Mayaula Mayoni amefariki

saitama_kein

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
981
99
Mwanamziki mkongwe wa mziki wa dansi nchini toka nchini Kongo Kinshasa, Fredy Mayaula Mayoni (RIP) amefariki dunia siku ya 27-05-2010 huko jijini Brussels, Ubeligiji, kwa ugonjwa kansa ya ubongo (brain trumour).

Marehem Mayaula Mayoni (64) ni mwanamziki aliyekulia na kusomea jijini Dar wakati wa utoto wake miaka ya 60s, kwani baba yake alikuwa ni moja wanadiplomasia katika ubalozi wa Kongo(Zaire) nchini Tanzania. Marehem pia aliwahi kucheza kandanda katika timu maarufu nchini Yanga(Young Africa) ya jijini Dar.

Vijana wa kizamani watamkumbuka marehemu Mayaula pale alipojiunga na bendi ya TP OK Jazz,iliyokuwa inaongozwa na gwiji Franco Luambo Makiadi, uko Kongo. Mayaula alijiunga TP OK Jazz baada ya kurudi kwao Kongo (DRC) na kujikita katika ulimwengu wa mziki ,ambako aliachia wimbo maarufu "Cherie Bondowe" au "Sherry bondowe", wimbo ambao ulimpa umaarufu sana.marehemu pia aliwahi kufanya kazi na mwanamziki ambaye pia marehemu Mpongo Love.

Mungu amlaze pema peponi Mayaula Mayoni
Amin

source: Michuzi​
 
Ngoja tujikumbushe vibao vyake vilivyotesa saana enzi zake akiwa hai:

1.Bondowe


2. Bondowe No.2
 
Last edited by a moderator:
Akiendelea kutunga wakati angali kijana mdogo kabisa. Huu wimbo wa Ndaya alitunga na kuimba kwenye background Vocal. Kwa kweli tutam-miss sana huyu jamaa.


Baadaye alirudi tena kwa nguvu miaka ya 90 na kuja kutesa kwenye karibu kila sherehe na huu hizi nyimbo mbili alizotunga yaani:



Ehh, jamaa nilisoma sehemu kuwa alikuwa Mhandisi wa Electronics kama sikosei.

Ngoja niweke album yake kwa kumbukumbu. Rest in Piece MAYAULA Mayoni Don P.
 
Last edited by a moderator:
RIP... Nyimbo zako zitaendelea kukuweka hai masikioni mwetu.
Hasa wimbo wa "Mbongou" au pesa kwa kiswahili.
 
Mkewe, Stella Amri tulikuwa pamoja Magomeni enzi za ujana wetu. Kama kuna mtu ana contacts zake naomba niwape pole.
 
Mkewe, Stella Amri tulikuwa pamoja Magomeni enzi za ujana wetu. Kama kuna mtu ana contacts zake naomba niwape pole.

Jasusi, hebu tumwagie zaidi historia za huyu jamaa. Kuna moja nimesoma kutoka kwa Mkongo mmoja na naiweka hapa:

The musician Freddy Mayaula Mayoni died this Wednesday, May 26, 2010 in Brussels at the age of 64 years, according to an announcement of the Congolese Lipopo Friendship, an organization based in the Belgian capital. This loss puts an end to a long period of sickness that ate away the deceased for several years.

According to our colleagues in the Congolese press, singer-songwriter "Ousamane Bakayoko"Suffering from right hemiplegia, from Tanzania, where he was staying, had been in first, return to Kinshasa in August 2005 with her son Dedy who was studying in South Africa. Mayaula who had lost the use of the word, seemed abandoned to its fate in the family home on May 20 at the headquarters in the town of Kalamu. After many SOS launched in his favor, the authorities had taken charge of his medical evacuation to Belgium and the medical costs entailed.
A prolific writer and talented guitarist left to posterity a rich repertoire, demonstrating his inspiration that crossed several times and trends in Congolese music. We can cite some timeless tracks "Honey Bondowe"A recovery that will be one of his early hits,"Nabali misery"" Libal Bombande complicated""Mummy"... that marked its passage through the group OK Jazz of Franco. Mayaula Mayoni was also with Empompo Loway and Lutumba Simaro, one of the mentors Mpongo Love singer for whom he wrote the song "Ndai"And will sing, years later,"Nasi Nabali"By Tshala Mwana.
From his solo career, as we note titles "Love the kilo," Ousmane Bakayoko "," Dom Padrino "," Dudu "," Mbongo " or "Kotik you", "Mamiwata", "Doudou mwen", "OBDP" from the album " Love kilo, Released in 1993 and produced the song with the assistance of Lassa Carlito and Pembey Sheiro.
Apart from his musical career, Mayaula was also a brilliant footballer. It had evolved from 1967 to 1971 the position of left winger football team V Club at the time chaired by Franco, who later became his boss in OK. Jazz. It was part of what the sports press had dubbed Congolese "attack machine gun" with Kembo, Mayanga and Kibonge Gento. Good dribbler and scorer, he has even been selected the national team, the Leopards in 1968

[AFRIQUECHOS.CH] : Adieu Mayaula Mayoni !
 
Wadau mmesahau kuwa kati ya mwaka 1970 au 1971 Fred Mayaula (RIP) allichezea Yanga walipocheza na a na Sunderland (Sasa Simba), aliibanjua Sinderland bao mbili yeye mwenyewe na kuipa Yanga Ubingwa wa Tanzania. Wakati huo kipa wa Yanga alikuwa Elias Michael (RIP) na Sunderland alikuwapo Hassan Mlapakolo kama sijakosea. Pia walikuwamo Yanga Gilbert Mahinya, Omari kapera, Juma Bomba, Maulid Dilunga (RIP), Athumani Kilambo, Kitawna Manara, Abdulrhaman Juma (RIP), Awadh Gesani. Sunderland walikuwapo pia Emanuel Albert (Bonge), Mustapha Choteka, Arthur Mambeta, Hamis Kilomoni
RIP Fred
 
RIP Mayaula. Thanks Sikonge...hiyo Bondowe imenikumbusha mbali sana.
 
RIP Mayaula, alikuwa rafijki yangu sana. Alipokuwa Dar tulikuwa tulikutana mara kadhaa pale Igongwe Bar wakati bado inamilikiwa na Bwana Sharifu wa Balozi Majaar.


Again, Tutakukosa sana Mayaula.

Sote tunaelekea huko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom