Mazingaombwe ya Polisi na Uhamiaji: Mke wa Askofu Mkomba amlilia Kikwete

RealMan

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,367
1,388
SIKU moja baada ya gazeti la Tanzania Daima kuandika habari ya kupotea kwa Askofu wa Kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship, Mulilenge Mkombo na polisi kukanusha, mkewe Gilina Mkombo, amejitokeza na kumuomba Rais Jakaya Kikwete aingilie kati.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Gilina Mkombo alisema familia yake haijui ni kwa nini mumewe apewe mateso makubwa kwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi ambalo amedai linashirikiana na Idara ya Uhamiaji.

Alisema si kweli kwamba Askofu Mkombo ameachiwa huru tangu Jumatano kama polisi walivyonukuliwa na gazeti hili toleo la jana, bali askofu huyo ameswekwa rumande, kwenye Kituo cha Polisi Tazara, huku akiwa mgonjwa na hapatiwi matibabu yoyote.

Alisema pamoja na kutompatia matibabu yoyote, Jeshi la Polisi limekataa dhamana kwa askofu huyo licha ya mke wake na nduguze kujitokeza kumdhamini.

Aliongeza kuwa baada ya kutomuona kwa muda walipelekewa taarifa na wasamaria wema kuwa Askofu Mkombo ameswekwa rumande katika kituo cha polisi Tazara huku hali yake ikiwa mbaya.

"Tulipoelezwa hivi tulikwenda pale Polisi Tazara na kweli tukamkuta, amewekwa rumande, tukazungumza naye akatuambia mambo ambayo kwa kweli yalituacha midomo wazi," alisema Gilina.

"Mume wangu aliniambia kuwa baada ya kutolewa gerezani, alipakiwa kwenye ndege ya Shirika la Kenya (KQ) wakipitia Nairobi, Kenya, Ndola, Zambia na baadaye kutua Lubumbashi, nchini DR Congo, kisha maofisa wa Uhamiaji na askari polisi waliomsindikiza wakamtaka ashuke wakimwambia amefika kwao," anasema.

Aliongeza kwa kuwa hakuwa na nyaraka zozote, mamlaka ya DR Congo uwanjani hapo ilikataa kumtambua wala kumpokea, kuona hivyo wakaamua kumpeleka mjini Kinshasa, lakini huko nako wakaulizwa nyaraka zenye mihuri ya balozi wa DR Congo nchini Tanzania lakini hawakuwa nazo hivyo nako akakataliwa ikabidi warudi naye.

Anasema baada ya kukataliwa na serikali ya DR Congo, walirudi naye na baada ya kushuka Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere walimpeleka hadi kituo hicho cha Polisi Tazara na kumtupa ndani anakoshikiliwa hadi sasa bila kupelekwa mahakamani.

Alimuomba Rais Jakaya Kikwete aingilie kati suala hili na kumuokoa Askofu Mkombo ambaye chuki za makanisa zinasababisha ateseke na sasa anakaribia kufa akiwa katika vyombo vya dola ambavyo amedai vinatumiwa na watu wanaolionea wivu kanisa lao.


Source: Tz Daima
 
Mhh,wanalionea wivu kanisa lao?imekaaje hii ama alikua ameangia kwenye politic ama subversion sababu hadi watu wahangaike kumrudisha kwao ujue kuna namna hapo
 
Mhh,wanalionea wivu kanisa lao?imekaaje hii ama alikua ameangia kwenye politic ama subversion sababu hadi watu wahangaike kumrudisha kwao ujue kuna namna hapo

Inashangaza namna linavyopelekwa.
Tanzania hii unaweka ukaka bila kibali cha msingi usiguse masilahi ya watu.

Inawezekana huyu bwana ameingia kwenye anga za watu
 
Hii thread kama siielewi vile....inamuonea huruma mkongo aliyeishi kiharamu huku ikilaumu polisi kwa kutaka kumrejesha kwao? Sijui sisi tunachotaka hasa ni nini.... wahamiaji haramu wakiachwa...shida, wakishughulikiwa ..., tabu! Tunataka nini?
 
La msingi watueleze amefanya kosa gani??,maana kama ni uhamiaji haramu ishu ilikuwa ni wahusika kumshtaki then mambo mengine yatafuata!!
 
Hii thread kama siielewi vile....inamuonea huruma mkongo aliyeishi kiharamu huku ikilaumu polisi kwa kutaka kumrejesha kwao? Sijui sisi tunachotaka hasa ni nini.... wahamiaji haramu wakiachwa...shida, wakishughulikiwa ..., tabu! Tunataka nini?

Mi nafikiri sheria lazima zifuatwe, apelekwe mahakamani ikionekana ameiingia nchini kinyume cha sheria basi sheria zote za kumrudisha kwao zifuatwe au siyo mkuu na wala siyo kupelekwa pelekwa tu.
 
Back
Top Bottom