Mayai ya kienyeji /vifaranga wa kienyeji

ok, vipi hicho kizazi ni endelevu kweli? maana niliwahi zungumza na reseacher mmoja akanieleza hivyo.

Jaribio hili halina zaidi ya miezi 9 Sijajua itakuwaje baadae ila vifaranga wamekua na wamefikia kutaga ninawatunza kienyeji yaani wanatembea tembea nje.
 
Asante, Kariakoo bei yao kwa kilo ni sh. ngapi maana naona bei yao ni juu. Manzese huwa ndo nanunua pumba ila mashudu sijawahi ona manzese labda nijaribu ku-check vizuri.
Kuhusu hizo mbegu labda nikufanyie mpango wa kuzipata

mahitaji yako ya mashudu ni kiasi gani?na dagaa pia.
Niko karibu na source ya vitu hivo.
 
Mama Joe

Hawa kuku ni wa kienyeji, ninazo mbegu tatu tofauti (Kienyeji asili, Kuchi chotara na Rhode red island)
Kuhusu chakula kuna mtu alitaka mchanganuo kwa style hiyo ili apate mwanga kidogo ila kawaida kuku wa kienyeji hawaitaji chakula cha dukani japo wakila hicho cha dukani haina shida yoyote. Ndo maana pia nikasema gharama ya chackula itapungua kulingana na mahali na mahali, kulingana na upatikanaji.

Asante

Kuku wa "kienyeji asili" andiyo lakini asili ya wapi? Tanzania, Malawi, Msubiji au nchi nyingine yoyote ya africa, maana hawa wote ni asilia wanaotofautiana tu kwa sifa flaniflani kutokana na nchi husika mfano wengine wanene, wanataga tu hawaatamii, wanataga na kuatamia, miguu mirefu n.k.

Naomba pia kujua vifaranga vyako ni majike tu au na majogoo. Je unawtofautishaje majike na majogoo katk vifaranga vya umri wa siku moja?

Mkuu, kuku asili wa Tanzania. Vifaranga ni majike na majogoo kwa pamoja na kutofautisha wakiwa wadogo si rahisi sana.

Asante
 
Hebu tujuzeni kuhusu soko la kuku wa nyama chotara na mayai,maana kuna jamaa yangu hapa Atown kama miezi miwili hivi alikuwa anakaribia kuwehuka,mayai hayana soko......kuna mpaka mayai ya mchina yanaingia kwa bei chee kupitia Kenya
 
Kitu kimmoja nashindwa kuelewa. Hawa ni kuku wa kienyeji lakini naona malisho ni sawa na hao wa kisasa, sasa tofauti inakua vipi?
 
Kitu kimmoja nashindwa kuelewa. Hawa ni kuku wa kienyeji lakini naona malisho ni sawa na hao wa kisasa, sasa tofauti inakua vipi?

Duuh, samahani kuchelewa kujibu.
Kuku wa kienyeji anaweza kula vyakula vya dukani pia anakula chakula ambacho unatengeneza mwenyewe. Kikubwa ni kwamba hana masharti ya ulishaji kama wa kisasa.
 
Hello! Nina uhitaji wa MAYAI ya kuangulisha vifaranga wa broiler kwa yeyote aliye na info naomba anisaidie.
 
Wafugaji wenzangu hongereni,

Bado vifaranga wanapatikana na pia tumeongeza mbegu ya kenbro ktk kundi.
Unaponunua vifaranga kwetu unapata fursa ya kupata chakula cha kuanzia (Starter) hii ni kuhakikisha vifaranga wanaendelea kukua katika ubora ule ule.

Karibuni nyote
 
Kwa yeyote anayefanya biashara ya dagaa wa mwanza wa kuku na mashudu ya pamba, plz tuwasiliane
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom