Mazishi aina hii yanatisha

Yaani kuna watu kumbaaf kabisa, hii thread aina mantiki yoyote apart of provoking a group of people. Napita admin ondoa hii...

Watu hufa kila siku, na watoto huzaliwa kila siku, nasi tunaojadiliana hapa lazima tutakufa na kuzikwa, na haya hutokea mara kwa mara. Huenda wewe ukishajua yanayoendelea unaweza kuacha wosia wako unapenda wakuzikeje, na kwa utaratibu gani ambao unaona inafaa. Kila siku tunazika wafu kwa njia mbalimbali, tamaduni mbalimbali, imani mbalimbali nk, nini cha ajabu kuona hii thread haina uzito stahiki?
 
jeneza kufukiwa na majari[/QUOTE]
Baadhi ya watu hawapendi au wanaumia kusikia sauti ya udongo au mabonge ya udongo yanapoangukia jeneza. Huenda hayo majani ni kupunguza kishindo cha udongo juu ya jeneza. Pia inawezekana hakuna jeneza hapo.
 
jeneza kufukiwa na majari
Baadhi ya watu hawapendi au wanaumia kusikia sauti ya udongo au mabonge ya udongo yanapoangukia jeneza. Huenda hayo majani ni kupunguza kishindo cha udongo juu ya jeneza. Pia inawezekana hakuna jeneza hapo.[/QUOTE]

download+(14).jpg



Kwa imani ya hayati sidhani kama amezikwa kwenye sanduku, ila ni sanda tu iliyohifadhi mwili wake. Unaweza kuona jinsi majani yaliyowekwa juu yake pembeni kushikizwa na mawe yanayoshindilia yale matawi na majani yaliyohifadhi mwili, unaona hata President amekunja uso kwa kuonja na kuhisi anapotia udongo.

Kwa vyo vyote kuna kitu kinatufunza hapa katika maisha yetu, tunajisikia tulivyo lakini ipo siku tutashindiliwa ndani ya handaki na miili yetu iendelee kudecompose. Dunia na viumbe vyake ni mzunguko kujirudia ulikotoka.
 
Kwa taarifa yako ukizikwa kwenye sanduku unavimba hadi sanduku nhalikutoshi. Kwa uzikaji huo,maiti analazwa moja kwa moja, udongoni na hayo majani chini yake kuna ubao kuzuia mchanga. Maiti huyo hatoi wadudu na atakaa mpaka atakauka na kubaki mifupa. Kama ni sehemu yenye baridi sana hata ipite mwaka atabaki hivyo hivyo. Therefore it is the best way of burial kwani ndio unarudi mavumbini kweli kweli, sio kucheleweshwa mpaka sanduku lioze ndio uonje udongo.

Anyway, tuwogope MwenyeziMungu kwani ipo siku tutakufa na kuulizwa juu ya matendo yetuu hapa duniani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom