Mazishi ya Muasisi wa Chama yapata msukosuko

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Mazishi muasisi CHADEMA yapata msukosuko

na Christopher Nyenyembe

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani hapa, kimepata msukosuko kwenye mazishi ya muasisi wa chama hicho, Edna Kanjanja, baada ya kikundi cha watu waliodai kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, kuamuru bendera iliyokuwa imefunikwa kwenye jeneza iondolewe.


Watu hao wanadaiwa kumshinikiza Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) jijini Mbeya, Godlove Mwapyale, kuondoa bendera hiyo iliyokuwa juu ya jeneza, vinginevyo asingeweza kuendesha ibada ya mazishi.

Tukio hilo lililotokea jana, saa nane mchana nyumbani kwa marehemu, eneo la Kituo Kikuu cha Mabasi, Kata ya Sisimba, nusura lizushe vurugu ambazo kwa busara ya pekee kutoka kwa viongozi wa CHADEMA Mkoa, waliwazuia wanachama wenzao waliopandwa na jazba kutokufanya chochote.


Akizungumza na Tanzania Daima baada ya mazishi hayo yaliyofanyika kwenye makaburi ya Nzovwe jijini humo, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, George Mtasha, alisema chama hicho kimesikitishwa na kitendo kilichofanywa na watu hao.


Akielezea tukio hilo, alisema chama hicho kilikuwa kimeandaa gari aina ya Toyota Pick up kwa ajili ya kubeba mwili wa marehemu, huku gari hilo likiwa limefungwa bendera ya chama na nyingine kufunikwa kwenye sanduku, lakini walijikuta kwenye wakati mgumu walipoamriwa kutoa bendera hizo.


"Mimi kama Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa, nilikuwa nimemwakilisha Mwenyekiti wa Taifa ambaye hakuweza kufika, ili kuhakikisha tunafanikisha mazishi ya Kanjanja na anazikwa kwa heshima zote za chama, badala yake wakajitokeza watu watatu na kuamuru bendera ziondolewe.


"Marehemu alikuwa Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa, ni mlezi wa chama mkoa na mdhamini, hivyo isingewezekana akazikwa bila kupewa heshima na chama. Mbona wenzetu CCM wanafanya hivyo, lakini bendera zao haziondolewi? Iweje watu hawa waondoe na kutupa chini bendera zetu?" alihoji mwenyekiti huyo.


Viongozi kadhaa wa chama hicho walieleza hali hiyo si ya kidemokrasia na wanafanya mawasiliano na Makao Makuu, ili kuchunguza na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu hao.


Kanjanja aliyezikwa jana, pia aliwahi kuwa mhasibu wa chama hicho mwaka 1995-2004 na mjumbe wa baraza kuu toka mwaka 2004-2008. Ameacha watoto wawili, Daniel na Irene.
 
marehemu alale pema peponi.

hao mambo ya ndani naona walikuwa wanatafuta zogo tuu hususan
kama bendera zilizohusika zilikuwa za chadema.
 
Haaah! Kweli hii inashangaza kama sio kusikitisha. Niliposoma heading ya thread nilidhani ndani nitakutana na story may be bendera iliyozuiwa ni ya taifa, kumbe ni ya chama.! What the hell is this?

Inavyoonekana itafika mahali hawa CCM watukataze hata kuwasiliana sisi kwa sisi. Huo ni ukoloni wa fikra, tuukatae!
 
Dah!Yaani uhuru sasa "unabakwa" kwa kila hali.Nyakati zimebadilika serikali,chama tawala kitambue hivyo.
 
Back
Top Bottom