Mazoezi ya JWTZ yashtua Bandarini!

Labda zilikuwa njiani kuelekea Congo DRC na nchi nyingine katika ukanda wa maziwa makuu mzee wangu
 
Makubwa hayo. haya tunasubiri habari kamili.

Yaa Allah inusuru TZ na mabalaa hayo
 
Hii habari imekanushwa na vyanzo vya uhakika hivi punde- ni wanamaji wa wa jeshi la tanzania walikuwa kwenye mazoezi ya kushtukiza.

Vyaeni vyetu vyenu, indeleeni na shughuli kama kawaida!
 
Hayo mazoezi ya wanamaji yanayoleta impact kubwa namna hii yameanza lini? Watu wamesimamisha kazi zaidi ya saa moja. Wametolewa maofisini kwa ving'ora. Taharuki ilikuwa kubwa. Watu wameambiwa wataalam wa JWTZ wamefanikiwa kuyategua kwa hiyo warudi kazini! Nani anamdanganya mwenzie hapa? Tusubiri tusikie zaidi.
 
Bajati yao haijapita huko Bungeni na wanataka kuonyesha kwamba wako imara na ulinzi lazima kuwazuga wabunge nadhani ili wakubalike ama ?
 
Hao waliokuwamo ati wamekimbia wamekimbilia wapi baharini? na kuna juhudi zozote za makusudi zilizofanywa kuwafuatilia ili wakamatwe? watusaidie kueleza ilikotoka na yalikuwa yanapelekwa wapi!
 
Mimi niko Dar es Salaam wajameni, ngoja nianze kusali maana hajui yakilipuka destination itakuwa wapi?

Du tuna ulinzi makini kweli kwenye taifa letu.
 
Ukweli ni kwamba: Kuna meli imeleta silaha za majirani zetu wa Uganda. Silaha hizo ni pamoja na Vifaru, magari ya Deraya na Mabomu. Vifaru na magari vimesha pakuliwa toka melini na tayari viko kweneye mabehewa tayari kwa safari.

Sasa ilikuwa zamu ya kushusha mabomu, katika hilo zoezi wataalamu wa melini wakabaini kuwa baathi yalikuwa yamekaa vibaya hivyo yangeweza kulipuka wakati wowte.

Hapo hatua za tharura zikachukuliwa, kazi zote zikasimama, watu wote wakakusanywa kwenye emergency assembly point, kisha wataalama wa kutegua mabomu wa TPDF wakaitwa nao wakaingia kwa kasi na boat yao na wakafanikiwa kuweka mambo sawa. Kazi za bandari zikarejea katika hali yake ya kawaida.

Sasa unajua suala la kusafirisha silaha ni jambo nyeti, na mara nyingi general public katika hili huwa hawaambiwi ukweli ndio maana katika hili mtasikia story nyingi.
 
Bajati yao haijapita huko Bungeni na wanataka kuonyesha kwamba wako imara na ulinzi lazima kuwazuga wabunge nadhani ili wakubalike ama ?

Mkuu, wani bajeti yao inapitishwa na bunge? si wanapanga tu....unajua tena mambo ya usalama wa taifa, eeem au ni ile kuwa hawakaguliwi na CAG? sijawahi sikia mbunge akatoa shilingi kwenye bajeti ya JW?
 
Ukweli ni kwamba: Kuna meli imeleta silaha za majirani zetu wa Uganda. Silaha hizo ni pamoja na Vifaru, magari ya Deraya na Mabomu. Vifaru na magari vimesha pakuliwa toka melini na tayari viko kweneye mabehewa tayari kwa safari.

Sasa ilikuwa zamu ya kushusha mabomu, katika hilo zoezi wataalamu wa melini wakabaini kuwa baathi yalikuwa yamekaa vibaya hivyo yangeweza kulipuka wakati wowte.

Hapo hatua za tharura zikachukuliwa, kazi zote zikasimama, watu wote wakakusanywa kwenye emergency assembly point, kisha wataalama wa kutegua mabomu wa TPDF wakaitwa nao wakaingia kwa kasi na boat yao na wakafanikiwa kuweka mambo sawa. Kazi za bandari zikarejea katika hali yake ya kawaida.

Sasa unajua suala la kusafirisha silaha ni jambo nyeti, na mara nyingi general public katika hili huwa hawaambiwi ukweli ndio maana katika hili mtasikia story nyingi.

Story yako inaelekea in ukweli. Tunashukuru kwa taarifa hiyo muhimu!!
 
.... test kwamba digital media [JF na Michuzi] watakajua habari hizi mapema kabla ya [IPP na New Habari] au test gani mkuu?

Hii habari imekanushwa na vyanzo vya uhakika hivi punde- ni wanamaji wa wa jeshi la tanzania walikuwa kwenye mazoezi ya kushtukiza.

Vyaeni vyetu vyenu, indeleeni na shughuli kama kawaida!
Laibon ameeleza vizuri. Majaribio au mazoezi ya kushtukiza kufanywa pia sehemu kama mahotelini, ku-simulate tukio, mfano tukio la moto. Hakuna anayetahadharishwa, hata wageni waliolala hoteli hugundua kilichotokea baadae zoezi likiisha.

Hii husaidia watu wa fire kwa mfano, kuwa alert and to respond quickly.
Nakumbuka kuna habari ya wafanyakazi wa zimamoto KIA ambao walijaribiwa na kukutwa hawafai, maana kukimbia tu hawawezi.
 
Hayo mazoezi ya wanamaji yanayoleta impact kubwa namna hii yameanza lini? Watu wamesimamisha kazi zaidi ya saa moja. Wametolewa maofisini kwa ving'ora. Taharuki ilikuwa kubwa. Watu wameambiwa wataalam wa JWTZ wamefanikiwa kuyategua kwa hiyo warudi kazini! Nani anamdanganya mwenzie hapa? Tusubiri tusikie zaidi.
Wanaweza kwenda Sudan na Congo kwa ajili ya mazoezi lakini sio bandarini na sehemu ambazo watu wanahangaika kila siku na hususani bandari yetu
 
kwa mujibu wa ulamaa, Tanzania kwa mara nyingine tena tumekuwa kichochoro cha kusafirisha silaha, na kama ni kweli za uganda, hawa jamaa wanajiandaa na vita ya nani au Kenya (MIGINGO Island)?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom