mazoezi ya ndege za kijeshi dar es salaam leo ina maana gani?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
hii ni sawa na kututisha.kwanini wasifanyie mapolini au baharini?hatutishwi na ndege.maandamano yapo palepale.
 
hivyo vindege hata manati yaweza kuvipopoa ..... tena wananchi wawe makini .... zaweza kulipuka zenyewe .... pale msata mwaka jana ndege vita imedondoka yenyewe
 
Hivyo vitisho tumesha zoea, bado mazoezi ya vifaru kwani mazoezi ya mabomu wamesha maliza, lakini atishiwi mtu nyani apa, vita mbele mpaka kieleweke. CCM mkifika 2015 kweli mnabahati
 
Aaaaaaah,watanzania jamani!

Kwani siku zote mazoezi ya wanajeshi yana maanisha nini?

Ina maana leo ndo mara ya kwanza kufanyia dar?

Au wewe ndo mlengwa mwenyewe hadi unaogopa?

Kama unapanga uhaini uta kamatwa tu na bora ujisalimishe sio kukaa na mipanic yako hapa
 
Wala Kikwete asitutishe na nyoka aliyekufa; midege yote ya kijeshi, vyombo vyote vya dola ni mali zetu sisi wenyewe ndio tunaozigharamia siku zote na wala hatukuviweka hapo kuwalinda mafisadi kwa namna yoyote ile!!!
 
Hawawezi kujitofautisha na watoto wadogo? Au wanadhani watz ndio makinda wa jana
 
Zisije zikadondokea watu tukaingia kwenye maafa mengine, they are flipping bungers.
 
Anaiga ya Gaddafi... anaweza tumia styre ie ile ya kubombardment kwa kutumia airfighter
 
Vikipigwa vibomu vya machozi mnakimbia ovyo ovyo - mh. Pinda leo midege si mchezo
 
wasije wakayandondosha midege yenyewe mara ya mwisho kuwashwa ni miaka ya 80 wakati wa vita ya Amini, haiaminiki, wakafanyie huko anga ya baharini mbali na si kwenye anga ya makazi ya watu, tafadhali.
Watu hatuna imani kabisa, juzi juzi tu wamefanya uzembe mabomu yamelipuka hatujasahau hata kidogo eti mazoezi ya ndege za kijeshi kwenye anga letu.

Wao ndiyo wanafanya sisi tusiwaamini.
 
yasije kudondokea Raia wasiyo na atia, kwani ayachelewi kuzimikia juu
 
kitendo hiki kwa sasa kinatutisha watanzania tulio wengi kwani hatuiamini tena serikali na vifaa vyake vya kijeshi. kama mkidondosha ndege au kugonga jengo this time no body will understand you kama gongo na mbagala things will change completely. kwanini msifanyie baharini bwana?????????
 
wanatest kama bado zinaweza kuruka

sasa sijui kwa nini wasiende maporini
 
Seriously, I hope hapatatokea matukio yanayosababishwa na - makosa ya kibinadamu.....
 
Back
Top Bottom