Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Kuna njia mbalimbali za mazishi kadiri ya mila, desturi, tamaduni na mapokeo, hali kadhalika imani kama:
- kuichoma moto miili ya watu,
- kuivunja miguu ili shimo la kuzika liwe dogo,
- kuitumbukiza shimoni na jaza udongo juu yake,
- kuhifadhi mwili kwenye sanduku kisha kuutumbukisa shimoni,
- kuchimba shimo na kutengeneza chumba ambacho hakifikiwi na udongo,
- Kuitelekeza porini na kuhama makazi kama baadhi ya jamii za wachungaji, nk.
Wote hao na taratibu zao wanajali hadhi ya binadamu, na kwamba akishakata roho mwili ni udongo tu unaoweza kufanyiwa kwa namna ye yote ili kuufanya urudie udongo.
"Kumbuka binadamu u mavumbi na utarudia kuwa mavumbi."