Max - Malipo

payuka

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
829
127
Sina nia ya kuwaharibia hawa jamaa biashara, ila natoa angalizo kwa mtu ambaye bado hajaingia kwenye huu mkenge wa kununua mashine yao ....apige hesabu Nzuri.


Kwanza kabisa napongeza jitihada za Tanesco kujitahidi kuwasogezea wananchi vituo vingi zaidi vya mauzo la LUKU (TOKENS). Haya basi tuje kwa Max-Com Limited Company pale Millenium......Hawa jamaa wanatumia wafanyabiashara Katika Kuziuza hizi Mobile Vending Machine zao..Na utaratibu unakuwa kama ifuatavo:-
  1. Bei ya Mashine ni laki tano (Tsh.500,000) ambapo inatakiwa ku-sign contract ya miaka miwili na ukiterminate contract yao @ any time before the expiry of contract unarudishiwa 50% ya deposit yako (Laki mbili na Nusu)
  2. Baada ya hapo Unaanza kuuza Luku Pamoja na Vocha..( Hapa ndo kichwa Kinauma)- Luku unapata asilimia 1.5 and Vocha Asilimia 4% .....sasa ukianzia kwenye luku Mfano: Ukiuza Luku ya Milioni Moja (1000,000) faida yako inakuwa ni Tshs. 15,000 .......(Swali ni je ...unatumia muda gani kuuza Kiasi hicho cha Luku ...wakati huo huo Competition ni kubwa mtaani i.e. Kila mtu ana hiyo mashine)
  3. Mbali na hapo kuna zile karatasi ambazo unatakiwa uzinunue kutoka kwao ...kwa ajili ya ku-print risit ....paper roll moja inauzwa Tsh.2000
Lengo ni kushauri mtu yeyote anayetaka ku-invest kwenye hii biashara awe amejipanga....sio biashara ya kuleta faida yoyote .....Ni biashara inayosaidia kuvutia Customers endapo una business nyingine.
 
Biashara yoyote kabla hujaingia lazima ukokotoe faida na hasara! ukiona haikulipi achana nayo.
 
Nimejaribu biashara ya M-Pesa na Tigo pesa, naona hizi zinalipa sana! Nilitaka kujaribu na hii! Mmh..afadhali umenijuza! Kidogo ningeingia mkenge.
 
kuna msemo wanasema "ikiuma sema"

kwwli imeumana.... Acha hiyo kitu njoo tuuze sera za kuondoa ngla
 
ni kama ziada hasa kama unatoa mpesa na tigo pesa.mi inanilipa kwa voucher za ttcl broadband sana na hii ni kutokana na kujuana na watumiaji wa broadband mana nimechukua tenda za kuwa recharge kila mwezi luku hailipi kabisa labda na dstv kama unawatu unakula tenda ya kuwarecharge kila mwezi
 
Millenium towers WAPO

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Nasikia sikia tu kuhusu maxmalipo sizijui zinafanya kazi zipi na jinsi gani ya kuzipata wanajamvi hembu nsaidieni!!Na ni wapi exactly I can get it

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Natanguliza shukurani zangu za dhati.napenda kuomba kufahamishwa na kupanuliwa mawazo kuhusu hzi mashine za maxmalipo.wapi zinapatikana,bei zake na mengine kuhusu uzoefu wa biashara ya namna hyo.asanteni sana.
 
Natanguliza shukurani zangu za dhati.napenda kuomba kufahamishwa na kupanuliwa mawazo kuhusu hzi mashine za maxmalipo.wapi zinapatikana,bei zake na mengine kuhusu uzoefu wa biashara ya namna hyo.asanteni sana.
 
2010,walikuwa wanatoa kamesheni ya asilimia 1.5,ya mauzo utakayofanya,na bado unatakiwa ununue karatasi za risiti,na kwenda bank kuweka pesa,kwa ufupi imekaa sana kama huduma na si biashara,we kwenye milioni moja,unapata elfu 15!labda kwa sasa wameongeza,ofisi zao zipo kijitonyama,ukipita kituo cha victoria,kuna gorofa opposite na blek point bar.kwa maelezo zaidi wasiliana na huyu jamaa ni mfanyakazi pale.0716953699
 
nlizitumiaga nkawarudishia sio kama selcom hawajitangazi but mashine zao ziko poa mfano maxmalipo ukiprint luku ikagoma badae inaprint wakati mteja ashaondoka nlikula hasara sana na hawa jamaa nkaamia selcom wako poa hamna usumbufu huo labda kama wamerekebisha madhaifu hayo kwa sasa
 
nlizitumiaga nkawarudishia sio kama selcom hawajitangazi but mashine zao ziko poa mfano maxmalipo ukiprint luku ikagoma badae inaprint wakati mteja ashaondoka nlikula hasara sana na hawa jamaa nkaamia selcom wako poa hamna usumbufu huo labda kama wamerekebisha madhaifu hayo kwa sasa

du hebu niambie mkuu vp selcom wana m pesa tigo na airtel money na wanalipaje faida?
 
Habari wakuu,
nimekuwa nikisikia matangazo kuhusu mashine za max malipo za kampuni ya Maxcom (T) Ltd, Lakini sielewi bado ufanyaji wake wa kazi hasa suala la huduma za kifedha kama vile mpesa, tigo pesa n.k
hivi ukiwa na hiyo mashine je bado kuna shida ya kutafuta laini (sim card) ya uwakala au inakuaje?
Pia kama kuna mtu anafahamu ufanyaji wa kazi nyingine za mashine hii anitoe ushamba tafadhali.
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom