Maximo Kocha Mpya Yanga

Mhhh kazi kweli kweli........jiwe walilolikataa vibarua limekuwa jiwe la pembeni..............kahangaika kutafuta timu weee kakosa ndo anarudi Yanga......duuu bora hata angeenda hata Abajalalo.....
 
Jamani Maximo hana uwezo Yanga mnapotea yule ni mhamasishaji wa mazoezi hana lolote,na yeye njaa zake zitamuumbua anakuja kumaliza jina lake kabisa shauri yake angejipoteza kabisa abakie na sifa asizokuwa nazo analotafuta atalipata!!alionja kuku wa kienyeji ndio wanaomrudisha si mpira maana hana kiwango!!
 
Maximo alizoea timu ya Taifa ambayo alikuwa na wigo mpana wa kuchagua wachezaji, sasa nyie mnataka kusajili 30 tu halafu ndo awe anaogelea kwenye idadi ndogo namna hiyo huyo ndo mtamfukuza kabla hata msimu haujaisha, wanaosema wachezaji walikuwa hawajui kupiga pasi mnaongelea wachezaji gani, humu humu kuna uzi unaongelea malegend kama Masha, sana sana alimtoa tu Tegete inabidi aongezewe mkataba tena ili aendane na Maximo. Wachezaji wengine mnaotakiwa kusajili ni kina Dihile, Mwarami, Henry Joseph, Ivo na wengine vipenzi vya Maximo, namuonea huruma ndugu yangu Chuji lazima apigwe benchi, akija na kiingereza chake kile, I want players who are patriotic, displined and Young that can determine the future of Dar Young Africans Club, huku nyie mshachukua mijamaa ina miaka kibao.
 
Yebo mnatiishaa! Mbwana Samata, Drogba, Okwi, Sunzu, yo-nje wote jangwani. Du jangwa limegeuka bustani.
 
Mbwana samata anakuja next week kumwaga wino mkuu!

Hata Okwi anaweza kusainishwa pia. Shs bilioni 2 kwa Manji ni hela ya chai tu. Ona alivyomfanya Yondani na sasa anavyoivuruga Simba sasa...... Pesa ni balaa.
 
Kinachonishangaza ni why Yanga ikifanya kweli ninyi mashabiki wa simba mnachonga?kwa taarifa yenu kaseja kajileta wanaume wamemchomolea.
 
Mkataba ni wa miaka mingapi? Kwa Yanga niijuayo itakuwa vigumu sana Maximo kumaliza mkataba salama.

Hawajazungumzia mkataba ila inaonekana kwa kuanzia atakuwa nao mpaka Kagame Cup. Anakuja na mkewe.
 
Kudadeki lazima simba wapakatwe chezea pesa wewe.Manji tunakutakia maisha marefu.Ubingwa wa Afrika huo unanukia
Sema hivi fisadi tunakutakia maisha marefu.....ama kweli mwanaume alie mbaka mama yako ndiyo ukazaliwa utake usitake utamwita baba tu....hahahah
 
Back
Top Bottom