Mazishi arusha vs kula kuku zanzibar

Mkombozi

JF-Expert Member
Feb 19, 2008
806
426
Hali ya kusikitisha ni kwamba mauaji yaliyotokea yanaonekana kama Serikali iliua sisimizi.Wakati wakazi wa Arusha wameomboleza leo,Viongezi wa juu wa Serikali wako Zanzibar wanakula kuku.Hii ni dharau kubwa na serikali imeonesha hata ikiua idadi yeyote ya raiya hamna anayejali.Waliuawa wafanyabiashara wa Morogoro ikaundwa tume.Haya ya arusha wmegfanya kama wanyama.Inakuaje nyumbani kwako kuna msiba halafu unafanya sherehe?Ni dharau kubwa kwa wakazi wa Arusha na watanzania kwa ujumla.Nimesikitika sana
 
Mkuu ulitaka sherehe yao iahirishwe? au ulitaka nini hasa kifanyike na wazanzibar?
 
Mwanza, Musoma na Shinyanga msilale.

Jumamosi TUNATAKA MAANDAMANO!!!!

Kwa ruhusa au bila ruhusa
 
Hali ya kusikitisha ni kwamba mauaji yaliyotokea yanaonekana kama Serikali iliua sisimizi.Wakati wakazi wa Arusha wameomboleza leo,Viongezi wa juu wa Serikali wako Zanzibar wanakula kuku.Hii ni dharau kubwa na serikali imeonesha hata ikiua idadi yeyote ya raiya hamna anayejali.Waliuawa wafanyabiashara wa Morogoro ikaundwa tume.Haya ya arusha wmegfanya kama wanyama.Inakuaje nyumbani kwako kuna msiba halafu unafanya sherehe?Ni dharau kubwa kwa wakazi wa Arusha na watanzania kwa ujumla.Nimesikitika sana

Mkombozi,

Leo kwa wazenj ilikuwa kusherehekea ukombozi wa umma wao. Kwa hiyo, si rahisi kuiahirisha sherehe kama hii ya kitaifa.

Ninakuelewa hisia zako , lakini pia tizama mambo kwa ujumla wake! Kikwete na viongozi wa bara na Muungano ni waalikwa tu leo huko Zenj. Wenye sherehe ni wazanzibari.

JK alisema , "Zanzibar ni nchi nadani ya muungano"
 
Mkuu ulitaka sherehe yao iahirishwe? au ulitaka nini hasa kifanyike na wazanzibar?

sera za kikwete za kususa kwa sababu ya hasira.

kwa nini wasitume hata muwakilishi wa serikali?

mbona maziko ya dr. remy walituma kiongozi wa serikali.

aibu kuu.

ccm inakufa hivihivi nikiwa ninaona. kweli kila kitu kina mwisho wake!!!

chadema msilegeze. tunawasapoti. tunawakumbuka katika sala zetu. mtashinda!!
 
Hakuna lililoharibika,vyote vilikuwa muhimu na vyote vimefanyika vizuri......maisha yaendelee,we do not have to argue about everything!
 
sera za kikwete za kususa kwa sababu ya hasira.

kwa nini wasitume hata muwakilishi wa serikali?

mbona maziko ya dr. remy walituma kiongozi wa serikali.

aibu kuu.
Mkuu,

Wao ndio wauaji halafu watume wawakilishi wa nini?

Yaani si itakuwa ni usanii tu ,pia kuwaongezea waombolezaji uchungu na hasira?

Bora tu wameacha waombolezaji wamefanya mazishi bila kusababishiwa kuhisi "kichefu chefu" cha kuwepo kwa mwakilishi wa serikali.
 
Napenda msimamo wako huu uwe wa viongozi wa chama chako! will support that

chadema wanaweza kufanya maandamano bila vurugu. kwani hukuona leo msafara wa kutoka hospitali kwenda viwanja vya nmc? mbona wamelinda wao wenyewe chadema bila hao wazee wa intelijensia?
 
chadema wanaweza kufanya maandamano bila vurugu. kwani hukuona leo msafara wa kutoka hospitali kwenda viwanja vya nmc? mbona wamelinda wao wenyewe chadema bila hao wazee wa intelijensia?

mkuu...leo ndio imedhihirisha kuwa ... kati ya serikali na chombo chake cha maovu ...polisi ...ni nani alivunja amani siku ya tarehe 5/01/2011 ..., leo tumeshuhudia watanzania walivyo wapenda amani bila kujali dini na kabila ...CCM itawatokea puani propaganda na mbinu yao ya kuwagawa matanzania kwa kutumia udini kwani mungu ndio anaonyesha uhalali upo wapi... bravo wanamapindizi wa demokrasia... tudumishe undugu wote kwa pamoja

on board sisiem pia wanakaribishwa kuungana na tanzania mpya inayojali demokrasia na haki...

almighty god rest the souls of our beloved heroes in eternal peace.... amen ...amen...., amen
 
nadhani tusiwalaumu bali tuwaombee kwa mungu awasamehe dhambi zao. Kuua si mashara roho inakuwa inakusuta saana na hufikia hata wauaji kujiua wenyewe.

Kwa uwezo wake mwenyezi mungu atawalipa haki yao tusiumize kichwa na mwak huu huu mtaanza kuona mapigo ya mwenyezi mungu yakiwashukia moja baada ya mwingine.

Pia mkumbuke kuwa wengi kati yao ni wagonjwa hivyo tuzidi kuwaombea zaidi mungu awasaidie wapate afya njema.

na hao wenzetu wapemba waliouwawa ni ndugu zetu tusibaguane kwa Utanganyika na Uzanzibar sote ni Watanzania na Afrika ni moja.

Sumu ya ubaguzi itatupeleka pabaya hivyo si vyema kuichochea na tena nawaasa wana JF kuacha kabisa hizi "comments" za Utanganyika na Uzanzibar, maana zikitoka hapo zitaingia kati ya Upemba na UUnguja, itakuja Umakunduchi n.k itatumaliza tuache kabisa haya.

Tuzungumzie jinsi gani tunaweza kuiondosha nchi hii ktk UFISADI bila kuangalia fisadi ni Mtanganyika au Mzanzibar.
 
chadema Arusha baada ya kuona miili ya marehemu inacheleweshwa kutoka kutokana na kufanyiwa uchunguzi wakaanza kuimba tunawapa dakika moja mkichelewa tunaingiaa tehe Mimi nawaambia 2015 nchi yetu hii
 
Back
Top Bottom