Mazishi ya Kanumba, kamati yapiga hela ndefu

Mbali na misiba hata kwenye harusi muhimu waweka hazina wawe ndugu aliyependekezwa na wanandugu. Nakumbuka yaliyonitokea kwenye kamati ya harusi ya kaka baada ya kubaki salio la 1000000/= mwenyekiti na katibu wakataka 400000 nikawamgomea then baada ya harusi wakataka kutumia hizo hela kuvunja kamati nikagoma. Baada ya fungate nikamkabidhi kaka akazitumia kununulia mabati na kumalizia nyumba yake ijapokuwa walinichukia lkn baadae walieleweshwa
 
Pamoja na yote ila ni fundisho kubwa sana kwa sisi tulobaki.....mtu akipata mafanikio anakaa mbali sana na familia kiasi cha kuwa anamilikiwa na jamii zaidi ya familia yake (sikatai kupendwa na watu wanaokuzunguka hata kushirikiana nao) ila haya ya kamati ya mazishi ya style hii ni indicator ya modern culture kutawala sana maisha kiasi cha kukosa hata uamuzi wa kifamilia kwenye mambo ya maana, makubwa na mazito it be a sad or happy moment.

Mytake; Kwa yaliyotokea yawezekana kuwa hata yeye marehemu alikuwa anawachukulia wazazi wake "poa" mbele ya marafiki zake ndo maana hiyo kamati ilikuwa na nguvu to that extent.......tumeona misiba mingi ya watu wa caliber tofauti tofauti oftenly last say hutoka kwa wazazi au familia husika, wengine mnakuwepo kutoa ushauri na kuhakikisha mipango ya familia inaenda sawa. In other words tunapopata mafanikio kwa umakini tupiganie sana umoja na ustawi wa familia zetu ili iwe kimbilio wakati wa maisha, ugonjwa na umauti na kamwe hatutokaa tujute.....we shud never leave our parents and families exposed, spineless and with an egg shell status.....we shud always avoid these at any cost

Ushauri: Kama umeamua kuishi hiyo modern culture then weka will mapema kama wafanyavyo hao walioianzisha ili kuja kupunguza mivutano kama hii otherwise tegemea familia yako kuyumba sana sana pindi utakapo oa, zaa, ugua au aga dunia


Ni maoni tuuu

ulichosema ni kweli kabisa
 
Waliokula hela za msiba watapata matatizo makubwa sana,mi yangu macho mi kinachonishangaza walishatangaza kuwa mtu asiye mwanachama wao hawataenda ilikuaje tena kuwa mpaka kwn kamati? wewe JB na wenzako mmeshalaanika mtabakia kununua vigari vitagongwa mtabaki km mlivyo. maneno ya watu ni mabaya sn nyie hata kwa siri rudisheni,hata haya hamna looooh! usuper star wa njaa tu nyie ndio mngeongoza kwa kutoa michango mikubwa kinyume chake nyie ndio mnaiba mtapukutika km ***** mi nipo hapa!
 
mkuu inawezekana ni matumizi mabaya ya hela,pia msimba mkubwa kama ule nadhani pia matumizi yatakuwa mengi...ila kama kweli kuna hujuma imefanyika basi ubinadam kazi

Mi nadhani kila kitu kilikuwa documented... Hasa mapato.. Kwenye matumizi hapo inategemea...

Lakini gharama za ujenzi wa majukwaa,kampuni ya mazishi,na vingine vina documents.. Sijui vyakula..
 
naskia milion 30 zilitumika kununulia suti nyeusi za tukio..

Kha! ivi ilikuwa lazima kuvaa suti nyeusi kama huna. Kwanini iwe gharama ya wafiwa? Kwani si wangevaa nguo zao nyeusi tu kama mtu hana suti. Hii kwakweli kwa mtizamo wangu ni mis-use of funds. Sidhani kama familia ya Kanumba ingekubaliana na hili.
 
Wengi mtakuwa mmefatilia kwa karibu yote yaliyotokea katika kifo cha Msanii Steven Kanumba. Baada ya kifo hiki watu mbalimbali wakiwemo wabunge wamezidi kupaza sauti zao kutaka kifanyike kitu ili kazi za wasanii zisiimbiwe. Hii ndio iliyonipelekea kuandika hili ili kuona changamoto hii tutaikabili namna gani.

Wote tulishuhudia Clouds FM radio na TV zikirusha na kutangaza live matukio yote ya kifo cha Kanumba. Ila sina uhakika kama Familia ya Marehemu Kanumba ilitoa idhini ya chombo hicho cha habari kufanya hivyo walivyofanya. Na kama walipata ni kiasi gani familia imelipwa kwa ajili hiyo. Na kama hawajafanya yote hayo (Kupata ruhusa na kuliilipa familia) basi wamefanya WIZI mkubwa.

Hakuna atakayebisha kwamba Chombo hicho cha habari kimejinufaisha sana na msiba ule kwa njia mbali mbali. Kwanza watu wengi kukijua kuwa kipo, watu wengi kununua starTY ili tu wanase Clouds TV na kushuhudia matukio ya msiba wa Kanumba na pili kuwanyima haki wanafamilia kuja kutoa DVD za coverage yote ya musiba wa Kanumba na kupiga pesa kidogo kwa ajili ya maisha.

Wote wanajua wenzetu walivyofaidika kwa kuuza rights za matangazo. Mfano kifo cha Michael Jackson, Whitney Huston na hata mjuu kuu wa mandela aliyetaka kuuza rights za kurusha kifo cha Mandela kabla hata hajafa.

TUTAMALIZAJE WIZI HUU WA VYOMBO VYA HABARI KAMA CLOUDS RADIO AND TV. Nipo tayari kufungua kesi ya madai kwa niaba ya familia ya Kanumba ili Clouds Walipe maana wamefaidika.[/QUOTE
 
Shitaki peke yako.Hatuna haja kuangalia ya KImagharibi.Hatujaja kuishi kutegemea mali za marehemu.Usilete uchonganishi.Usiwachonganishe waliofanikisha zoezi na kuwakashifu.Au ulitaka uteuliwe wewe!
 
Ulichoongea ni kweli kabisa. By the way, hivi walipata wapi ruhusa ya ku'spend hizo so called "70 million"? Its like karibia hela yote iliokusanywa wamesema imeenda kwenye gharama za mazishi wakati familia iliokua inamtegemea marehemu imeachwa with peanuts! Kwanza, its obvious msiba hauku cost all that money, and familia ilitakiwa kua na maamuzi ni jinsi gani msiba uwe na hata gharama zake. Alafu they should provide mchanganuo wa jinsi walivotumia hizo hela supported by receipts! Sio tu kudanganya watu. Yaani watu wengi wanalalamika sana, kamati imetia aibu!




Waliokula hela za msiba watapata matatizo makubwa sana,mi yangu macho mi kinachonishangaza walishatangaza kuwa mtu asiye mwanachama wao hawataenda ilikuaje tena kuwa mpaka kwn kamati? wewe JB na wenzako mmeshalaanika mtabakia kununua vigari vitagongwa mtabaki km mlivyo. maneno ya watu ni mabaya sn nyie hata kwa siri rudisheni,hata haya hamna looooh! usuper star wa njaa tu nyie ndio mngeongoza kwa kutoa michango mikubwa kinyume chake nyie ndio mnaiba mtapukutika km ***** mi nipo hapa!
 
Binafsi naona tatizo ni kuwa na mtu mmoja tu "nguzo" katika familia au pengine hata katika ukoo mzima,anapoondoka sasa matokeo yake ndo yanakuwa kama hayo,msiba ulikuwa ni wa Kanumba iweje kamati isimhusishe hata ndugu mmoja wa Kanumba,eti alikuwepo akaondolewa kwa sababu kamati ilitaka ifanye mambo kwa uhuru zaidi,ni uhuru gani waliokuwa wanautaka zaidi ya ule wa kuiba,mimi nafikiri Familia yenyewe ndo inapaswa kujilaumu kwa kutengeneza mwanya huo.
 
KAMATI YA MAZISHI YA KANUMBA NA KASHFA YA KUCHAKACHUA MICHANGO

Hawa wenye suti na miwani myeusi ndio baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wanaodaiwa kufanya upigaji huo wa fedha za michango ya msiba

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka ndani ya familia ya Kanumba, kamati hiyo imedaiwa kufanya uchakachuaji wa michango hiyo inayokadiriwa kuwa mamilioni ya fedha, achilia mbali

vitu kadhaa, yakiwemo magunia 32 ya mchele.
Chanzo hicho kimeidokeza Sayari kuwa, dalili za hali hiyo zilianza kujitokeza mapema kabisa pale mwanandugu mmoja alipoenguliwa kwenye kamati hiyo, kwa kile kinachoelezwa, kamati hiyo kufanya jukumu hilo kwa uhuru zaidi.
Dalili nyingine, ni kitendo cha wajumbe wa Kamati hiyo kutoweka baada ya mazishi hadi walipofika nyumbani kwa marehemu Alhamisi usiku.
Kwamba, pamoja na mambo mengine, kwenye kikao kilichofanyika siku hiyo kati
ya wanandugu na kamati hiyo, Mama Kanumba amezuia kuzungumzia suala la michango.
"Mama Kanumba ametakiwa asiseme lolote kwa Waandishi wa Habari kuhusu michango&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; kaelezwa kama atafanya hivyo, huenda asipate kitu kabisa," alisema ndugu huyo.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Kamati hiyo imetoa onyo hilo kwa vile tangu kwisha kwa maziko ya Kanumba, wamekuwa wakipata usumbufu wa simu watu kuulizia kilichokusanywa na kilichobaki.
Chanzo hicho kimedokeza kuwa, baada ya kamati hiyo kukutana na wanafamilia kwa mara ya kwanza baada ya ukimya mrefu, ilisema michango yote ni sh mil 51.
Kati ya fedha hizo, gharama za mazishi ni shilingi mil 48 huku kukiwa na deni la sh
mil 2 za ukarabati wa barabara Leaders kutokana na uharibifu uliofanywa na waombolezaji.
Chanzo hicho kimedokeza kuwa, walipohoji fedha zilizochangwa kupitia M-pesa kupitia namba ambayo ilitangazwa, walielezwa ilipatikana sh 20,000 tu.
Kilisema, kiasi hicho ni kiduchu mno kwa sababu mashabiki wa Kanumba wa Mwanza pekee, walichanga sh 300,000.
Kilidokeza kuwa, pia kulikuwa na gunia 32 za mchele zilitotolewa na msamaria, hazijulikani zilipokwenda.
"Licha ya kutolewa gunia 32 za mchele, hazijulikani zipo wapi&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];. fikiria hata mfiwa, anakosa hata gunia moja la kwenda kuanzia maisha mapya bila mwanaye," kilidokeza chanzo hicho.
Kilipoulizwa kwanini hawakuweka ndugu kwenye kamati hiyo tangu mapema, kilisema alikuwemo, lakini akaenguliwakwa kwa zengwe.
Uratibu wa msiba huo ulikuwa chini ya Kamati iliyokuwa chini ya Gabriel Mtitu na wajumbe kama Ray, Cloud, Steve Nyerere, Hapines Magese, Mtitu William, Jacob Steven na wengineo.
Sayari ilipomtafuta Mtitu kwa njia ya simu jana, alisema kutokana na usumbufu ambao wanaupata kwa wengi kutaka kujua juu ya michango hiyo ya msiba, Kamati yake imeamua kukutana na waandishi wa Habari kesho Jumanne kuweka kila kitu bayana.
"Kuna mengi yanasema hadharani na chini ya zuria kuhusu rambirambi, kwa lengo la kuweka bayana kila kitu, tumepanga kukutana na waandishi wa Habari Jumanne (kesho) kuanzia majira ya saa nne," alisema Mtitu.
CHANZO:GAZETI LA SAYARI
Ni kawaida ya watu waOVU kupenda kuvaa mamiwani makubwa myeusi kuficha Sura zao huku dhamira zikiwasuta. Walikuwa wapigaji hawa.
 
Back
Top Bottom