Mazee MAPESA kwa hili ulichemsha!

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
Wakuu,

Juzi mzee Mapesa alinichefua kiasi nikasema huyu mzee amekosa mwelekeo?, badala ya kujibu hoja ya msingi ya mbunge kijana Lissu yeye anakurupuka na kutoa lugha za matusi katika chombo kikubwa kabisa cha kutunga sheria nchini , hivi sheria zinatungwa kwa matusi? huyu mzee tumweke kundi lipi?

Mhe. Lissu alikuwa analieza bunge athari za kupitisha kanuni hiyo mpya huku alitoa mifano ili wabunge waelewe, lakini babu yangu akakurupuka na kurusha kombora sasa sijui ni kipi hasa kilichomuuma?

Hoja hujibiwa kwa hoja na wazee ndiyo mifano ya kuingwa na vijana, sasa mzee wa miaka 70 ukianza kutoa mitusi bungeni je kina Mnyika, Halima na wengineo vijana wajifunze nini? je hukuwa na maneno mengine ya kutumia badala ya hayo uliyoona yanafaa?

Kwa lugha yako chafu hukuwa mnamdhalilsha Lissu wala CHADEMA bali wewe mwenyewe na chama chako chenye mbunge mmoja. Binafsi umenikera sana tena mno nyie ndiyo wazee wetu tunawategemea kuliongoza taifa letu matokeo yake ndiyo mnakuwa msatari wa mbele kujikomba komba na omba omba visenti kusaidiwa saiwa tu na serikali, je mkipewa hizo kamati mnazozililia mtaziongoza inavyotakiwa? mimi nafikiri mtakuwa mnarudisha fadhila kwa serikali kwa kuficha maovu yapite.

ngoja ninywe maji nipunguze hasira kwanza... nakuja.
 
Huyo mzee aliona kitumbua chake kinaingia mchanga. Ndo maana akawa anatukana hovyo. Binafsi kauli yake ilinikera basi tu, ila time will tell watu tunawaona wataishia kubaya.
 
Mimi simlaumu Cheyo, lawama zangu ni kwa huyu spika zao la mafisadi anayerusu bunge kugeuzwa kijiwe cha mipasho
 
Wakuu,

Juzi mzee Mapesa alinichefua kiasi nikasema huyu mzee amekosa mwelekeo?, badala ya kujibu hoja ya msingi ya mbunge kijana Lissu yeye anakurupuka na kutoa lugha za matusi katika chombo kikubwa kabisa cha kutunga sheria nchini , hivi sheria zinatungwa kwa matusi? huyu mzee tumweke kundi lipi?

Mhe. Lissu alikuwa analieza bunge athari za kupitisha kanuni hiyo mpya huku alitoa mifano ili wabunge waelewe, lakini babu yangu akakurupuka na kurusha kombora sasa sijui ni kipi hasa kilichomuuma?

Hoja hujibiwa kwa hoja na wazee ndiyo mifano ya kuingwa na vijana, sasa mzee wa miaka 70 ukianza kutoa mitusi bungeni je kina Mnyika, Halima na wengineo vijana wajifunze nini? je hukuwa na maneno mengine ya kutumia badala ya hayo uliyoona yanafaa?

Kwa lugha yako chafu hukuwa mnamdhalilsha Lissu wala CHADEMA bali wewe mwenyewe na chama chako chenye mbunge mmoja. Binafsi umenikera sana tena mno nyie ndiyo wazee wetu tunawategemea kuliongoza taifa letu matokeo yake ndiyo mnakuwa msatari wa mbele kujikomba komba na omba omba visenti kusaidiwa saiwa tu na serikali, je mkipewa hizo kamati mnazozililia mtaziongoza inavyotakiwa? mimi nafikiri mtakuwa mnarudisha fadhila kwa serikali kwa kuficha maovu yapite.

ngoja ninywe maji nipunguze hasira kwanza... nakuja.

sio hili tu huyu mzee anachemka kwa mambo mengi tu mbona...ananiudhi
 
Bora Cheyo kuliko Lissu,Lissu hana nidhamu kabisa!

Nidhamu ni kitu gani kwani? Kwa hali ilivyokuwa pale Bungeni juzi, Mh.Tundu alipaswa kusema/kufanya nini ili aonekane kuwa na nidhamu? Au hana nidhamu tangu zamani?
 
Bora Cheyo kuliko Lissu,Lissu hana nidhamu kabisa!

Heshima kwako Dyslexia,

Kila mtu ana uhuru wa kuongea atakavyo lakini wakati mwingine ni vyema ukatoa majibu pasipo shaka yoyote balada ya kubwatuka.Lissu ni mmoja wa wabunge wa CHADEMA ninaowatarajia kufanya mambo makubwa ndani ya jengo letu idodomya.
 
Nidhamu nini?
Ndiyo mzee kila kitu?
Kusema mambo ya kufurahisha watu tu?
Uoga?
Zao la mafisadi nidhamu maana yake "Kubali yote usipinge chochot"
 
Back
Top Bottom