Maximo needs to go

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,200
79,433
Ni zaidi ya miaka mitatu kocha huyu wa Kibrazil anaendeleza ubabaishaji najua anaweza kudai ati wachezaji wanakosa professionalism lakini hiyo si sababu kwa vile Uganda imeshinda kikombe hiki cha Cecafa Challenge kwa kutumia wachezaji wanaochezea ligi ya Tanzania! Hii inamaanisha ana wachezaji wenye viwango vya kutosha wakiwemo wanaowaweka benchi hawa wachezaji wa Kiganda kwenye ligi ya bara!

Suala ni kuwa Maximo hana ujuzi zaidi ya alipotufikisha tunahitaji mawazo mengine kuinua soka letu maana huyu baba inaelekea anabahatisha na pata potea yake!
 
Ni mzigo mwingine kwa soka la tanzania.
 
Aende tuu........uwezo hana....anakomaliaa ninii si aende tuuu??????/
 
Angekuwa kocha kweli mwenye uhakika na taaluma yake angekuwa ashaondoka huyu!!!!!!!
Anajua kuwa akiondoka hapa bongo hawezi pata kibarua popote pale.
 
This is my txt msg 2 Maximo....

''Ahante Maximo kwa kuinua soka la Tanzania. Kwakuwa uwezo wako umefika mwisho, bora ujiondokee, usisubiri kufukuzwa. Ukifukuzwa utajisikia vibaya na heshima yaki itashuka zaidi. Tafakari ... chukua hatua''
 
Maximo ni takataka na wala hana muda wakubabaisha watanzania tena.
Labda akae kwa manufaa ya CCM
 
Maximo hawezi kwepa lawama kwa performance mbovu ya timu yetu kili stazs. Kwanza amesababisha wachezaji especially mabeki wapewe red card kutokana na mfumo wake wa uchezaji (defensive game). Timu inapocheza mchezo wa kujihami mabeki wanalazimika kucheza physical game (yaani kutumia nguvu) na hii inapelekea kucheza faulo kiurahisi then yellow cards alafu red card.

Timu ilikuwa haichezi i dont know what is wrong wit maximo!. Naunga mkono amefikia mwisho hana jipya analoweza fanya
 
This is my txt msg 2 Maximo....

''Ahante Maximo kwa kuinua soka la Tanzania. Kwakuwa uwezo wako umefika mwisho, bora ujiondokee, usisubiri kufukuzwa. Ukifukuzwa utajisikia vibaya na heshima yaki itashuka zaidi. Tafakari ... chukua hatua''

Translation either in English or Portugues, Masikio is no Good in Swahili! then mtumie
 
huyu jamaa sio siri muda wake umefika, ila kwa jinsi serikali yetu ilivyo atabaki mpaka amalize muda wake coz nadhani pia itakuwa ni njia mojawapo ya mkuu kutoka next yr kwenye election....... ooh mi nilileta kocha akainua kiwango cha soka......., ..watu makofi tafadhali.........
 
atarudi na kutoa sababu kibao sijui vijana wamecheza vizuri,timu haikucheza mechi za majaribio..blh blah...

atakwenda Brazil likizo na atarudi kutengeneza hela za bure...tunalalamika humu ndani lakini wote tunajua Maximo atabaki tuu...ujnga mtupu...ahhh ananiboa tuuuuuuuuuuuuuuu
 
Mlioko dar tunaomba jibu kama maximo kaja dar au kapanda ndege ya kwenda kwao halafu mabag atatumiwa..
 
Hivi tatizo ni maximo kama kocha au nimichezaji yenyewe??? nashindwa kuelewa. Jamani hapa kuna suala la kujituma, naona wachezaji wetu hilo hawalijui. tutakalia kulaumu Makocha na kuwafukuza kumbe tatizo ni michezaji yetu, hata Rwanda ambao ni mayai wametufunga???????????? Kazi kwenu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom