Mazingaombwe ya UVCCM yaendelea!!

Babu Lao

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
2,043
179
MAMBO yazidi kuwa magumu ndani ya jumuiya ya vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) na chama cha mapinduzi baada ya vijana sasa kutaka kuonyesha wazi kutumika kusafisha njia ya urais mwaka 2015 baada ya kuibuka kundi linalotaka CCM kuifuta UVCCM kwa madai kuwa imekuwa ni chimbuko la malumbano ya kukivuruga chama.

Pia kikundi hicho cha UVCCM mkoa wa Iringa kimeibuka na kutaka viongozi wote wa UV CCM ambao wamekuwa wakiongoza malumbano dhidi ya viongozi wa CCM wenye mamlaka ndani ya UVCCM kujiuzulu nafasi zao wanazozitumikia kwa wakati mmoja ili kuinusuru jumuiya ya UVCCM na kama njia ya kutoa nafasi kwa chama kuunda ama kuipika upya jumuiya hiyon ambayo imepoteza mwelekeo sasa na kuwa kama chama cha upinzani ndani ya CCM.

Tamko hilo la kupinga lililopewa jina la UV CCM irude kwenye misingi yake lilitolewa jana kwa waandishi wa habari na mjumbe wa baraza kuu la UVCCM mkoa wa Iringa Yusuph Mabena (pichani) kwa niaba ya vijana wenzake wajumbe wenzake wa baraza hilo waliokutana katika ukumbi wa Hoteli ya Ruaha mjini Iringa.
Hata hivyo tamko hilo limekuja zikiwa ni siku chache toka waziri mkuu mstaafu Frederick Sumaye na kuinyoshea kidole jumuiya hiyo ya UV CCM kuwa imekuwa ikitumika kwa maslahi binafsi kwa ajili ya kupanga safu ya wagombea wa nafasi ya urasi mwaka 2015 jambo ambalo ni kinyume na taratibu za chama hicho.

Mabena alisema kwa wao kama wanachama wa UV CCM na wana CCM wameamua kutoa tamko hilo ili kuwezesha kuifanya UV CCM kurejea katika misingi yake na tamko lao limelenga kukinusuru chama na sio tamko la kutumiwa na mtu yeyote ama mgombea wa nafasi ya urais mwaka 2015 kama wengine wanavyofanya.
“Mimi Yusuph Mabena ambaye ni mjumbe wa baraza la UVCCM mkoa wa Iringa nikiwa na wenzangu ambao ni wana CCM na wana UV CCM tunatoa tamko la kulaani mienendo yoyote ndani ya jumuiya ambayo inaonyesha kuitoa UVCCM katika misingi ya kuanzishwa kwa jumuiya na pia tunatoa tamko la kulaani mienendo yote ya UVCCM Taifa ambayo inaonyesha kwa,mba kwa sasa UVCCM imekuwa chama cha upinzani ndani ya CCM”

Mabena alisema kuwa ikumbukwe kuwa CCM inaweza kuwepo bila ya UVCCM na kuwa kama sio CCM UVCCM isingekuwepo hivyo kundi lolote linaloonyesha kupinga na kuishambulia CCM halina budi kufumbiwa macho na linapaswa kuogopwa kama ukoma .
“Ieleweke wazi kuwa jumuiya ya chama inayopinga chama hiyo tayari imejiingiza katika upinzani na inapaswa kushughulikiwa kwa kuhakikisha inavunjwa na kuundwa jumuiya ambayo ni msaada ndani ya chama vinginevyo CCM itajimaliza kwa kutumia jumuiya hiyo ya UVCCM ambayo ni inaupinzani mkali kuliko vyama vya upinzani….mtoto aliye tumboni akiamua kuua mama yake ni dhahiri ameamua kufa ….sasa kama humo tumboni kuna zaidi ya mtoto moja na hao wengine wanatama kuendelea kuishi na kumwona mama yao anaishi hawawezi kumwacha mwezao kuendelea na mipango ya kumuua mama yao watamshughulikia “
Hivyo aliwataka viongozi wa UVCCM Taifa kama wanakitakia mema chama kuacha mara moja kutoa matamko yasiyo na tija katika chama na kuwa iwapo wataendelea na matamko hayo basi wajue wazi kuwa wao kuwa hakuna vijana watakao waunga mkono kwa kuacha waendelee kuua chama hicho.
Hata hivyo alisema kuwa uongozi mbovu wa UVCCM Taifa ndio ambao umesababisha CCM kupoteza majimbo mbali mbali ya uchaguzi mwaka 2010 kutokana na kupanga safu yao ya kitaifa kwa ajili ya kuzunguka majimboni kufanya kampeni na kuwaacha vijana ambao ni wenyeji wa majimbo husika jambo ambalo lilipelekea vijana waliotengwa kugeuka wapinzani ndani ya CCM.

