Mazishi ya Mh. Regia Mtema huko Ifakara (updates)

Hapana usalama wa jk uko intact ila ni kuepusha kuacha ratiba zingine za ziara yake mkoani kwetu
 
Hali ya hewa ni cool,maombolezo na nyuso zenye simanzi,

wabunge wengi wamefika,viongozi mbalimbali wamefika.

Mkuu wa kaya mpaka sasa wanasema atafika kwa Choppa.

Tunaendelea kuwaweka watu kwenye nafasi zao,tukiendelea kusubiri.

Pole sana Mamii jipe moyo
 
Tunawashukuru wote mnaotujuza mambo ya ifakara. Poleni sana, kwani najua kwa vile watu ni wengi mnajitahidi sana kupata updates.
 
Wakati huu ni mgumu zaidi Josephine. Haulingani na ilivyokuwa Ruvu ajalini, Tumbi hospitali, Muhimbili, Tabata, Kanisani Segerea, Karimjee wala njiani kuelekea Kilombero. Kote huko mliiona maiti yake au Jeneza lake. Sasa mnamuaga rasmi. Hamtamwona tena Regia.
 
Hapana usalama wa jk uko intact ila ni kuepusha kuacha ratiba zingine za ziara yake mkoani kwetu

.
Siku zote mahali walipokusanyika wana chadema ni amani na salama. Ukiona hali ya hewa imechafuka, fuatilia mara zote kama hutakuta ni polisi wa sisiem wameichafua.
.
 
Tuliambiwa kwamba na msaidizi wake wa kazi za ndani alifariki.
Mbona hatuambiwi kama wanazikwa wote sehemu moja au yeye anazikwa wapi(kwao)
na lini?
 
so painful!kila nikimuwazia twin wake naumia zaidi maana naona atakuwa na uchungu kuliko mtu yeyote!!R.I.P Regia na Mungu ampe nguvu Remija ya kuvumilia na kujua sisi wote ni wapitaji hapa dunian
 
Tububujikwe na machozi huku tukikumbuka kuwa wote tupo safarini, kwa hiyo cha msingi ni kujiweka tayari muda wote mungu atakapotuhitaji kwenye makao ya milele- Mioyo na wanyonge wote aliowatetea itakuwa faraja kwake huko aliko - Kwa muda wake duniani Regia katimiza wajibu wakei, tujiulize je sisi tunatimiza wajibu wetu?, Je tunawapa chakula wenye njaa? Je tunawafariji wenye shinda? Tunawatetea wanyonge? Je tunagawana kilichopo kwa usawa? je tuna upendo wa dhati kwa wenzetu? n.k

Maisha ya duniani ni mapito, tukumbuke kujenga hazina mbinguni kama wenzetu Regia alivyopigania kila siku - kuwakomboa wanyonge hasa vijana wa nchi hii. R.I.P Regia, you have done your duty - kazi ni kwetu sisi tuliobakia duniani tujiulize kama tunatekeleza wajibu wetu ipasavyo kama mwenyezi mungu alivyokusudia uwepo wetu duniani.

Mama Josephine na wote huko, mungu awape ujasiri kumalizia shughuli ya kumlaza mwenzetu kwenye nyumba yake ya milele. amin. So painful....very hard to accept...
 
Dah siwezi amini yaani ndo safari ya mwisho hii kwa my Dear Hon. Regia, Rest in Peace
Pamoja Josephine endeleea kutupa updates!
 
Kifo chako, maombolezo yako na mazishi yako dada regia umeandika historia mkoani morogoro, nauota mkoa mpya wa kilombero, naiota wilaya mpya ya malinyi naliota daraja na barabara nzuri ya lami mikumi-ifakara-malinyi-songea; uliamini ktk hilo nasi tulikubaliana na wewe, sasa umetuacha kimwili tukiwa na tumaini lilelile ulilolijenga juu ya mambo haya dada Regia.

Nenda salama mwana wa bonde la mto kilombero, nenda kwa amani mwisukulu mtemanyenja, muhumbo mulungu atutangi twayaku, upate pumziko la amani regia e.mtema.
 
Nilipokuwa nasikiliza propaganda za ccm kidogo nikubali kuwa chadema ni cha wachagga.
Nikamwuliza rafiki yangu je regia watampeleka marangu au machame?
Akaniambia achana na hao mafisadi wanawadanganya watanzania ili wawaibie.
Poleni naa masiba malizeni mrudi watanzania wanawasubiri wakombozi wao.

R.i.p dada regia.
 
Back
Top Bottom