Mazishi ya Mtu Asiye na Dini

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,077
17,208
Habari zenu,

Hivi watu ambao hawana dini huwa hawafi au?

Manake humu JF wapo wengi wasioamini uwepo wa Mungu lakini kiuhalisia sijawahi kuhudhuria mazishi ya Mtu asiyeamini uwepo wa Mungu hapa Tanzania,

Sasa kwa anayejua hebu atupe experience Huwa wanazikwaje zikwaje?

Wanaombewa dua na kusaliwa?
au inakuaje kuaje?
-
SWALI LA NYONGEZA KUTOKA KWA CleverKING
-
Mleta mada naomba niunganishe hili swali
kwenye hii mada yako...
Ni hivi,nijuavyo mimi kwa mfano,
Waislamu wana makaburi yao na Wakristu
wana makaburi yao, je hawa wasio amini
dini yeyote huzikwa kwenye makaburi ya dini ipi?
 
Habari zenu,
Hivi watu ambao hawana dini huwa hawafi au?
Manake humu JF wapo wengi wasioamini uwepo wa Mungu lakini kiuhalisia sijawahi kuhudhuria mazishi ya Mtu asiyeamini uwepo wa Mungu hapa Tanzania,
Sasa kwa anayejua hebu atupe experience Huwa wanazikwaje zikwaje?
Wanaombewa dua na kusaliwa?
au inakuaje kuaje?
Dar es salaam wanaombewa wanaimbiwa lakin mikoan haipo iyo
 
Unayo dini au Hauna dini utazikwa tu,Kama Una dini utazikwa na sheikh Kama ni muislam ama Kama mkresto utazikwa mchungaji ama padri..
Kama hauna dini utazikwa tu kwa style yoyote ile,hata manispaa watakuzikaaa tu...

Ovaaa
 
One of my relatives walikuwa wakristu by then they badae wakawa wapo Tu walipofariki kaburi lilichimbwa wakafukiwa, hakuna padre wala sheikh so what???
Anhaa, Sasa wamewapa maelekezo ya kuwazika au mlijiamulia wenyewe tu?
 
Hahaaaa hua ipo mkuu mi niliwahi kuikuta sehemu na ilikuwa hv kwa mzee alieandaliwa!!!
Musiba hoyee!!!
Jenesa nzuri si nzuri!
Marehemu imependesa hijapendesa!!!
Kwansa natangulisa shukurani sangu sa satii kwa hii mutu kufa!!
Nashukuru imekufa kwansa imesababisa sisi tumekula muchele ambayo hua tinakulaga sikukuu tuu na imesababisha sisi tukanywa ile maji ambayo wanakunywagwa ile inayofanyaga kazi maofisini kule mujini!!
Musiba hoyeee!!!


 
Kuzikwa ni utaratibu wa dini.. sasa hawa kama wanajinadi kuwa hawana dini.? basi ni vema wapelekwa mstuni au baharini
Nani aliyekwambia kuwa kuzikwa ni utaratibu wa dini.. ?! So paka na wanyama wengine wanapozikwa huwa kwa dini gani ?!
Kuzika kumekuja baada ya kuona umuhimu wa kuhifaziwa mzoga wako maana ukiachwa nje utanuka uozo na haitapendeza..

Pia the idea of seeing ur beloved one rotting is not good ! So what can be done ?! Be buried or cremated !
 
Back
Top Bottom