Hivyo alisema kuwa iwapo malumbano ya UVCCM na viongozi wastaafu ndani ya chama na viongozi wa CCM yataendelea basi ni vema UVCCM itamke wazi kuwa si jumuiya ya CCM bali ni chama cha upinzani ndani ya CCM na kusajiliwa rasmi .
Kwa upande wake mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa Fadhil Ngajilo alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi juu ya tamko hilo alisema kuwa ni utovu ni nidhamu na kuwa kupitia vikaoa vya UVCCM wataamua cha kufanya .
Alisema ni kinyume cha chama kutumia vyombo vya habari kutoa mambo ya chama na kulitetea baraza la UVCCM Taifa ambalo lilitumia vyombo vya habari pia kuwashambulia baadhi ya wastaafu na viongozi wa chama kuwa lilifanya hivyo baada ya viongozi hao kutangulia kutumia vyombo vya habari kutuhumu UVCCM .
“Tunataka wana CCM wafuate taratibu za vikao sio kwenda katika vyombo vya habari kukishambulia chama ama UVCCM kwani kuna vikao kuanzia kata hadi Taifa ambavyo vinaweza kuwasikiliza “
Hata hivyo alisema kuwa wanachama ni wajumbe wa vikao vyote CCM japo wapo baadhi ambao wamekuwa mstali kukokosoa chama hadharani,
Kwa kuwa viongozi walitangulia wasema hadharani ndio sababu ya baraza kutoa tamko lile la kwanza la kulaani ili kuepusha shari.

Hata hivyo alisema kuwa kutokana na UVCCM na CCM inaendeshwa kwa misingi ya vikao wale wote wanakiuka misingi hiyo watashughulikiwa kupitia vikao.

Imeandikwa na Francis Godwin kutoka Iringa
 
Ni kawaida yao....mimi kwa sasa uwa nasoma habari zao na kuzipuuza....
 
Tumewachoka kwani wote ni walewale kasoro makundi tofauti ndani ya nyumba mbovu!
 
Mbona Tender (Tendwa) yupo kimya? anasubiri nini? kwa nini asikufute? au anasubiri bwana wake ampe maelekezo?. Hiki sio chama bali ni genge la wahuni ndio wanaoongoza nchi. Futa CCM isiwepo kabisa Tanzania, hili genge ndio kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya taifa letu.
 
waacheni wamalizane ..sie yetu masikio tuendelee kukilea chama chetu ...P's...P..er!
 
1:MBONA MNATUKANYAGA WENGINE KAMA MAJANI? 2:MBONA WEWE UMESEMA? 3:HERI MIMI SIJASEMA! Wote walikufa so is ccm!
 
Ee mungu baba yetu mkuu wa yote tuondolee huyu ccm anaenda kinyume na matakwa yko.ni fisadi mwizi jambazi na amesababisha vilio kwa wengi. Watu wanakufa njaa kwa ajili yake. Alaaniwe na wengi baba sikia kilio chetu wananch wanyonge tuondolee huyu agent wa shetani asiyekuwa hata na chembe ya woga juu yako mungu baba
 
Back
Top Bottom