Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,487
- 40,989
- Thread starter
- #21
Bora tu ungekuwa muwazi zaidi ukasema kuwa kuzaliwa kwake na kulelewa katika uislam ndilo tataizo badala ya kuzunguka.
Wanaosema nchi imemshinda wao hasa walitaka nchi iweje? Labda watoe mfano wa nchi yoyote ya kiafrika ambayo ina kiongozi shupavu amabe ameivusha nchi yake kutoka ktk dimbwi la umaskini? Hakuna.Nchi zote za jirani zina matatizo
Napenda kuheshimu maoni yako lakini utakuwa hukunitendea haki kusema kuwa dhamira yangu ilikuwa 'kosa kulelewa katika uislam'. Natambua kabisa kuwa mataifa yetu ya kiafrika ni maskini LAKINI Tanzania ni maskini kupindukia (we are below poverty line). Nchi kama Botswana na Namibia zipo mbali sana kutoka kwetu kimaendeleo, na Mwananchi mmoja wa Botswana alipohojiwa juu ya nini sababu ya mafanikio yao alisema hivi, 'There are people who think Botswana development is because of diamonds but if that is the reason, they need to understand that the same diamonds have been the cause of war and subsequently a source of poverty. If there is a reason behind Botswana achievement then it is not natural resources but we have been lucky, since independence we are have been blessed to have good and visionary leadership'.
Pamoja na kwamba nchi zote za kiafrika ni maskini lakini karibu nchi zote, pamoja na zile ambazo sehemu kubwa ya maeneo yao ni majangwa, zimekuwa na maendeleo makubwa zaidi ya kiuchumi kuliko Tanzania yenye rasiliamali nyingi za asili.
Tusikimbilie kwenye ukabila, udini, n.k. Daima tuyaangalie mambo katika uhalisia wake, tukiweza kufanya hivyo tutakuwa katika nafasi ya kuona kama malezi ya watoto wetu yanawajenga kuelekea tunakotaka tufike au hapana, kwa sababu tusingependa na wao waje waishi kwa shida na mateso kama tulivyo sisi. Mimi naamini kuwa malezi yetu yana mchango mkubwa kutufanya hivi tulivyo, kama ni watu wazuri au wabaya. Hatua ya kwanza ya maendeleo ni kuyatambua mapungufu yako na kuweka dhamira ya kubadilika. Kama kuna makuzi katika jamii ya Pwani yanayozorotesha maendeleo ya watu wake, ni lazima tuyakubali ili tuweke nia ya kubadilika.
Amani na ustawi wa Taifa hili utategemea sana maendeleo na ustawi wa watu wake wote wala siyo kundi fulani. Tukisema kuwa watu wa Pwani huzipa uzito mkubwa sherehe (wenyewe huita shughuli) kuliko kazi siyo dharau au dhihaka bali tunaitaja hiyo kama kasoro katika ustawi wa watu wake, na hapa tunaangalia jamii kubwa ya Pwani ambayo ipo vijijini na wala siyo kundi dogo la wasomi wa Pwani ambao wameachana na tabia hizo.
Bwana Kalamazoo, mimi naheshimu sana imani za watu, siyo uislam tu bali zote. Na utambue pia kuwa kwa vile jamii kubwa ya wakazi wa Pwani ni waisam, viongozi wa dini ya kiislam wana nafasi kubwa sana ya kubadilisha makuzi ya watu wa Pwani. Kupenda sherehe kuliko kufanya kazi sidhani kama ni hitaji la dini yeyote. Kufanya kazi kwa bidii, sidhani kama kuna dini yeyote inayozuia hilo. Kuongea sana kuliko kutenda, siamini kama ni hitaji la dini yeyote. Tusipende kukimbila kwenye dini, hata kwa yale mapungufu yetu ya kila siku, ili ionekane kuwa kutotimiza wajibu wetu kama raia na kama wazazi ni hitaji la dini, na hivyo anayetamka kuwa tabia hiyo siyo njema anaishambulia dini fulani.