinahusu taaluma nyingine.
 
mi sikuamini na sitaamini kama kilichoahidiwa na serikali kitatekelezwa...watz hatujaanza kubaguana leo,,,viongozi wanatibiwa india,,wenye mishahara mikali mnatibiwa aghakani, regency,,,,leo sie walalahoi tuliozoea shida mntuingiza katika mitafaruku ya kuua mhimbili yetu ponepone pekee kwetu..kweli jamani???????????????????
 
Ikulu ni Mahali patakatifu, Ikulu ni Mzigo. Ukiona mtu anakimbilia Ikulu ni wa kumwogopa kama Ukoma. Jamaa alikimbilia akidhani ni sehemu ya kwenda kucheza Tokomile na Kufukua mashimo mengi.
 
Basi madaktari wakikinukisha hiyo tar 3......
Vichwa panzi waongo utawasikia "Rais si aliahidi kulishughulikia suala lao kwenye hotuba ya juzi"...
Utafikiri bado tupo kwenye zama za ahadi.

Mkuu ile haikuwa hotuba ilikuwa ni TV talk show...
 
Uamuzi huu unaweza ukawa na madhara kwa umoja wa hawa watu...ni kweli kuwa kada nyingine hazikugoma ila walikuwa wanawasapoti wenzao.Nadhani madaktari watumie busara kwa hili,inaweza ikawa ni mwanya wa serikali kuwabana kwa udhaifu huu...Vp Dr Ulimboka yupo?
 
Ndugu wana jamii!
Sitaki kuamini kuwa serikali imefanya kosa katika kuwaita kada nyingine, tatizo ni tafsiri ya neno daktari. Kiserikali, kutokana na matatizo ya huko nyuma, neno daktari linamaana ya kada zote za afya kutokana na mfumo udaktari uliopo wizara ya afya, ambapo hata kada zingine kama za nurse, famasia ati kurugenzi zinaongozwa na daktari. Sasa, serikali inalitambua hilo ndio maana, haiwezi kuboresha maslahi ya madaktari bila ya kuziboresha kada zingine.HAIWEZEKANI. Nao pia wana madai yao, ndio maana hata wauguzi wanadai kurugenzi yao, famasi kadhalika, sasa mnataka madaktari ndio wawasemee???? huko nyuma wakati wa Raisi mwinyi, mgomo ulitokea, na baada ya serkali kukubali matakwa ya madaktari, maslahi yaliboreshwa kwa madaktari tuu, hii ilileta shida sana pae manesi walipogoma. Na kiukweli, kada zote za afya zinafanya kazi kama timu ya pamoja na hakuna aliye juu ya mwingine, tatizo ni saikolojia ya madaktari wa tanzania kujiona wako juu kuliko taaluma zingine, nenda ulaya, mgonjwa hawezi kupatiwa dawa kama haijapitiwa na mfamasia, n.k , hivyo wasijione ni special sana, kada zote zinaumuhimu, leo manesi wakisema hatufanyi kazi, madaktari mnaweza kufanya kazi peke yenu???? mlipogoma, vifo si vingi sana kama manesi wakigoma.
Acheni ubinafsi, ndio sababu hata manesi wataka idara yao, na si kila kitu paka mganga mkuu hata kama kinahusu taaluma nyingine.

hii propaganda yako irudishe hukohuko TBC
 
Back
Top Bottom