samora10
JF-Expert Member
- Jul 21, 2010
- 7,594
- 4,798
wana JF habari toka tarime zinasema serikali imekataa kuruhusu wale marehemu waliouwawa na polisi kuagwa uwanjani kabla ya kwenda kuzikwa...
source; tundu lissu
Tundu Lissu
(7 minutes ago)
Niko Tarime tangu jana jioni. Na jana mchana Jeshi la Polisi likiongozwa na Kamishna wa Polisi Chagonja walikubalina na ndugu wa marehemu pamoja na uongozi wa CHADEMA ukiongozwa na Wakili Mabere Marando kwamba marehemu wataagwa katika uwanja wa Saba Saba kesho kuanzia saa 2 asubuhi kabla ya kupelekwa katika vijiji vyao kwa ajili ya mazishi. Tumekuwa katika maandalizi ya mazishi hayo tangu jana jioni. Hata hivyo, jioni hii tumeletewa barua ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Tarime kututaarifu kwamba haturuhusiwi tena kuwaaga marehemu wetu kama ilivyokubaliwa jana. Nimewasiliana na uongozi wa juu wa CHADEMA i.e. Mwenyekiti Mbowe na Dr. Slaa juu ya jambo hili na wao wakazungumza na IGP Mwema. Inaelekea, according to Mwenyekiti quoting IGP Mwema kwamba amri ya utukataza kuwaaga marehemu imetoka juu zaidi na nje ya Jeshi la Polisi. This could only mean Ikulu au Ofisi ya Waziri Mkuu Pinda. Msimamo wetu ni kwamba polisi waliowaua Watanzania hawa hawawezi kutufundisha namna ya kuomboleza au kuwalilia hao waliowaua! Inaelekea wanachotaka kufanya na kuzuia Arusha kujirudia: mara baada ya mauaji ya Arusha tulifanya mazishi ya umma kwenye viwanja vya NMC ambayo yalihudhuriwa na zaidi ya watu laki moja na ambayo yalikuwa ya amani entirely. Kama mnavyojua, mjadala ulioibuka baada ya mazishi hayo ya amani ulihoji kama polisi walikuwa na sababu yoyote ya kuua waandamanaji waliokuwa wanaandamana kwa amani. Kuna hoja imejengwa kwa muda mrefu sana kwamba watu wa Tarime ni wakorofi na wapenda fujo. Hoja hiyo imetumika kuhalalisha mauaji ya wananchi wa Tarime: waliouawa wiki iliyopita wanafikisha idadi ya wananchi wa Nyamongo waliouawa kwenye Mgodi wa North Mara kufikia 28 tangu tarehe 20 Julai 2005 walioua watu watatu wa kwanza. Hadi sasa hakuna mtu yeyote ambaye amewahi kukamatwa au kushtakiwa au kuwajibishwa kwa namna yoyote ile kutokana na kuhusika na vifo hivi. Wote waliouawa wameuawa mchana kweupe mbele ya mashahidi. Utaratibu wetu wa kisheria unataka kifo chochote chenye utata kichunguzwe katika Mahakama ya Korona (Coroner's Court) ili kuthibitisha kama kina lawama au la! Hakujawahi kuwa na mahakama ya aina hiyo katika mauaji yote 28. Umefikia wakati wa kumaliza tatizo hili la mauaji ya wananchi wetu. Kama ni kweli ni wavamizi au majambazi kama alivyodai Waziri Kagasheki ni wajibu wa Mahakama ya Korona kuamua hilo sio mkuu wa wauaji! Kama majambazi hawa wanastahili adhabu ya kifo au la ni kwa mahakama za nchi yetu kuamua na sio police executioners! Sisi hatutakubali kuliachia hili liishe hivi hivi. Watu 28 ni wengi sana kufa bila maelezo ya kuridhisha. Tuko hospitali ya Tarime usiku huu na hatutaondoka hapa mpaka tuwazike wafu wetu kwa tunayoifahamu sisi na sio tunayotakiwa kufundishwa na Jeshi la Polisi la Tanzania! Kama waliua hadharani kwa nini hawataki tuomboleze hadharani? Tunaomba Watanzania mtusaidie kwenye jambo hili