Maximo unajifunza nini kuhusu kombe mabara

Grader

JF-Expert Member
Feb 23, 2009
445
64
Katika michuano inayoendelea kule kwa baba Mandela,mimi ni mfuatiliaji na mshabiki mkubwa wa mpira hasa kwa timu inayocheza mpira mzuri na kamwe sina uzalendo na klabu,dini,kabila wala nchi hata bara.
Je Maximo anajifunza nini kuhusu kinachoendelea kule south Africa kwani unaona utovu wa nidhamu uliofanywa na Misri hasa wachezaji wake kuvinjali na Vimwana wakati ni mwiko mkubwa wa soka ukiwa kambini.
vilevile Maximo asitumalizie pesa za Rais wetu akiwa anajenga cv mbovu kupita kiasi. Nina maswali mengi kwake;
1.Mbona cv yake iwe wazi kwani perfomance yake inashuka mpaka sas naona bora timu akapewa Mziray.
2.Mbona mikakati yake siyo endelevu.
3.Halafu mbona analeta ukabila na uzalendo kuwaleta nchini wabrazili wenzake kufanya kazi bila kujali cv's zao nzuri.
4.Mbona anabadilisha badlisha timu kila mara bira kujali uchezaji hebu ajifunze kutoka south Africa timu yao inavyojengwa.
 
Mkuu Grader nami nina swali , huo mpira wa taifa stars unaozungumzia hauna uendelevu jiulize ulianza lini kuonekana mpaka watu hasa wapenda soka wakavutiwa nao! mi naona mpira wa Tz bado haujafikia viwango hivyo mnavyofananisha na timu kubwa kama ya south au misri. Timu ya taifa imeanza kupanda chati miaka ya hivi karibuni. Inatakiwa tufike wakati wa kujadili uwezo wetu na tuangalie jinsi gani ya kuuendeleza na sio kujiweka kwenye mfanano na timu ambazo wao soka hawajaanza kulishughulikia leo. Huyu kocha mi siwezi kumlaumu coz wakati anakuja bongo kulikuwa hamna wachezaji ambao unaweza kusema ni wa kudumu timu ya taifa so inambidi aendelee kufanya hivyo kubadili timu mara inapombidi ili apate walau wachezaji kadhaa wa kuunda first eleven ya kudumu. Hilo suala la Maximo kuleta makocha from Brazil bila kujali cv zao ingependeza kama ungeweka data zaidi.
 
Tukiendekeza mawazo haya kwamba kocha wa taifa stars peke yake anaweza kuleta maendeleo ya soka hapa nchini hatutafika popote. Maximo amejitahidi kwa upande wake, vilabu vyetu ambavyo ndio tunategemea viwe kiwanda cha aji wa kuchezea timu ya taifa vimefanya nini? kila siku ni malumbano, majungu, fitna na ubabaishaji mwingi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom