Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

Tanzania Railway Stesheni, ilimtoa baba ako kijijini
ikamleta mjini, kwa senti ishirini
kuikashifu ya nini, kwani imetutoa mbali
tusidharau mbachao, kwa msala upitao

Mh,acha bhana,...yaani unataka kusema
hahaha,TRC oyeeee!
Wahindi noma,yaani wameua shirika wakafundisha wafanyakazi
mashairi duh
 
Kwa heri magulumangu, muda wa kinywaji umewadia
ninatoka nyumbani kwangu, kwenda kusalandia
sisahau kipochi changu, starehe kwenda lipia
maisha ni safari, ishi upendavyo nakwambia
Duh! kwa kweli umenifurahisha sana mrembo, kumbe na wewe wamo ki hivi? keep it up
 
Mh,acha bhana,...yaani unataka kusema
hahaha,TRC oyeeee!
Wahindi noma,yaani wameua shirika wakafundisha wafanyakazi
mashairi duh

Hindi haiko jua shairi bebe...iko kura tambuu tu...kwenda wewe sako...
 
hhaaa,mi nashangaa sana, nilikuwa siipendi malenga..lakini hapa ni kiboko....magulumangu kama Andanenga vile..kila comment ina shairi lake..namie naomba unijbu kwa shairi, wewe na Shantel..mpo juu,na kilio chenu chasikika.
 
Nia sikuwani nayo,menijia hili jambo,
si mgema nia ninayo,sifa tiwa maji tembo,
sinziga bahati unayo,usicheze nayo fimbo,
Shanteli akipata wanja,malengani bado wapo,

Sio kwamba nakuponda,ndo vina baba vilivo,
sijali wala kukonda,mwendo dundo ka volvo,
mesahau langu tanda,malenga mpaka naivo,
Shanteli akipata wanja,malengani bado wapo,

tutaimba na kikwetu,mwadila baba gawiza,
muiteni wetu jetu,asipende bangaiza,
ana sumu kama chatu,vina vyake bila hiza,
Shanteli akipata wanja, malengani bado wapo.....
 
i can guess, magulumangu yuko likozo, manake akibanwa huptea kabisa humu.

hongera kwa kupata likizo mpendwa!
 
Sugu wetu malaria,Aspirini dawa yake,
Babukijana silia,unga mkono babake,
Quinine sijetupilia,Field masha iwe mwake,
Maxence nakuomba,nipe na mimi uwanja,

Magulumangu dimbani, hongera nakupatia,
Kwa kuniweka kundini, kuishinda malaria,
Ila huyu wa jamvini, Amelogwa atakua,
Klorokwini kamshinda, Aspirini nitaweza?

Labda kikombe cha babu, tena kwa kufakamia,
Asinyweshwe kwa adabu, hatapona malaria,
Tena afungwe bawabu, asije akakimbia
Huyu Malaria Sugu, Mimi ameshanishinda.
 
i can guess, magulumangu yuko likozo, manake akibanwa huptea kabisa humu.

hongera kwa kupata likizo mpendwa!

Judith umenishusha dear sijaona umenitupia angalau mistari minne hivi, hujasoma kilio changu kwa maxence? Unga mkono kwa mistari dada
 
Magulumangu dimbani, hongera nakupatia,
Kwa kuniweka kundini, kuishinda malaria,
Ila huyu wa jamvini, Amelogwa atakua,
Klorokwini kamshinda, Aspirini nitaweza?

Labda kikombe cha babu, tena kwa kufakamia,
Asinyweshwe kwa adabu, hatapona malaria,
Tena afungwe bawabu, asije akakimbia
Huyu Malaria Sugu, Mimi ameshanishinda.

Kikombe bila imani,malaria hajapona,
Hata ale krokwini,kamwe hajajakupona,
juju pia haijani,ni naija hata ghana,
Tumwache ile kichwani,Itatoka kwa maombi,
 
Back
Top Bottom