Maziwa, matiti au nyonyo?

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
WanaJF,
Naomba msaada katika matumizi sanifu ya maneno haya, haswa pale inapotokea nimeulizwa na mtu asiyejua Kiswahili. Mfano mtu akiniuliza katika Kiingereza tafsiri ya:

'Milk' in Swahili - nitasema 'maziwa'
'Breasts' in Swahili - nitasema 'matiti' au 'maziwa'

Kwa sababu neno milk linatafsiri kamili, yaani maziwa; basi naomba mnisaidie kujua matumizi fasaha ya neno la Kiswahili linalo maanisha 'breasts'.

Akhsanteni.

SteveD.
 
Milk ni maziwa ila kuna wengine wanatumia creme ikimaanisha maziwa pia.

Breasts ni matiti. Mfano mwanamke ana matiti halafu hayo matiti yana chuchu ambazo ndio zinatoa maziwa maranyingi wakati amejifungua mtoto.

Tusikie zaidi kutoka kwa wanaJF wengine.

Bel.
 
SteveD,

Try http://africanlanguages.com/swahili/; for "matiti or titi" I got breasts or nipples while for "maziwa I got milk. Using "maziwa" to mean "matiti" is a kind of street language or a word used by people from a specific area. Language experts have the right terminologies for such words.
 
Last edited:
Milk ni maziwa ila kuna wengine wanatumia creme ikimaanisha maziwa pia.

Breasts ni matiti. Mfano mwanamke ana matiti halafu hayo matiti yana chuchu ambazo ndio zinatoa maziwa maranyingi wakati amejifungua mtoto.

Tusikie zaidi kutoka kwa wanaJF wengine.

Bel.

Upo sahihi kabisa mkuu. Wapo watu wanafanya makosa (wakati mwingine hata mimi mwenyewe) kwa kuyaita matiti kuwa ni maziwa.
 
Maziwa ni kimiminika(liqiud state)Matiti ni maungo (physical).Kiswahili nacho ni kirefu pia.Huwezi kuita matiti maziwa ila lugha hii ya kuita maziwa inatumiwa kwa watoto wadogo ili kuweka hali ya ustaarabu wa kutaja viungo vilivyosetiriwa kwa mwanadamu.Kiswahili hakina neno maziwa kwa mana ya matiti.Mathalani kina mama utawasikia wakisema maziwa yangu yanauma,Ukweli ni matiti yakiwa na maziwa kama hajanyonyesha kwa muda ndo yanauma.Lakini hata MEWATA katika matangazo yao mara nyingi madaktari wao kwa kutokujua au kwa mazoea wamekuwa wakitumia neno hilo kumaanisha matiti.Mkuu wewe huwezi kuwaambia wenzako maziwa yako yanauma!!!!Tutakutizama kwa jicho la mshangao!!
 
Nitaanza na neno Matiti, tumelitohoa katika kiingereza cha kimarekani "Tits" wakimaanisha Breasts (Waingereza). Hivyo jina sahihi ni Matiti ama kama ni moja Titi. Maziwa ni kitu kilichotoka katika matiti yani yale majimaji, ama unga uliotengenezwa kuwa maziwa. Hivyo maziwa yanaweza kuwa katika umbo la maji (kimiminika) ama yabisi (ngumu).
 
WanaJF,
Naomba msaada katika matumizi sanifu ya maneno haya, haswa pale inapotokea nimeulizwa na mtu asiyejua Kiswahili. Mfano mtu akiniuliza katika Kiingereza tafsiri ya:

'Milk' in Swahili - nitasema 'maziwa'
'Breasts' in Swahili - nitasema 'matiti' au 'maziwa'

Kwa sababu neno milk linatafsiri kamili, yaani maziwa; basi naomba mnisaidie kujua matumizi fasaha ya neno la Kiswahili linalo maanisha 'breasts'.

Akhsanteni.

SteveD.

Ndugu steve inasaidia kuona kuna baadhi yetu tunaijali lugha yetu kwa kuienzi kwa namna moja au nyingine na wewe kwa hili umechangia kufanya hivyo pia kuna neno moja ambalo sitoweza litamka pia linatumiwa vibaya hapa TZ kwa mfano utasikia mtu anasema muangalie ana (MK )mkubwa lakini basi kile kinachooneka sio (MK )yale yanaitwa (MA) ni ufujaji wa lugha kwa makusudi
 
Kiswahili kama lugha nyinginezo duniani, kina neno moja moja lenye maana nyingi na kuna maneno mengi yenye maana moja. Yote haya yana ufununu wa maana halisi hususan yanapotumiwa katika sentenso, kimaandishi au kimazungumzo. Wanaowasiliana huelewana kirahisi tu.

1. Maziwa ya yule dada ni makubwa sana. Mtu akisema au akiandika hivyo, inaeleweka kwa uwazi na wepesi kuwa kinachozungumzwa hapo ni sehemu ya mwili wa yule dada.

2. Maziwa ya yule dada yamejaa sana na yanatoa maziwa mengi. Ikisemwa hivyo, inaeleweka kwa uwazi na wepesi kuwa neno "maziwa" la mwanzo ni sehemu ya mwili wa yule dada na neno "maziwa" la pili ni kile kinachotoka ndani ya ile sehemu ya mwili wa yule dada, nacho ni "maziwa ya kunyonywa au kunyonyeshwa mtoto."

Maneno yote mawili "maziwa" na "matiti" ni sahihi katika Kiswahili sanifu. Neno "maziwa" hutumika sana mrima na neno "matiti" katika sehemu za mwambao.

Kuna neno tuliloliazima kutoka kwa Wareno. Neno "meza" ambalo lina maana ya chombo tukitumiacho wakati wa kula au kuandika. Yaani kiti na "meza." Lakini, tunalo neno "meza" lenye maana ya kuingiza chakula ndani. Yaani, kukipitisha ndani zaidi ya kooni.

Kwa hiyo neno ni moja lakini lina maana zaidi ya moja, kama vile kwa mfano "nyanya" tunda linalotumika katika mapishi na "nyanya" mzaa baba au mama, ambaye wa mrima humwita "bibi."
 
WanaJF,
Naomba msaada katika matumizi sanifu ya maneno haya, haswa pale inapotokea nimeulizwa na mtu asiyejua Kiswahili. Mfano mtu akiniuliza katika Kiingereza tafsiri ya:

'Milk' in Swahili - nitasema 'maziwa'
'Breasts' in Swahili - nitasema 'matiti' au 'maziwa'

Kwa sababu neno milk linatafsiri kamili, yaani maziwa; basi naomba mnisaidie kujua matumizi fasaha ya neno la Kiswahili linalo maanisha 'breasts'.

Akhsanteni.

SteveD.

Kiswahili ni lugha iliyorithi kwa asilimia kubwa, tabia na miundo ya lugha ya kiarabu. Mara nyingi tunapozungumza kiswahili huwa tunatumiaaina ya misemo ambayo bila ya kukusudia au kwa kukusudia huwa inaficha au kupunguza makali ya kile tunacho kimaanisha, na hii ni katika kuonyesha heshima kwa mzungumzaji na msikilizaji.

Nikirejea kwenye maneno yalio kusudiwa na mtoa mada "Matiti au Maziwa" Kilugha maneno haya yana maana tofauti. Lakini ki Istilahi huwa neno moja utumiwa kuficha ukali wa neno lingine, hapa tunakuwa tumetumia tamathali za usemi zinazofanya neno liwakilishalo kitu kingine (Tashabiha).

Mara nyingi hali hii ya kutumia tashbiha inapelekea wale wasiokuwa mahili au wanagenzi wa lugha ya kiswahili hususan watoto kupata tabu kutambua kilicho kusudiwa, vile vile husaidia kuonyesha uungwana na heshima kama nilivyodokeza hapo juu.

Kuna maneno ukiyatamka kama yalivyo, yaani kuyatamka kavu kavu, uonekana ni matusi na waliokuwepo watakuona ni mtovu wa adamu.
Tunaweza kutamka neno kama lilivyo pale tu tunapokuwa tumekaa watu wa rika moja. Utashangaza na kuonekana wa ajabu maneno kama haya yafuatayo ukayatamka kama yalivyo mbele ya watoto au watu waliokuzidi umri.
Mfano:
Neno kama Ngono au kufanya mapenzi litamke kwa asili yake, Uume au uke. Nakumbuka sisi tulikuwa tunafundishwa kutamka chini kwa babu (dudu) au kwa bibi. Vile vile tunatumia neno " Haja kubwa na ndogo" lakini tunajuwa tuna maanisha nini.

Vilema tunawaita kwa jina la walemavu wa viungo n.k

Kwa uoni wangu nadhani si vibaya mtumiaji akatumia neno maziwa akimaanisha Matiti, hii inategemea na maali alipo. Ila huwezi kutumia neno matiti ukimaanisha maziwa. (My Milk is standing)

Naomba kuwakilisha

XP
 
Mkuu X-P kiusahihi ni 'naomba kuwasilisha' na si 'naomba kuwakilisha' kama ulivyondika hapo mwisho wa mchango wako...Heshima mbele mkuu..Be blessed
 
Akhsanteni wote kwa ufafanuzi murua kabisa wa tafsiri na matumizi ya maneno niliyouliza (ulizia??).

X-P, je matumizi ya neno "nyonyo" au "manyonyo" yaweza kusemeka ni moja ya tashbiha (-euphemistics- kwa jinsi nilivyoelewa tafsiri ya tashabiha/tashbiha kwa maelezo yako juu, sina uhakika kama neno tamathali nalo lina maanisha 'uephemism') za neno matiti au ni mojawapo ya nomino wakilishi tu?

SteveD.
 
Mkuu X-P kiusahihi ni 'naomba kuwasilisha' na si 'naomba kuwakilisha' kama ulivyondika hapo mwisho wa mchango wako...Heshima mbele mkuu..Be blessed

Ndugu yangu Balantanda, nashukuru kwa kunisahihisha. Na vile vile heshima ulionipa ya ukuu mimi sinayo, mimi ni mjoli tu katika huu ulimwengu.

Akhsanteni wote kwa ufafanuzi murua kabisa wa tafsiri na matumizi ya maneno niliyouliza (ulizia??).

X-P, je matumizi ya neno "nyonyo" au "manyonyo" yaweza kusemeka ni moja ya tashbiha (-euphemistics- kwa jinsi nilivyoelewa tafsiri ya tashabiha/tashbiha kwa maelezo yako juu, sina uhakika kama neno tamathali nalo lina maanisha 'uephemism') za neno matiti au ni mojawapo ya nomino wakilishi tu?

SteveD.

Neno "nyonyo" au "manyonyo" Nadhadhani yanatokana na Neno NYONYA. Likimaanisha kitendo cha kuingiza kitu mdomoni na kuvuta kwa ndani kwa madhumuni ya kupata kile kilichokuwa ndani ya hicho ulichokitia mdomoni. (Draw into the mouth by creating a practical vacuum in the mouth).

Bado tunarudia pale pale kutumia hizi tamathali za usemi, hii ni lugha ya kitoto (An informal term...), ninaposema lugha ya kitoto nina maanisha kuwa ...tunawarahisishia watoto kuelewa tunacho kikusudia. Au tumeiga matamshi ya kitoto...

Mama anaye nyonyesha akimwambia mtoto wake "...nyonyoo" ni rahisi kwa mtoto kuelewa kuwa anatakiwa anyonye. Na anapoambiwa "...nyonyo" anatakiwa aelewe kuwa hapo pamekusudiwa Maziwa/Matiti ya mama yalio kifuani au kwenye chupa.

Mfano mwingine kwa kupanuwa wigo ni matumizi ya neno kojoa, kwenda haja ndogo = jojoa ... kubwa=Nnya.

Kwenye lugha ya Kiingereza pia wanamatumizi ya maneno ya kitoto kama vile Dad or Daddy = Father, Mum or Mummy = Mother.

Nawasilisha kama mdau alivyoshauri

XP
 
Kiswahili kimeazima maneno ya kiarabu, kihindi,kireno, kiingereza. Mengi katika maneno yaliyoazimwa ni kutoka lugha ya kiarabu.

Lugha yoyote inayokua, huazima maneno kutoka kwa wengine. Kama vile kiingereza kilivyoazima maneno ya Kifaransa, Kijerumani, Kilatini na kadhalika.

Kiswahili ni kibantu kama kilivyokuwa kinatumiwa na watu wa makabila tofauti, walipokuwa wanawasiliana kibiashara na hata kuoana kabla ya wageni kuingia katika nchi yetu.
 
WanaJF,
Naomba msaada katika matumizi sanifu ya maneno haya, haswa pale inapotokea nimeulizwa na mtu asiyejua Kiswahili. Mfano mtu akiniuliza katika Kiingereza tafsiri ya:

'Milk' in Swahili - nitasema 'maziwa'
'Breasts' in Swahili - nitasema 'matiti' au 'maziwa'

Kwa sababu neno milk linatafsiri kamili, yaani maziwa; basi naomba mnisaidie kujua matumizi fasaha ya neno la Kiswahili linalo maanisha 'breasts'.

Akhsanteni.

SteveD.

Kiswahili kinakuwa kwa hiyo yote hayo ukitumia ni sawa mradi ueleweke.
 
English recognize the presence of breasts on men's chests,sasa kiswahili kinasemaje,vile vijinundu vilivyopo vifuani mwa mwanaume vinaitwaje,matiti,chuchu,manyonyo au maziwa?Naomba kuelimishwa
 
Kimsingi "ziwa" ni lile bwawa (yaani mahali pa maji); kutoka hapa maana imeendelea kutaja hata "bwawa" kwa mwanamke au sehemu penye "maji" yake ya kumlisha mtoto; mwishowe yale "majimaji" yanatajwa kwa jina la mahali yanapotoka kuwa "maziwa".

Nikichungulia kamusi zangu za kale tayari kuna maana ya "ziwa/maziwa" kwa matiti ya mwanamke; titi peke yake si lile la mwanamke tu hata mwanaume ana matiti mawili (kama "nipples"); kwa hiyo naona maziwa ni sanifu tu.
 
Kwanza nadhani ningependa kukushukuru kwa kuuliza Swahili hili ambalo linaonekena kuwa rahisi lakini kindani ni swali rahisi. Jina sahihi la Kiswahili ni MATITI, Maziwa ni jina la heshima ambalo kwa Kiswahili tunaliita Jina la Kitasifida au Tasfida. Kiingereza ni Eupheminism. Endelea kutupa maswali tujaribu kuimarishi Lugha niipendayo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom