Maxence Melo: Wamiliki wa JamiiForums ni Watanzania wanaoitumia

Big up moderators ole wao wanaodharau maoni yetu na kutuita wahuni huku wakiuza nchi yetu kwa wawezekaji.

JF ndio mahali pekee pa kutolea madukuduku yetu,sisi wengine ni wanyonge hatuna uwezo wa kushawishi magazeti na vyombo vingine vya habari waandike malalamiko yetu ,lkn hapa tupo huru.

Mfano ni jambo la kushangaza kuona kuwa deni la taifa linapanda mara mbili kwa mwaka mmoja bila maendeleo yoyote kuonekana alafu tumsikilize mchemba na upuuzi wa takwimu.

Watanzania sasa tunauelewa mkubwa wa mambo kuliko miaka 5 nyuma, tunaona namna ambavyo watawala wanataka kulazimisha wapendwe wakati sisi tunashinda njaa wao wanakopa fedha badala ya kuzitumia kwa maendeleo wanatanulia kwenye posho na safari za nje kila wiki.

Long live JF tutasema ukweli bila kumuonea aibu mtu wala kumuogopa Tanzania ni yetu sote na yao
 
Nitajisikia vema, siku BC wakimchukua maelezo mmoja kati ya ma-moderator wa Jukwaa la siasa, 'mh Paw':rain:
 
Peoples' power!!!!
282223_336227283119272_90601204_n.jpg

duh! umetoa wapi hii, aisee ni kali
 
'Trending' ya siasa ndani ya Tanzania ndiyo inapelekea mijadala kuonekana kui-favor CHADEMA. Lakini ukiangalia kwa sasa hali inavyoelekea mwaka 2012 CHADEMA inaweza kupita kwenye wakati mgumu kuliko wakati wowote; hata hivyo ni endapo hawataweza kuling'amua hili na kulifanyia kazi. JF as JF haitozuia mjadala endapo ya CUF yatawakuta CHADEMA, ndo uhuru wa kujieleza huo, na kama kutakuwa na 'facts' basi huwezi kuzuia mjadala.

Hapa ndo sijamuelewa kabisa Maxence anamaanisha nini. Nimesoma repeatedly, six times...Cjang'amua
aliyemuelewa tafadhali?
 
Hongera sana Founder na waendeshaji wengine. Nice interview Maxence Melo, Big up.
 
Watu makini waliosoma topic hii yapo mengi ya kujifunza na kurekebisha mawazo yao na kubadilika. niwapongeze kwa dhati kwa hii thread, Mabadiliko huanza na mimi
 
Hapa ndo sijamuelewa kabisa Maxence anamaanisha nini. Nimesoma repeatedly, six times...Cjang'amua
aliyemuelewa tafadhali?
Dumelang, ukitaka kuelewa hapo palipo kusumbua usiisome kimtindo wa isolation... isome in relation na paragraph yote ambayo inahusu CDM. Ukisoma the above para toka hio para ya Trending utatambua kuwa hio ambayo hujaelewa ni point of opinion ya mhusika.

Kwamba tokana na matukio mbali mbali na baadhi ya tabia ya baadhi ya wanachama wa CDM wanaweza jikuta wana wakati mgumu kuliko vile ambavo wanafikiri itakuwa. For ni common knowledge kuwa wahusika na wanachama wa CDM wapo confident hadi wanakuwa over confident kuwa ushindi ni wao no matter what... wakisahau kuangalia wapi wanakosea waweze rekebisha mapema ili kuepusha kuwepo kwa unavoided obstacles. Walau mimi ndio nimeelewa hivo...

CHADEMA:
Kinachoipa CHADEMA credit kwenye social networks nyingi (si JF pekee) ni uharaka wa wao kujibu hoja wanapoona imelengwa kwao. Wengi wamejisajili kwa majina yao halisi na wanakuwa ‘active’ kwenye ‘hot issues’. Dr. Slaa, Zitto, Mnyika na Dr. Kitila Mkumbo ni baadhi watu toka CHADEMA ambao wako active JF. Lakini, kukubali kwao kukosolewa na kujibu pale wanapoweza ndiko kunakowafanya wengi wajikute wanakishabikia chama chao. Nina wasiwasi kuwa hata hao wanaowashabikia hawana kadi za CHADEMA.

Kifupi:
‘Trending’ ya siasa ndani ya Tanzania ndiyo inapelekea mijadala kuonekana kui-favor CHADEMA. Lakini ukiangalia kwa sasa hali inavyoelekea mwaka 2012 CHADEMA inaweza kupita kwenye wakati mgumu kuliko wakati wowote; hata hivyo ni endapo hawataweza kuling’amua hili na kulifanyia kazi. JF as JF haitozuia mjadala endapo ya CUF yatawakuta CHADEMA, ndo uhuru wa kujieleza huo, na kama kutakuwa na ‘facts’ basi huwezi kuzuia mjadala.
 
Waziri wa sayansi na technologia aliwahi kusema mmiliki wa jamii forum hafahamiki na alikiri kuwa mtandao huu umesajiliwa nje ya nchi je mmiliki wa mtandao huu ni nanii au kinanani
 
Wamiiliki wa JF ni Mwigulu Nchemba, Nape nnauye, Abrahamani kinana, Asharose Migiro, Mzee wa kilimo cha nyanya (Mangula) na yule mwenye sura ya kazi (Wasira).
 
Back
Top Bottom