Maziwa fresh

peter tumaini

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
573
94
HABARI WAKUU,

Nimepata sehemu ambayo naweza kupata maziwa fresh ya ng'ombe wa kienyeji ila mkoani.wadau challenge niliyo nayo kwa sasa ni jinsi ya kusafirisha yafike kwa customer yakiwa fresh na pia kumpata mteja wa kuwa namsambazia .
hivyo wadau naleta kwenu mwenye connection na mnunuzi wa maziwa fresh kama lita 5,000 kwa wiki kwa kuanzia na mwenye link au aliye na container za kusafirishia tuwasiliane hapa jamvini ikiwezekana twaweza fanya joint venture.

Nawasilisha.
 
wacha masihara wewe hivi unajua ili kupata lita 5000 itakubidi kukamua ng'ombe wa kienyeji wangapi?
 
Mkuu uko Kasulu nini? Maana huko mpaka tunamwaga maziwa kwa kukosa soko!
 
wacha masihara wewe hivi unajua ili kupata lita 5000 itakubidi kukamua ng'ombe wa kienyeji wangapi?

NARUBONGO

Hivi ng'ombe 600 wa maziwa kwa wiki hawatoi hizo lita 5,000 au wewe unafikiriaje?kama una soko lete tufanye kazi
 
NARUBONGO

Hivi ng'ombe 600 wa maziwa kwa wiki hawatoi hizo lita 5,000 au wewe unafikiriaje?kama una soko lete tufanye kazi

ok, mwanzoni ulisema ng'ombe wa kienyeji. Nilikuwa naona musoma dairy milk shops pale mwanza sijui kama bado wanaendelea, wacheck kwanza hao itakusaidia kuuza maziwa yako karibu na hapo shinyanga c'se nilisikia huwa wananunua maziwa kutoka kwa wafugaji kama anavyofanya asas
bei ya maziwa hapo shinyanga kwa lita ni sh ngapi? una usafiri binafsi wa kusafirisha maziwa? kama haunausafiri binafsi bei ya kukodi usafiri ni sh ngapi? umeshaangalia gharama za uhifadhi kwa wiki 1? (note: vifaa vya ukamuaji na usindikaji ni free of duty, itakusaidia)
Jaribu kufikiria kwa umakini mkubwa hayo juu

challenge kubwa utakayoipata ni quality ya maziwa c'se watu wa vijijini huwa wanachanganya sana maziwa na maji, hii inaweza ikakuharibia
 
wacha masihara wewe hivi unajua ili kupata lita 5000 itakubidi kukamua ng'ombe wa kienyeji wangapi?

hapa sio chini ya ng'ombe 7500. kwa maana ya wastani wa lita 1.5
ngo'ombe wa kienyegi kufugia maziwa ni utumwa.
 
hapa sio chini ya ng'ombe 7500. kwa maana ya wastani wa lita 1.5
ngo'ombe wa kienyegi kufugia maziwa ni utumwa.

mkuu kuwa serious basi NG,OMBE 7500 kwa lita 1.5 ni sawa na lita 11,250 kwa siku. mie naongolea kwa wiki
utakuta ng'ombe anayeweza toa lita 5 kwa wiki itatakiwa ng'ombe 1000 tu kupata hizo lita 5000 na huku kuna watu wana Ng'ombe zaidi ya 2000 mfugaji mmoja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom