Mazishi ya Prof. Jwan Mwaikusa

Pasco amekwama sehemu lakini updates ziko kama ifuatavyo:

Heshima za mwisho zimeisha toka Nkrumah Hall, na msafara wa kuelekea nyumbani kwa marehemu Sala Sala uliongozwa na pikipiki ya Traffic.

Mwili wa marehemu kwa sasa upo nyumbani ukisubiri taratibu za kifamilia
 
Mungu awafariji wafiwa na watanzania wote.
Nimesikitika sana kwa MAUAJI ya Prof. Ingawa sikuwa namfahamu ila biograph yake niliisoma kupitia makala ya Mukajanga a day after his assassination.

Najua kuna mkono wa watu humo ila MAZINGIRA yatawahukumu.
 
Mwili ushashushwa toka kwenye gari lililoubeba aina ya Mercedes Benz (Station Wagon) ambalo kwa nyuma lina vioo kitendo kinachomfanya mwombolezaji kuliona jeneza kirahisi, jeneza limeingizwa ndani kwa taratibu za kifamilia
 
MC kiongozi ni Dr. Sengodo Mvungi akisaidiwa na Hussein Kitta. Kuna idadi kubwa ya wanasheria na wamevalia mavazi yao rasmi wakiongozwa na Jaji mstaafu Barnabas Samatta, Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu, mawakili, mawaziri, wawakilishi wa vyama vya siasa akiwemo mchungaji Mtikila pia na wanajumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamejitokeza kwa mamia.

Ibada ya mazishi inaanza.
 
Ibada imeisha, haikuwa ndefu sana. Sasa zinaanza heshima za mwisho kwa miili ya marehemu wote wawili (pamoja na wa nduguye waliyeuawa pamoja Gwamaka).
 
Mavazi ya Majaji na wanasheria inaelekea yanawapa taabu (majoho mekundu na meusi mazito yanasharabu jua hivyo kuwasababishia joto)
 
Heshima za mwisho zinaendelea.

Pasco ni mmoja wa wanafunzi wa marehemu, alimfundisha UDSM, na anadai alikuwa mwalimu aliyonekana kwa wengu kuwa 'very fair'. Alibahatika kukutana naye Dodoma mwezi Aprili na walikaa Dodoma Hotel pamoja na Doc. Mwakyembe.

Wakiwa katika maongezi, Dr. Mwakyembe aliwambia kuwa maisha yake mwenyewe (Mwakyembe) yapo hatarini kwani kuna assassin alikuwa amelipwa kuhakikisha anamtoa roho lakini huyo mtu baadae aliingiwa na 'roho ya huruma' akaenda kwake Mwakyembe na ku-confess. Aliwambia kuwa alilazimika kusambaza taarifa hizo panapohusika na kuwambia kuwa chochote kitakachotokea basi wasishtuke kwani kuna mpango dhidi yake umepangwa. Prof. Jwan (marehemu) alimpinga na kusema "Death is always a surprise, as long as none can anticipate death".

Heshima za mwisho zinaendelea, kuna watu wengi sana
 
Asante sana mkuu Invisible kwa kutujuza.

Mungu awarehemu Prof na mwanaye.
 
Maprofesa wafuatao wameonekana mazishini:

Mark Mwandosya, Pius Ng'wandu, Issa Shivji, Geofrey Shaidi, Palamagamba Kabudi, Costa Mahalu, Fulgence Kazaura, Rwekaza Mkandala, Hamudi Majamba, Gamalieli Mgongo na wengine wengi.
 
Tangu heshima za mwisho zinaanza kutolewa takribani dakika 15 hivi, bado ni wanawake wanapita na muda wa wanaume bado!
 
Nimrod Mkono na Israel Sekirasa (wa SUMATRA) wanaonekana kuhudhuria pia. Kutokana na uwingi wa watu, zoezi la kuuaga mwili wa marehemu LIMEAHIRISHWA, waliobaki wataaga kwa 'jumla' baada ya mwili kutolewa nje. Sasa wanafamilia ndo wamepewa nafasi ya kuaga, wanaangua vilio sana
 
natoa pole sana kwa familia pamoja na wana jf wote walioguswa kwa namna moja au nyingine.wawe wapole mambo yote yatajulikana baada ya muda si mrefu.
 
Heshima za mwisho zinaendelea.

Pasco ni mmoja wa wanafunzi wa marehemu, alimfundisha UDSM, na anadai alikuwa mwalimu aliyonekana kwa wengu kuwa 'very fair'. Alibahatika kukutana naye Dodoma mwezi Aprili na walikaa Dodoma Hotel pamoja na Dr. Mwakyembe.

Wakiwa katika maongezi, Dr. Mwakyembe aliwambia kuwa maisha yake mwenyewe (Mwakyembe) yapo hatarini kwani kuna assassin alikuwa amelipwa kuhakikisha anamtoa roho lakini huyo mtu baadae aliingiwa na 'roho ya huruma' akaenda kwake Mwakyembe na ku-confess. Aliwambia kuwa alilazimika kusambaza taarifa hizo panapohusika na kuwambia kuwa chochote kitakachotokea basi wasishtuke kwani kuna mpango dhidi yake umepangwa. Prof. Jwan (marehemu) alimpinga na kusema "Death is always a surprise, as long as none can anticipate death".

Heshima za mwisho zinaendelea, kuna watu wengi sana

Invisible na Pasco... yaani nimesoma hii post nikasikia kama mwili umepigwa shoti ya umeme!!!! Roho imeniuma kama nilimjua marehemu...

Gone are the days when we trust one another
 
Invisible na Pasco... yaani nimesoma hii post nikasikia kama mwili umepigwa shoti ya umeme!!!! Roho imeniuma kama nilimjua marehemu...

Gone are the days when we trust one another
Mkuu De Novo, mwenyewe nimejaribu kufikiria na kuanza kuamini kuwa Tanzania is no longer safe!

Mwili wa marehemu sasa unapelekwa makaburini na jeneza lilibebwa na walimu wa sheria tu wakiwa wamevalia majoho yao.

Kaburi lipo jirani na nyumbani, limeshajengwa na kunakshiwa na vigae (marumaru)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom