Mazoezi ya JWTZ yashtua Bandarini!

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Kuna taarifa nimepata sasa hivi toka kwa mdau mmoja yupo Bandarini Dar es Salaam anadai kuna shehena ya mabomu imenaswa bandarini hapo.

Kama kuna waandishi wa habari (Clouds FM wamesharipoti nasikia) basi nawashauri wafuatilie kwa karibu
 
Last edited by a moderator:
siyo shehena ni boat inaenda kasi kuelekea ktk Oil Terminal ya kurasini,imeingia bandarini bila idhini
 
Wanajf, kuna habari kuwa meli moja iliyosheheni mabomu imekamatwa huko bandarini Dar. Hii ni kwa mujibu wa Redio Clouds ambayo imesema kwamba wanafuatilia na watatoa taarifa zaidi. Mwenye taarifa zaidi tafadhali atujuze.
 
siyo shehena ni boat inaenda kasi kuelekea ktk Oil Terminal ya kurasini,imeingia bandarini bila idhini
Poa mkuu, unaweza kutufahamisha zaidi ilikuwa na nini mpaka ikashtukiwa?
 
Ndugu zangu angalieni tusije tukashikishana uchawi hapa. Chondechonde na habari ambazo not proved. Mnatutisha tulionje ya bongo kwa usalama wa nchi na ndugu zetu. Tunaomba uhakika hapa janvini plz
 
Ufafanuzi umetolewa kwamba lilikuwa ni zoezi la kawaida la kuhakikisha usalama wa bandari. Vikosi na mamlaka nzima ya bandari walikuwa na taarifa ya zoezi hilo kufanyika leo. Zoezi limekwisha na watu wameambiwa waendelee na shughuli zao kama kawaida. Hii nayo ni kwa mujibu wa Redio Clouds kupitia afisa wa mamlaka ya Bandari aliyeongea live na Bonge(mtangazaji wa kituo hicho cha redio)
 
Nasikia ni jaribio/testing.
Kama ni testing basi wamejua kuwa media zitafanya coverage ya haraka sana! Kuna media nyingine tofauti na Clouds & JF walioweza kutangaza tukio hilo? Nini reaction ya security ya bandari yetu?
 
Tuko makini sana na mazoezi ila kwenye live envornment dooo ngoma huwa zinapita du daily hapo hapo.....
 
yani mi nasemaje nilizozipata hivi punde kupitia redio clous ni kwamba eti meli hiyo ilikuwa mazoezini, lakini isije ikawa kama ile ya mbagala mazoezi ukashanga watu wanapoteza maisha hivi hivi hawa watu tusiwaamini moja kwa moja mwenzenu nilijua mambo yale ya uvuvi yanarivenji jama waliopo karibu fuatilieni tujue mwisho wa hayo mazoezi ni nini.
 
Nimekutana na habari hizi kwa michuzi nimeona nishare hapa ili kama kuna mwenye habari zaidi na atuhabarishe maana hii inahusiana na usalama wa nchi hii

BREKING NYUUZZZZZ
HABARI ZIMEINGIA SASA HIVI ZINASEMA KWAMBA KUNA MELI IMEKAMATWA BANDARINI DAR AMBAYO INASEMEKANA IMEBEBA MABOMU NA WATU WOTE WA HUMO MELINI WAMEKIMBIA NA KWAMBA HAKUNA SHUGHULI INAFANYIKA HAPO BANDARINI MPAKA SASA.

WAFANYAKAZI WA BANDARI IMEWALAZIMU KUAMBIWA WATOKE NJE YA BANDARI BAADA YA BOTI YENYE SPIDI KALI KUINGIA BANDARINI BILA IDHINI, KWA MUJIBU WA HABARI ZISIZOTHIBITISHWA BADO.


GLOBU YA JAMII INAFUATILIA KUTHIBITISHA HABARI HII NA ITAWAPASHA UKWELI WA MAMBO BAADAYE KIDOOOOOOOGO....
 
Habari ndiyo hiyo, tuliambiwa kuna meli ilikuwa na mabomu imefunga berth namba 4. Tukatolewa mkuku maofisini. Badaye tukaambiwa wataalam wa kutegua mabomu toka JWTZ wameshayategua. Tumerudi kazini tunakula mizigo kama kawaida sasa! Bongo tambarare
 
Habari ndiyo hiyo. Watu walitolewa maofisini. Wakaambiwa kuna meli imefunga berth namba 4 ikiwa na shehena ya mabomu. Then baada ya kama lisaa limoja na ushehe tukaambiwa wataalam wa kutegua mabomu toka JWTZ wameshafanya vitu vyao, na mabomu wameshayategua. Watu wamesharudi makazini wanapiga bunda. Bongo tambarare, bongo nchi ya amani!!
 
Hizi habari wanaweza kujua ni wao mwenyewe na haiwezekani mamlaka zinazohusika zijulie hapo bandarini?? Hivyo ulinzi wa Nchi yetu upo wapi??
 
Back
Top Bottom