Afrika Furaha
JF-Expert Member
- Dec 16, 2010
- 329
- 9
Wana JF, kipindi hiki cha sikukuu watu wanatembeleana sana majumbani. Ktk nyingi nimejionea kitu kimoja kikubwa. Utakuta nyumba ina mlango wa mbele, ambao kimsingi ukiingia hapo utaanza kuingia sitting room. Pia kuna mlango wa pili ambao ukiingia unaanza kuona jikoni. Sasa kuna nyumba ambazo hazitumii kabisa mlango wa mbele, hata waje wageni wa wapi, na hata ukiingia ndani unaweza kukuta wameweka kochi mlangoni kwa ndani. Badala yake watu huingia ndani kwa kupitia uani au jikoni . . . sasa sijaelewa kwa nini kuna mazoea haya??